Inashangaza kidogo kwamba rais Mkapa alikuja kurekebisha chaos iliyoachwa na Mwinyi, na JPM akaja kurekebisha chaos iliyoachwa na JK. Mi binafsi nauona ubora wa rais Magufuli katika kufikiri kwake nje ya box. Na hilo ndilo lililomtofautisha na Mkapa. Mkapa alijenga institutions, lakini kama ni mfuatiliaji wa mambo, utagundua kuwa wanaoitwa "washirika" wetu huko nje pia walitaka (na walikuwa wakitushawishi) tuweke hizo institutions, ili uporaji wao upate uhalali wa kisheria. Kwa mfano, kwa bepari mnyonyaji, ni rahisi kudeal na semi autonomous agencies za serikali zinazodeal na madini (wakideal na mkurugenzi wa hiyo taasisi na watu flan flan mifukoni mwao, wakasign contract kwa niaba ya serikali, inakuwa imekwisha hiyo).
So mzee Mkapa alikutana na ubeberu sophisticated, uliotake advantage ya hali yetu mbaya ya kiuchumi, kuharibu kila mzizi wa kujitegemea tuliokuwa nao, ili tuzidi kuwa tegemezi. Ubora wowote wa kiongozi unapimwa au upimwe kwa namna gani nchi inazidi kujitegemea.