Upungufu mkubwa niliouona kwa Mzee Magufuli ni kuwa uwezo wake wa diplomasia ulikuwa chini sana. Mzee wetu alifikiri in binary terms: either you are with us or you are against us! Aliwaona wazungu wote kama mabeberu, mabepari, adui, n.k. Sijui ni kwa namna gani alikuja kuvaa huo mtazamo wake kuhusu wazungu, na kujenga hiyo falsafa yake. Labda ni zile dharau za kizungu dhidi ya mtu mweusi ndizo zilizomsababishia ajenge huo mtazamo, maana huwezi kuishi na wazungu bila kufeel hiyo sense kwamba wanamdharau mtu mweusi.
Lakini pia Magufuli amekaa serikalini miaka mingi sana. Atakuwa aliwacheki wazungu walivocheza na Mkapa, halafu wakacheza na Kikwete, akajenga mtazamo kwamba these guys cannot be trusted, hawako genuine, ni matapeli tu.
Ni kweli kuna haja ya kurudisha uhusiano mzuri wa kidiplomasia na ulimwengu, lakini siyo diplomasia inayojengwa kwa msingi wa "Tanzania inahitaji dunia kuliko dunia inavyohitaji Tanzania". No, hiyo ni diplomasia ya kitoto. Msingi wetu wa diplomasia uwe Tanzania inahitaji dunia, kama dunia inavyoihitaji Tanzania.