Hayati Magufuli alitaka kuiangamiza CHADEMA kwa mabavu, Rais Samia amewapa kamba wajinyonge wenyewe

Tukionee huruma hiki chama cha harakati
Kwa sasa dawa ya kuwamaliza imepatikana

Uhuru walipewa wanadhihirisha mbele ya watanzania kuwa wao ni wahuni na watapuuzwa wakijiangamiza wenyewe.
Haha kwa hoja hizi mtatoka kweli? Hata hivyo hongera sana kwa Uzi mzuri mno
 
Usidanganywe na hizo video chache. CCM wana uzoefu mkubwa sana wa siasa.

Ukumbuke awamu ya JK kila mtu akajua ndio mwisho wa chama, wakatumwa wazee kina Kinana na Migiro kuiangukia jamii ya wapiga kura.

Iwapo JPM alishinda kwa kishindo sioni namna ambayo Samia anaweza kushindwa, anatekeleza miradi ya marehemu, mmoja baada ya mwingine.

DP World watakapoanza kazi8 Novemba utayaona mabadiliko makubwa kwenye uchumi mzima wa nchi. Kuna uwezekano bei za bidhaa nyingi zikashuka, tukumbuke kuwa meli zao pekee ndio zitakazohudumia bandari hii ya Dar hivyo kuna gharama watakazozibeba wao ambazo zitakwenda kugusa bei za bidhaa mtaani.

Pia ushushaji na upakiaji wa haraka utakwenda kubadilisha masuala mengi ya kiuchumi ambayo kwa sasa bado ni mzigo.
Uzoefu wao ni kuiba kura hilo hata mtoto mdogo anajua,na kama unaamini kuwa Magufuli alishinda kwa kishundu basi utakuwa na mtindio wa ubongo.
 
Magu aliwashindwa vipi watu aliwapiga marufuku wasifanye mikutano ya hadhara wakatii, aliwatisha wakatishika wakakimbia nchi, akawapora majimbo yote na viti Maalum akawachagulia Wabunge ?

Wanaharakati wote wa kupinga Serikali na kulilia Katiba mpya walikuwa likizo ya lazima wakati wa Mwamba John Joseph Pombe Magufuli

JPM alikuwa chuma cha Mjerumani kile
Alikuwa chuma sasa yuko wapi? Hakuna mbabe mbele ya Mungu
 
Hoja ni kuwa walitii maelekezo yake au laa, aliwanyoosha au laa, Mbowe aliufyata hata kusema tu kuwa Akaunti zake zilipigwa pin aliogopa na kaja kusema miezi kadhaa baada ya Mwamba kuondoka? suala la kifo lipo kwa kila mtu na tofauti yetu ni muda na chanzo tu
Sasa hauoni kama CDM ni hatari. Bila wizi CCM wanajua fika hawatakiwi.
 
Uzoefu wao ni kuiba kura hilo hata mtoto mdogo anajua,na kama unaamini kuwa Magufuli alishinda kwa kishundu basi utakuwa na mtindio wa ubongo.
Kila siku mnadai kuibiwa kura wakati mnafanya siasa za matusi tu dhidi ya uongozi unaokuwepo madarakani.

Magufuli kajenga miundo mbinu nchi nzima siku zote alikuwa karibu na mtanzania wa kawaida kabisa, unapoamini kwamba na yeye aliiba kura ni sawa na kuwa mwendawazimu yule mwenye kustahili kufungwa kamba na kupelekwa milembe Dodoma.

JPM alifufua shirika la ndege linalozidi kukua kidunia, kajenga SGR inayokwenda kuleta mzigo kutoka Rwanda na Congo kuja bandarini Dar, kuamini kwamba na yeye aliiba kura ni kuwadharau watanzania waliompigia kura.

Huwezi kupewa nchi kwa kuja na mikakati mingi dhaifu inayoishia kukosoa na kuponda serikali kwa vibonzo vya facebook, twitter na humu Jamiiforum.
 
