Hayati Magufuli alipokuwa hai hakukuwa na uhaba wa mvua na ukame nchini kama sasa

Hayati Magufuli alipokuwa hai hakukuwa na uhaba wa mvua na ukame nchini kama sasa

Peleka sifa za kujnga, 2016 kulikuwa na ukame wa ajabu, mpaka akawa anaongea kwa kejeli kuwa mtu abadilishane ng'ombe watatu na debe la mahindi. Au mnadhani tuna ubongo mdogo kama nyie na hatuwezi kukumbuka chochote?
Lakini hapakuwepo na mgao wa umeme
 
JPM alikuwa ni mtu mwenye imani thabiti, kipindi cha corona tulishuhudia baadhi ya maaskofu wakijawa hofu na imani za kutetereka juu ya uwezo wa Mungu, lakini JPM mpaka anakufa alimwani Mungu ndio muweza wa yote.

Na hii ndio inathibitisha kuwa JPM alichukiwa na waovu kuliko watu wema, na ndio maana kipindi cha uongozi wake nchi ilitulia, kulikuwa na chakula cha kutosha, mvua za kutosha, umeme wa kutosha,
samaki ziwa victoria waliongezeka, uovu na ujambazi nchini ulipotea, waliojaribu kuvuruga amani ya anchi cha moto walikiona.
Ukute hao maasikofu ndo walipita nae...vibaraka wa COVID-19
 
Mcha Mungu Magufuli alipokuwa hai hakukuwa na uhaba wa mvua na ukame nchini Kama sasa

Kuondoka tu mcha Mungu Magufuli nchi ukosefu wa mvua kila Kona, ni ukame nchi nzima na tishio la njaa kila kona ya nchi hali ya hewa vipimo vyao vinaona ukame, ukosefu wa mvua na njaa tu inayokuja.

Mwenyewe mcha Mungu angekuwepo haya yasingekuwepo

Serikali badala ya kuitisha maombi wanaenda kuhudhuria mkutano wa Mabadiliko ya Tabia nchi kuomba pesa kwa wazungu kwani pesa zaweza leta mvua msimu huu?

Magufuli angeshaitisha maombi ya kitaifa lakini kwa kuwa alikuwa mcha Mungu, Mungu alihakikisha kipindi chake mvua ipo ya kutosha, ukame haupo na njaa haipo pamoja na yeye kutohudhuria mkutano wowote wa Mabadiliko ya Tabia nchi popote duniani.
Yes, Na vile vile katika kipindi chake watu walianza kutekwa, kupotea, kupigwa risasi, kuokota maiti kwa viroba fukweni, kutumbuana hadharani kwa viongozi wa umaa bila kufuata sheria na ustaarabu...wizi kwa kura wa waziwazi mchana kweupe, pia ndani ya chama chetu kuwa mtemi mtemi kukata majina ya washindi wa kura za maoni bila.aibu..na kuweka wa upinzani aliowanunua.

Andika sifa zote, si mvua tu kunyesha.

Andika yote tu..legacy yake ni ndefu sana
 
So unatuaminisha kwamba PR SAMIA amefyonza maji?
 
Kwa kuwa mla ngubi mwenzio ndyo ukaamua kumpa uchamungu????
Wote hao hawakuwa wacha Mungu

Ni kipindi Cha Magufuli tu Ndipo tulishuhudia neema ya mvua ,na chakula tele na ukame tuliusikia kwa Wenzetu

Magufuli alimpenda Mungu akiona Kuna challenge ya kitaifa aliitisha maombi ya kitaifa na yeye aliongoza laivu kuyashiriki huwezi mlinganisha na Nyerere mkumbatia wakomunisti wasioamini Mungu au ,Mwinyi,
Au Mkapa, Kikwete au Mama Samia. No no no please

Raisi Pekee Tanzania tulipata mjali Mungu na mheshimu Mungu waziwazi kitaifa Ni Magufuli tu hao wengine wote hamna kitu ikifika kwenye maswala ya Mungu kitaifa
 
