Mungu amlaze mahali pema peponi. Kazi zake zimeonekana na jitihada zake. Wengi wao humponda Magufuli kwa sababu chuki zinatuendesha ila kiuhalisia alifanya mengi na aliona mbali. Kwa wasiokuwa na faida nae nawapa pole sana ila kwa sie tulioona faida nae tunaendelea kumuombea. Huwezi kuwa raisi ukawafuraisha wote. .
Watu hupenda kushangilia vitu bila kutafakazi na mihemko ya vijiweni. Leo hii unaona kabisa mfumuko wa bei wa kiholea yote haya wanamuita dictator ila ilibidi ili mabepari na mabeberu wasitunyonye. Leo hii unaona panya road wengi na hao walifukuzwa machinga. Leo hii wazungu wanadai sisi ni marafiki zao na utumwa wa kumwabudu mzungu kila kitu; tangia lini mzungu akatupenda sisi. .
Ni vitu vingi watu wanapotosha, eti mnafungua nchi, sasa nchi imefunguliwa kipi ambacho tunafaidika na wazungu. Hatuwezi kuishi wenyewe sikatai ila AIBU tupu tunanyonywa hadi na wakenya? Mungu akulaze mahali pema peponi, mapungufu yako kibinadamu Mungu akusamehe, hakuna mkamilifu, umefanya makubwa sana. .