Tukionee huruma hiki chama cha harakati
Kwa sasa dawa ya kuwamaliza imepatikana

Uhuru walipewa wanadhihirisha mbele ya watanzania kuwa wao ni wahuni na watapuuzwa wakijiangamiza wenyewe.
Kizazi cha aina yako kinakaribia kufutika kabisa Tanzania. Wengi wenu ni wanufaika wa mifumo ya CCM au mmeathirika na ujinga na mazingira
 
Magu aliwashindwa vipi watu aliwapiga marufuku wasifanye mikutano ya hadhara wakatii, aliwatisha wakatishika wakakimbia nchi, akawapora majimbo yote na viti Maalum akawachagulia Wabunge ?

Wanaharakati wote wa kupinga Serikali na kulilia Katiba mpya walikuwa likizo ya lazima wakati wa Mwamba John Joseph Pombe Magufuli

JPM alikuwa chuma cha Mjerumani kile
Wenye busara hawakukimbia bali waliamua kukaa kimya waone mwisho wa ujinga wake utakuaje.Na madhara ya ule ujinga unaonekana leo kwa macho.Kama akili zako niza kichawa uwezi kuelewa.
 
Kila siku mnadai kuibiwa kura wakati mnafanya siasa za matusi tu dhidi ya uongozi unaokuwepo madarakani.

Magufuli kajenga miundo mbinu nchi nzima siku zote alikuwa karibu na mtanzania wa kawaida kabisa, unapoamini kwamba na yeye aliiba kura ni sawa na kuwa mwendawazimu yule mwenye kustahili kufungwa kamba na kupelekwa milembe Dodoma.

JPM alifufua shirika la ndege linalozidi kukua kidunia, kajenga SGR inayokwenda kuleta mzigo kutoka Rwanda na Congo kuja bandarini Dar, kuamini kwamba na yeye aliiba kura ni kuwadharau watanzania waliompigia kura.

Huwezi kupewa nchi kwa kuja na mikakati mingi dhaifu inayoishia kukosoa na kuponda serikali kwa vibonzo vya facebook, twitter na humu Jamiiforum.
Wewe huna akili naamua kukupuuza.
 
Tukionee huruma hiki chama cha harakati
Kwa sasa dawa ya kuwamaliza imepatikana

Uhuru walipewa wanadhihirisha mbele ya watanzania kuwa wao ni wahuni na watapuuzwa wakijiangamiza wenyewe.
Akili ya wanachadema imekomaa sana nyakati hizi. Wanajua njia ccm kujifanya wanapuliza huku wanang'ata. Fatilia maneno ya Mzee Cheyo. Bila katiba mpya, sababu zote za kiccm kutotimiza takwa la katiba mpya. Nikutotaka katiba mpya.
Vikao na vikosi kazi vya nini wakati iko wazi, kuwa tunataka katiba mpya, na hatutaki bandari yetu iuzwe. Lasilimali zetu ziheshimiwe.
Ndo maana Hawakuona haja ya kuhudhuria kwenye kongamano la kijinga kama lile. Wangekua wamejisariti wenyewe na wanainchi walio nyuma yao
Kwa icho kilichofanyika kwenye kongamano la chai, lunch na Dina Kwa siku tatu, Kwa pesa ya watanzania. NAWAPONGEZA CHADEMA KWA KUTOENDA UKO
 
Upinzani ni sehemu ya Watanzania
 
Tukionee huruma hiki chama cha harakati
Kwa sasa dawa ya kuwamaliza imepatikana

Uhuru walipewa wanadhihirisha mbele ya watanzania kuwa wao ni wahuni na watapuuzwa wakijiangamiza wenyewe.
CHADEMA IPO KWA TAKWA LA MUNGU NA HAITAKUFA BALI WENYE NIA MBAYA NA CHADEMA NDIO WATAKUFA
 
