Hayati Magufuli alionesha mara kadhaa kuwa ni mgonjwa wa moyo

Hayati Magufuli alionesha mara kadhaa kuwa ni mgonjwa wa moyo

Amekaa aka 5 tu madarakani impact yake ya maendeleo tumeiona kwa macho.Mungu amlaze pema peponi......
Yy aliyemuumba alikuwa na makusudi yake jina lake lihimidiwe.....
wale wazee wa kuchonga ngenga mnaweza kuendelea haina kwere
Na wale wazee wa mi5 tena + aongezewe muda vipi? Wakati unapanga yako na ALLAH anapanga yake, marehemu hasemwi kwa mabaya dini inakataza
 
..watu waliodai kuwa Magu ni mzima anachapa kazi ndio unawaamini?
Ndivyo walivyo Watanzania, kwa uongo, unafiki na uzandiki hawawezekani!

Kwa nini tuwaamini wanaodai alikuwa mzima anachapa kazi ingawa alikuwa hajaonekana kwa zaidi ya wiki tatu?
Kwa nini tuwaamini wanaodai alikuwa mzima hadi kuweza kuongea nao kwenye simu siku moja kabla ya dunia kutangaziwa kifo chake?
Rais wetu mpya naye hakubaki nyuma, kwa nini alidai aliongea naye akiwa Tanga lakini baada ya muda si mrefu akatangaza kifo chake!

Mtu hajiulizi kwa nini Wakenya wanaosema alikuwa mgonjwa tusiwaamini? Kwa nini wadai alilazwa Nairobi kama si kweli?
 
Pamoja na majonzi ya kuondokewa na mh. Rais lakini ni vema tukakumbuka maisha aliyoishi.

Magufuli kwa kutambua kwamba ana maradhi yasiyotibika alienda kupata kikombe Cha miujiza kwa Babu wa Liliondo . Baadae iligundulika kwamba kikombe kile ulikuwa usanii tu hivyo JPM aliendelea kuwa mgonjwa.

Pili kwa kutambua kwamba ana matatizo ya moyo- Magufuli Mara kadhaa amekuwa akijiepusha kushiriki katika masuala ya simanzi Kama misiba kwa sababu za kiafya.

Hi misiba ya karibuni hasa wa Balozi Kijazi bila Shaka ilimuathiri sana Magufuli.

Naamini si CORONA Wala Mabeberu

Alale salama.
Ukishakuwa mgonjwa wa moyo hauruhusiwi kuugua ugonjwa mwingine, kumbuka kuna magonjwa nyemelezi yanayowapata wadhaifu ikiwa pamoja na Korona.
Mbona mnahangaika sana!
 
Magu alikuwa na matatizo ya mooyo tangu mwaka 1991 hivi. Tarehe 28 February 2021 aliposhauriwa na madakatari ajipe mapumziko asifanye kazi, yeye aliendelea kufanya kazi na hivyo kukiuka ushauri wa madsakari jambo ambalo linaweze kuwa limecost maisha yake. Mawaziri wote waliosema alikuwa akiendela na kazi walikuwa right, ila huenda bila kujua kuwa jamaa alikuwa akifanya kazi kinyume na ushauri wa madaktari wake
Hizi pacemaker huwa zinahitaji kubadilishwa kila baada ya miaka 6 au 7 hivi.

Kuna risks za kutumia hivi vifaa bila kuchukua tahadhari.

1. Mgando wa damu kwenye sehemu ya kifaa hadi kwenye mkono ulio upande wa moyo. Kuna siku (hivi karibuni) akiwa kwenye ziara zake utamwona akiwa na bandage mkono wake wa kushoto.

2. Infection au au wadudu kushambulia sehemu iliyo na kifaa. hali hii hutokea miezi 12 tangu kifaa kipya kipandikizwe. Hivyo inawezekana kifaa kilipandikizwa miezi 12 ilopita. Moja ya dalili za infections ni joto kali na ndo ukaona feni yatumika kila mara.

Hii infection isiposhughulikiwa hupelekea mgonjwa kupata homa ya mapafu (Pneumonia) kuzunguka sehemu ya moyo na njia za damu kwenda kwenye moyo.