Mkuu usiingize hz aya ktk haya masiasa ya kitwaaghuut
Kwa hakika anayeleta mvua na Kuzuia Ni MwenyeziMungu Peke yake Kwa sababu zke.
Lakini katika Sababu ya kuzuiwa mvua na kupatikana Ukame ni madhambi ya Viumebe.
Na hawa viongozi wa CCM wamezidi mno katika kutenda madhambi ya Dhuluma ,na wala hawaoneshi nia ya KUTUBU na kumrejea Mungu mwenyezi.
Hata Hivyo mzee Magu alikuwa anapenda sana Kumtanguliza Mungu kwa kauli zake Hadharani Na kwa Hili yawezekana sana M/Mungu kufurahi na Utawala wake hata kama ulitenda maovu kiasigani, lakini kwa vile alitubu na Kumrejea Mungu huend basi Mungu alimbarikia utawala wake kwa Mvua..
Quran nayo pia ina ungana na Maandiko hayo hapo juu ya Taurati na Injili kuhusu Kumrejea Mungu.
Qur-an Sura ya 77Aya No10 - 14 inasema:-

10. Nikasema( Mmi Nuhu kuwambia watu wangu watendao maovu): Ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi; hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe.
11. Atakuleteeni mvua inyeshe mfululizo kwa misimu yake.
12. Na atakupeni mali na watoto, na atakuotesheeni mabustani ya (mazao mbali mbali) na atakufanyieni mito (inayotiririka).
13. Mna nini basi, hamweki heshima kwa Mwenyezi Mungu?
14. Na hali Yeye kakuumbeni hatua kwa hatua ( kuanzia Mimba ,utoto,ujana ,utuuzima na hatimae Uzee kisha Mauti)?

lakini wapi hawakuonesha utiifu na Gharika ikawakumba
 
Lakini hapakuwepo na mgao wa umeme

Haukuwa mkali kama sasa, lakini ulikuwepo. Ilipofika wakati wa kampeni mgao wa umeme ulianza taratibu, na sasa ni muendelezo tu wa tatizo lile.
 
Haukuwa mkali kama sasa, lakini ulikuwepo. Ilipofika wakati wa kampeni mgao wa umeme ulianza taratibu, na sasa ni muendelezo tu wa tatizo lile.
Muda ni mwalimu mzuri sana!

Tulipowambia kina makamba wameenda pale na hali ya umeme ni mbaya mkaanza kumtetea eti sukuma gang wanaona wivu. Sasa vilio kila kona kuanzia ufipa hadi moshi ni vilio vya umeme tu.

Na bado
 
Ndio maana Lisu aliwaita nyie ni wapumbavu kwa kufikiri awamu ya 5 tu ndio mambo hayo yanetokea!

Bomu kwenye mkutano wa chadema kule arusha ilikuwa kipindi cha Magu?

Yule mwangosi aliesamabratishwa na bomu kule iringa ilikuwa awamu ya Magu?

Ulimboka ilikuwa awamu ya magu?

Mvungi ilikuwa awamu ya magu?

Rwakatare kuitwa gaidi alikuwa magu yule?
CCM ni walewale ila awamu ya tano ilikuwa na uzuzu mwingi sana ambao nimekutajia hapo juu...kuongezea tu jamaa akawajaza ujinga vijana wakao wanatesa watu hovyo hovyo..

Na ndiyo maana Katiba mkaibana kabatini ili mtawale nchi kwa mabavu...

Anayeongelea katiba anaitwa Gaidi..CCM hamna jipya..ni jumba bovu !!
 
Muda ni mwalimu mzuri sana!

Tulipowambia kina makamba wameenda pale na hali ya umeme ni mbaya mkaanza kumtetea eti sukuma gang wanaona wivu. Sasa vilio kila kona kuanzia ufipa hadi moshi ni vilio vya umeme tu.

Na bado

Bora umeme ukatike kuliko kutawaliwa na dhalimu. Kwa taarifa yako umeme haupo lakini kwangu ni poa tu kuliko kuwa chini ya dhalimu. Hata hii kukatika sasa sababu ni yeye huko nyuma. Hutaki jinyonge. Ni hivi, hata ufanyike uchafu vipi, kwangu dhalimu ni dhalimu tu fullstop.
 
Utanyoooka tu!

JamiiForums430303985.jpg
 
Najua unajua ni wapi anakunyoosha ila ni ubishi wako tu

Unatamani angekuwa ananiumiza, kazi ya kilimo cha kisasa anakutana na nini wapi? Ninachojua anaiga tembo kunya lakini hana madhara. Kama unatamani tuone yuko kama dhalimu basi umeukalia.
 