Akili ya wanachadema imekomaa sana nyakati hizi. Wanajua njia ccm kujifanya wanapuliza huku wanang'ata. Fatilia maneno ya Mzee Cheyo. Bila katiba mpya, sababu zote za kiccm kutotimiza takwa la katiba mpya. Nikutotaka katiba mpya.
Vikao na vikosi kazi vya nini wakati iko wazi, kuwa tunataka katiba mpya, na hatutaki bandari yetu iuzwe. Lasilimali zetu ziheshimiwe.
Ndo maana Hawakuona haja ya kuhudhuria kwenye kongamano la kijinga kama lile. Wangekua wamejisariti wenyewe na wanainchi walio nyuma yao
Kwa icho kilichofanyika kwenye kongamano la chai, lunch na Dina Kwa siku tatu, Kwa pesa ya watanzania. NAWAPONGEZA CHADEMA KWA KUTOENDA UKO
Hakuna anayetaka kuuza bandari hilo ni neno zito sana. Ni upangishaji ili tija iweze kuongezeka.

Kubakia na uendeshaji ule ule wa kizamani wakati dunia imeshabadilika kwa kasi ni kujidanganya, ni kuishi na fikra za kijamaa wakati dunia ya kisasa haina urafiki na ujamaa. Rasilimali zetu zitaongezwa ubora wa matumizi yake kwa kutafutiwa mpangishaji mpya.

Wakati tunapokuja na akili kwamba nchi inataka kuuzwa na rasilimali zetu kutoheshimiwa, tukumbuke tu kwamba bandari yetu inahudumia nchi saba zinazotuzunguka.

Haiwezekani tukaiona tija pana ya sekta ya bandari kwa kuendelea kutegemea teknolojia za kizamani.
 
Nia ni njema
Njia ni ovu.
Tutafikiaje Nia njema?
Nia sio kuuza, ila njia ni ya kuiuza. Je mwishowe itakua haijauzwa?
Unampangisha mtu nyumban, na kumpa hati miliki, umempangisha au umemuuzia.
Tukubali tukatae mikataba mingi ya inch hii ni mibaya Kwa sababu ya njia. Hua mwl anaekopa fedha na kuweka Bondi kadi ya Benk na namba ya Siri Ili atatue mambo ambayo kimsingi ni muhimu Kwa familia yake, tunamuita mjinga, Kwa nin Tanzania isiwe ya wajinga Kwa kusaini mikataba mibovu Kwa kuweka lehani lasilimali za taifa??
Ndo maana tunasema wameuza Kwa sababu mkataba ni mbaya
 
Ukiwa hujaelewa kitu ni vizuri uandishi wake usiwe na maneno ya kujifanya unaelewa unachokiongea.

Hati miliki ya bandari ni mali ya bandari yenyewe, ambayo ni mali ya serikali ya JMT.

DP World anapangishwa magat namba tatu mpaka namba nane.

Mwendeshaji mwingine anayetafutwa muda huu atapangishwa magati namba nane mpaka kumi na moja.

Kuna mwendeshaji mwingine anayetafutwa muda huu kwa ajili ya bandari ya Mbegani Bagamoyo, atapangishwa pia.

Kuna mwendeshaji mwingine anatafutwa muda huu kwa ajili ya bandari ya Tanga, atapangishwa pia.

Hawa ni wapangaji sio wamiliki, sasa hayo masuala ya bandari zetu kuuzwa ni matokeo ya uelewa mdogo wa hao wanaoipinga mipango ya kiserikali.

Rasilimali za Taifa sio bandari, kile ni chombo cha kibiashara. Ni sawa uwe na nyumba kadhaa za kupanga na wakati wewe mwenye nyumba unaishi eneo hilo hilo, unavuta kodi yao kwa mujibu wa mkataba mnaokubaliana na wao wanaendelea kutoa huduma bora za bandari.

Watu wangu wanapotea kwa kukosa maarifa - Biblia Takatifu.
 
Back
Top Bottom