3. Kifaa hiki kikipandikizwa vibaya na kukawepo nguvu kubwa basi husababisha kuweo njia za wazi (air leak) ambapo hewa hujipenyeza kwenda kwenye mapafu. Hapo ndipo huitajika upasuaji kuondoa hewa ya ziada.
Hivyo hupenyezwa kiwaya kidogo kutoa hewa na mgonjwa hutakiwa kukaa hospitali kama siku mbili hivi.

Moja ya hatari ya pacemaker kushindwa kufanya kazi yake sawasawa ni kukutana na miali mikali ya mvuto au magnetic fields.

Mgonjwa alieathirika na kushindwa kwa pacemaker kufanya kazi yake sawasawa ni pamoja na mapigo ya moyo kuwa ya taratibu sana, kizunguzungu, kupiga kwikwi mfululizo na kupoteza fahamu na kuanguka ghafla.

Marehemu alikuwa akitumia kipoza hewa, na gari maalum kwa ajili ya kutoa huduma ya kwanza, na pia mmoja wa walinzi alianza kubeba kisanduku kidogo pengine kwa ajili ya kuichaji pacemaker.

Hivyo Pacemaker ni kifaa muhimu sana na kinahitaji watu ambao wanaelewa matumizi yake na utunzaji wake.

Naamini watu hao wapo na waliaminiwa kukitunza kifaa hicho.

Pia hospitali ya MOI huenda ina vifaa muhimu vya kushughulikia watu wenye pacemaker na kuhakikisha hawavurugio utaratibu mzima wa mstakabali wa kifaa hicho na hali ya mgonjwa.

Hata hospitali ya Mzena sidhani kama ina wataalam wa kushughulikia pacemaker.

Lakini pia siwelewi kwanini marehemu hakupata nafasi ya kubadilishiwa kifaa ambapo sasa hivi hukohuko walikoweka vifaa vya mwanzo, sasa hivi wanatengeneza kifaa hicho chenye umbo la dawa ya kidonge.

Kifaa hicho kipya hupandikizwa moja kwa moja kwenye moyo na hutumia wireless technology ambapo kukiprogram inakuwa rahisi na pia kunazuia infections ambazo husababishwa na kupandikizwa kifaa cha zamani ambacho hutumia nyaya.

RIP John Pombe Joseph Magufuli.
 
Keshamaliza zamu yake, bado yako na yangu, tengeneza maisha yako kabla hujatembelewa na umauti, haitasaidia kumsema vibaya zamu zetu ziko palepale iwe Kwa magonjwa ama ajali ama vyovyote vile

Mwacheni apumzike Jembe

Aliingia kwenye kinyang'anyilo cha Uraisi Kwa miujiza, kafanya kazi zake nyingi na kubwa Kwa miujiza na ametutoka Kwa miujiza kwani hakuna aliyefahamu kuwa ataondoka
GOD BLESS LEMA ALIKUWA ANAJUA KUWA ATAFIA MADARAKANI.KIBURI KWISHA MAGUFULI
 
Na wale wazee wa mi5 tena + aongezewe muda vipi? Wakati unapanga yako na ALLAH anapanga yake, marehemu hasemwi kwa mabaya dini inakataza
Tunaruhusiwa Ku plan for our future.....
japo maisha yetu hayana guarantee
 
Huyo alikuwa yeye

Mbona Magufuli alikuwa anapanda sana, mwenyewe alisema amekwenda nchi nyingi sana Ulaya ikiwemo Canada, Ujeremani, Uingereza nk
Hata huyo Kenyatta kuna kipindi fulani huko nyuma alikuwa akipanda ndege kabla ya kushauriwa kuacha kwa sababu za kiafya.
 
Mjinga tu wewe
Pamoja na majonzi ya kuondokewa na mh. Rais lakini ni vema tukakumbuka maisha aliyoishi.

Magufuli kwa kutambua kwamba ana maradhi yasiyotibika alienda kupata kikombe Cha miujiza kwa Babu wa Liliondo . Baadae iligundulika kwamba kikombe kile ulikuwa usanii tu hivyo JPM aliendelea kuwa mgonjwa.