Unatamani angekuwa ananiumiza, kazi ya kilimo cha kisasa anakutana na nini wapi? Ninachojua anaiga tembo kunya lakini hana madhara. Kama unatamani tuone yuko kama dhalimu basi umeukalia.
Anaiga kunya kwa tembo huku mwenyekiti anasota rumande mwezi wa 3 huu?

Hivi kweli bavicha mlifikiri akifa Magu ndio mambo yenu yatakuwa mteremko?

Hivi 2025 mtashiriki uchaguzi?
 
Wilderness Voice

Kuna sauti ikikuambia tukaombe au tunamtegemea Mungu kweli utaisikia. Lakini siyo sauti ya Magufuli. Kamwe huyu Mungu tunayemwabudu Wakristo Mungu wa Abraham, Izaka na Yakobo siye Mungu aliyekuwa ana mwabudu Magufuli.

Kwa matendo aliyowatendea wenye vyeti feki, aliowatumbua kazini, aliowapeleka Segerea, aliowaua kwa kikundi cha WASIOJULIKANA, aliowanyima nyongeza za mishahara, aliowabomolea nyumba Kimara kamwe hawezi kuomba Mungu akamsikiliza.

Labda mungu (m- ndogo) wa Gwajiboy, Mch Mashimo. Hilo DUBWASHA mnalilisifia kwa Tanzania likikuwa Moja tu. Nalo liliingia kwa bahati mbaya toka Burundi. Baada ya kulizika pale Chato mnamo tarehe 27/ 03/ 21, Tanzania imekuwa kama imepata Uhuru wa pili

Hakika nasema Mtanzania halisi hawezi kuwa na chuki ambayo Magufuli alikuwa nayo dhidi ya Watanzania.

Kwa wanaompenda nawashauri wamfuate huko kuzimu, hamna namna
Mungu ndiye ajuaye nafsi zetu, swala la kuzimu soon nawe utaenda.
 
Mcha Mungu Magufuli alipokuwa hai hakukuwa na uhaba wa mvua na ukame nchini Kama sasa

Kuondoka tu mcha Mungu Magufuli nchi ukosefu wa mvua kila Kona, ni ukame nchi nzima na tishio la njaa kila kona ya nchi hali ya hewa vipimo vyao vinaona ukame, ukosefu wa mvua na njaa tu inayokuja.

Mwenyewe mcha Mungu angekuwepo haya yasingekuwepo

Serikali badala ya kuitisha maombi wanaenda kuhudhuria mkutano wa Mabadiliko ya Tabia nchi kuomba pesa kwa wazungu kwani pesa zaweza leta mvua msimu huu?

Magufuli angeshaitisha maombi ya kitaifa lakini kwa kuwa alikuwa mcha Mungu, Mungu alihakikisha kipindi chake mvua ipo ya kutosha, ukame haupo na njaa haipo pamoja na yeye kutohudhuria mkutano wowote wa Mabadiliko ya Tabia nchi popote duniani.
Aisee, Hamieni Chato kwenye kaburi lake ili mumwabudu vizuri,eti mcha Mungu Magufuli,hilo liuaji katili limekuwa mcha Mungu?
Kwa hiyo Magufuli ndo mtakatifu wa Tanzania nzima wewe Boya?
Hata kabla hajazaliwa mvua zilikuwa za Tabu.
Miaka haifanani wewe kiazi
 
Anaiga kunya kwa tembo huku mwenyekiti anasota rumande mwezi wa 3 huu?

Hivi kweli bavicha mlifikiri akifa Magu ndio mambo yenu yatakuwa mteremko?

Hivi 2025 mtashiriki uchaguzi?
Mwenyekiti kusota ndani hakuanza kipindi cha mama wa kambo, bali hata kipindi cha dhalimu. Wapinzani hatutaki mteremko maana tuna wapigakura wa uhakika. Ccm ndio inahitaji mteremko maana ndio inashurutisha kukaa madarakani kwa shuruti.

Mimi sio msemaji wa chama chochote cha siasa hapa nchini, ila nitashiriki kupiga kura mazingira yakiwa tofauti na sasa, kinyume na hapo sijihusishi na ukhanithi.
 
Uhanith?

Mungu wako si amewaondolea mbaya wenu aliekuwa anasababisha uhanith bila kumwaga damu?
 
Back
Top Bottom