Hayati Magufuli alionesha mara kadhaa kuwa ni mgonjwa wa moyo

Hayati Magufuli alionesha mara kadhaa kuwa ni mgonjwa wa moyo

Wanaomshambulia Magufuli wote wanasukumwa na chuki binafsi hayo mengine ni blah bkah tu.
Hayo matatizo ya moyo amekaa nayo tangu akiwa anasoma Master degree miaka takribani thelathini. Na katika miaka hiyo 30 ameifanyia makubwa sana nchi hii: yeye ndiye baba wa miundombinu tangu akiwa waziri na hadi alipokuwa Rais. Pili alikomesha ufisadi uliokuwa umetalaki serikalini .
Hivi uliona wapi mtu anaacha kazi ili asubiri kifo? Mbona wale wanaomkosoa wao hawakai wakasubiri vifo vyao na wanaendelea na kazi zao? Kifo ni siri ya Mwenyezi Mungu kila mmoja kitamfika kwa namna yake lakini hatutakiwi tukae tu kusubiri kifo.
Kimsingi watanzania tumegawanyika makundi mawili tu bila kujali vyama vyetu: wanaotaka kuiba na wanaopinga wizi. Wale wanaopinga wizi wanamunga mkono Magufuli wamo ndani ya CCM na pia nje ya CCM; na wale wanaounga mkono wizi/ufisadi wanampinga JPM na wamo ndani ya CCM na pia vyama vya upinzani.

Watu kama kina Maria wakati wa JK alikuwa anapata sana kazi ya kuwa moderator katika mikutano ya taasisi za serikali na kulipwa pesa lukuki, lakini wakati wa Magufuli alipoteza hizo kazi ndio sababu mojawapo ya kumchukia JPM.

Watu walivyo wajinga eti wanahoji kwa nini aligombea urais! Hivi mtu akiwa anaumwa ndio akae asifanye shughuli? Wao hawaumwi?

Rais Buhari wa Nigeria alilazwa nje ya nchi muda mrefu sana lakini baadae alirejea na bado aligombea urais kwa mara ya pili na hadi sasa yupo. Marais kufia madarakani hutokea na hakuna anayeweza kujua kama yupi atamaliza kipindi chake na yupi hatamaliza. Rais wa Malawi alikufa akiwa madarakani, Rais Mwanawasa wa Zambia naye alifia madarakani; pia huko miaka ya 1979 Rais Neto wa Angola alikufa akiwa anatibiwa huko Urusi. Katiba kwa kulitambua hilo ndio maana imeweka utaratibu mzuri pindi likitokea. Sio marais tu hata wabunge/madiwani pia wanakufa mara tu baada ya kuchaguliwa au wakati wa kampeni. Kifo hakina uhusiano na shughuli anazozifanya mtu.

Kazi alizozifanya JPM zimeacha alama ya kudumu katika nchi hii na zitaendelea kuchangia sana kuchochea ukuaji wa uchumi kwa miaka mingi ijayo.

Tunamwomba Mwenyezi Mungu ampokee mbinguni, akishafika mbinguni atakuwa mwombezi wa nchi yetu.
tukisema chuki binafsi watu wanabisha
 
Heee ulikuwa haujawahi kuona ...alikuwa anatembea na acc mpaka kwenye open space anawekewa
Duuh ngoja nicheki tena clip zake[emoji22][emoji22]

Nimetoka kumuaga sio siri nimeumia daah[emoji24][emoji24][emoji22]
 
Kuhusu kusafiri moja ya sababu ni pacemaker ,haitakiwi kukaa hewani kwenye ndege kwa saa nyingi,na pia swala la "KINGE" nalo ni la pili.

Kuhusu kwamba ni tatizo la moyo ndio lilimuondoa inawezekana ni kweli kwasababu uviko(covid) nayo inaleta complications kwenye moyo kwa tatizo lake.

Magufuli anaye Dr wake wa moyo KISENGE ambaye alikuwa anamonitor afya yake kila muda si rahisi afikie kuumwa serious na kufariki kwa ghafla....UVIKO ime accelerate ugonjwa wa moyo.
Mbona KISENGE[emoji848][emoji848]

ila wazazi tuwe makini na majina ya watoto wetu
 
Na amejiachia legacy ya hovyo na ya ajabu.

Kupoteza watu, kuua watu, kukwapua ela za watu, kuanzisha bwawa la mamba kuwakomoa wakosoaji wake (mamba walikua wakiachwa mpaka wiki wakiwa na njaa akikaribia mtu kutupwa umu ili ukitupiwa tu umo mamba wanakutafuna mpaka viatu vyako na autaonekana milele), kudhalilisha wamama, kuua demokrasia ya nchi, wizi wa kura wa hatari, ujuaji wa kila kitu.
Kuigeuza nchi kuwa ya kidikteta.

Lijamaa lilikuwa la ovyooo kabisa.
Heee bwawa la mamba? Wapi huko?
 