Pili kwa kutambua kwamba ana matatizo ya moyo- Magufuli Mara kadhaa amekuwa akijiepusha kushiriki katika masuala ya simanzi Kama misiba kwa sababu za kiafya.

Hi misiba ya karibuni hasa wa Balozi Kijazi bila Shaka ilimuathiri sana Magufuli.

Naamini si CORONA Wala Mabeberu

Alale salama.
 
Je, yawezekana pia hayo matatizo yake ya moyo ndo yaliyomfanya asiwe anasafiri sana hususan nchi za nje?

Manake wakati mwingine ujinga unaweza ukamfanya mtu amhukumu kimakosa mtu mwingine.

Sisi tulikuwa tukitania ni kwa sababu alikuwa haongei vizuri Kiingereza na ndo maana alikuwa hasafiri sana kwenda nchi za nje.

Nimelifikiria sana hili suala na naona lina make sense.

Dah! I wish I knew he had some serious heart problems.
Yawezekana ikawa kweli

Ila yeye na wahusika hawakuliweka wazi walituficha

Pengine lawama ziwarudie wao .

Matatizo ya moyo Ni serious issue kwa mtu mwenye cheo Cha Rais ,umma lazima ufahamishwe kuondoa sintofahamu na prejudices
 
..endelea kuwaamini majaliwa, kipilimba, na chalamila.

..sisi tunawaamini waliotushtua kuwa anaumwa na kuwa amepelekwa Nairobi.
At least nimeongea na daktari mmoja pale JKI kabla ya kuandika hapa; mimi sisomi twitts na tabloids za Kenya.
 
Sawa amefanya kwa sehemu yake ila naamini alikuwa hajamfikia mzee Mkapa.
Kama ni mfuatiliaji pitia uhalisia wa hali aliyoikuta nchi yetu na alikoiacha, usisahau kupitia reform program zote alizoanzisha na matokeo yake!.
Inashangaza kidogo kwamba rais Mkapa alikuja kurekebisha chaos iliyoachwa na Mwinyi, na JPM akaja kurekebisha chaos iliyoachwa na JK. Mi binafsi nauona ubora wa rais Magufuli katika kufikiri kwake nje ya box. Na hilo ndilo lililomtofautisha na Mkapa. Mkapa alijenga institutions, lakini kama ni mfuatiliaji wa mambo, utagundua kuwa wanaoitwa "washirika" wetu huko nje pia walitaka (na walikuwa wakitushawishi) tuweke hizo institutions, ili uporaji wao upate uhalali wa kisheria. Kwa mfano, kwa bepari mnyonyaji, ni rahisi kudeal na semi autonomous agencies za serikali zinazodeal na madini (wakideal na mkurugenzi wa hiyo taasisi na watu flan flan mifukoni mwao, wakasign contract kwa niaba ya serikali, inakuwa imekwisha hiyo).

So mzee Mkapa alikutana na ubeberu sophisticated, uliotake advantage ya hali yetu mbaya ya kiuchumi, kuharibu kila mzizi wa kujitegemea tuliokuwa nao, ili tuzidi kuwa tegemezi. Ubora wowote wa kiongozi unapimwa au upimwe kwa namna gani nchi inazidi kujitegemea.
 
Itakuwa ndiyo sababu ya yeye kukataa kuvaa barakoa, pumzi ilikuwa ndogo. Naona watu wake wanaiga kukataa kuvaa barakoa. Ngoja tuone.
Yawezekana yeye alikuwa sababu zake za kiafya

Ila Hawa mazumbukuku aliowaacha wanaiga bila kujua

Halafu Ni watu wazima wenye akili na utashi
 
Corona wengi waliomzunguka imewaua na mlinzi wake tunaambiwa, amefia Nairobi walikokua wanauguzana.
Moyo mbovu unapona vipi Corona
Watu walio vulnerable ni wa hali ya chini, save ilianza kwa kuangusha figure kubwa kubwa za nyumba kuu, Wales wenye uwezo wa kufanya chochote kupambania uhai wao.

Ben, Kijazi, Maalim, Mlinzi, Mpango kuponea kwenye machine, mwanae kupona, mke wake kutoambukizwa.......wameichanga karata yao vizuri na Mungu awalipe kwa kadiri ya matendo yao.
 
Back
Top Bottom