Naona tabiri za haya mambo zilishatolewa na hawa watu huku..fuata hii link..

 
magufuli kama yeye mwanaume angepambana na tundu lissu kwa hoja kikwete kafurahi kimoyomoyo magufuli kufa maana alimuonya hakusikia.afe tu kwani nani anapata hasara
Haya yoote yeye hata Hana habari, haya yanakuhusu wewe ambaye zamu yako bado inakuja
 
N
Huyu bwana nadhani alikuja hapa Duniani ili kuionyesha Dunia jinsi mtu anavyoweza hata kubishana na vitu visivyoonekana

Kiufupi alikuwa amejigeuza ndio mshauri mkuu wa masuala ya fedha,sheria,elimu,afya,michezo,biashara,siasa,kilimo,anga,Tehama na unajimu

Alichokuwa amebakiza ni kimoja tu kifo ama uzima wa milele na ndicho kilichompata,sijui kwa nini hakumsikiliza muheshimiwa Lema
Ninacho jua ni kimoja tu watanzania wanalia juu ya Magufuli na Afrika nzima inalia nenda huko YouTube ukajionee mwenyewe lakini pia ninauhakika Magufuli ameingia mbinguni
 
Korona imempeleka mzee baba. Acheni ubishi korona ipo. Korona imepelekea moyo kufeli
Naona wale watu wa usalama wanaoongoza watu kuaga hata hawajajihami na barakoa hata za kuzugia. Watu wengi sana pale hawajajihami.

Seems these lessons are hard to learn
 
Naona wale watu wa usalama wanaoongoza watu kuaga hata hawajajihami na barakoa hata za kuzugia. Watu wengi sana pale hawajajihami.

Seems these lessons are hard to learn
Baada ya wiki mbili tunazika kiongozi mwingine kwa uzembe ulofanywa pale uwanjani. Mark my words.
 
Pamoja na majonzi ya kuondokewa na Mh. Rais lakini ni vema tukakumbuka maisha aliyoishi.

Magufuli kwa kutambua kwamba ana maradhi yasiyotibika alienda kupata kikombe cha miujiza kwa Babu wa Liliondo . Baadaye iligundulika kwamba kikombe kile ulikuwa usanii tu hivyo JPM aliendelea kuwa mgonjwa.

Pili kwa kutambua kwamba ana matatizo ya moyo- Magufuli Mara kadhaa amekuwa akijiepusha kushiriki katika masuala ya simanzi Kama misiba kwa sababu za kiafya.

Hii misiba ya karibuni hasa wa Balozi Kijazi bila Shaka ilimuathiri sana Magufuli.

Naamini si CORONA Wala Mabeberu

Alale salama.
Magufuli mtu mmoja selfish sana.

Pamoja na kujua ana matatizo yote hayo ya moyo kwa siku nyingi, kaenda kugombea urais, kazi yenye mikiki mingi kwa mtu mwenye matatizo ya moyo kuifanya. Na kutufia akiwa rais kwa kuwa mbinafsi.

This is very selfish. Yani alitaka kuwa rais yeye tu bila kujali afya yake.

Zaidi ya ubinafsi alikuwa na ubishi wa kijinga.

Mtu unajijua una matatizo ya moyo, unaleta ubishi kwenye mambo ya msingi kujikinga na maradhi yanayojulikana yanafyeka watu wenye matatizo kama yako.

Hapa tunajifunza mara nyingi elimu ya mtu haizidi utamaduni.

The guy supposedly had a Ph.D in Chemistry but he couldn't do basic protective science!
 
Je, yawezekana pia hayo matatizo yake ya moyo ndo yaliyomfanya asiwe anasafiri sana hususan nchi za nje?

Manake wakati mwingine ujinga unaweza ukamfanya mtu amhukumu kimakosa mtu mwingine.

Sisi tulikuwa tukitania ni kwa sababu alikuwa haongei vizuri Kiingereza na ndo maana alikuwa hasafiri sana kwenda nchi za nje.

Nimelifikiria sana hili suala na naona lina make sense.

Dah! I wish I knew he had some serious heart problems.
This was an open secret for quite sometime.
 
Je, yawezekana pia hayo matatizo yake ya moyo ndo yaliyomfanya asiwe anasafiri sana hususan nchi za nje?

Manake wakati mwingine ujinga unaweza ukamfanya mtu amhukumu kimakosa mtu mwingine.

Sisi tulikuwa tukitania ni kwa sababu alikuwa haongei vizuri Kiingereza na ndo maana alikuwa hasafiri sana kwenda nchi za nje.

Nimelifikiria sana hili suala na naona lina make sense.

Dah! I wish I knew he had some serious heart problems.
Ndio mjue, msipende kuwahukumu watu bila kujua wanakumbana na majanga gani maishani mwao! Ngosha alikuwa kidume, pamoja na mivuvuzera ya ufipa hayakumuondoa kwenye reli hata nucta! Huyu mzee ameteka heshima kwangu sana!
 
Pamoja na majonzi ya kuondokewa na Mh. Rais lakini ni vema tukakumbuka maisha aliyoishi.

Magufuli kwa kutambua kwamba ana maradhi yasiyotibika alienda kupata kikombe cha miujiza kwa Babu wa Liliondo . Baadaye iligundulika kwamba kikombe kile ulikuwa usanii tu hivyo JPM aliendelea kuwa mgonjwa.

Pili kwa kutambua kwamba ana matatizo ya moyo- Magufuli Mara kadhaa amekuwa akijiepusha kushiriki katika masuala ya simanzi Kama misiba kwa sababu za kiafya.

Hii misiba ya karibuni hasa wa Balozi Kijazi bila Shaka ilimuathiri sana Magufuli.

Naamini si CORONA Wala Mabeberu

Alale salama.
Pia alishindwa kufanya Kampeni za Urais, badala ya kukiri kuwa ni mgonjwa akatumia Polisi kumzuia Lissu kufanya Kampeni
 
Kosa kubwa kuliko yote aliyoyafanya ni alipoidharau corona na kufuata ushauri wa joseph Msukuma

Tulikuwa tunasema anajiamini nini au ameshachanjwa?
Joseph musukuma amemdanganya sana Rais, tusipoheshimu masharti ya kijikinga corona, kabla ya tar 26.3 tutakuwa na msiba mwingine mkubwa
 
Back
Top Bottom