Hayati Magufuli alivyoifilisi familia ya Jamal Malinzi

Hayati Magufuli alivyoifilisi familia ya Jamal Malinzi

Uchaguzi wa mwaka 2015 ni miongoni mwa chaguzi ngumu kuwahi kutokea nchini ukiacha ule wa 1995. EL alimkaba vilivyo JPM mpaka akakosa usingizi.

Bajeti ya kampeni ya CCM ilipwaya kwa mchaka mchaka ule ikabidi itafutwe njia mbadala ili mamvo yaende.
Wafanyabiashara mbalimbali na taasisi mbalimbali wakaombwa kuchangia na kuahidiwa kurudishiwa pesa zao baada ya uchaguzi.

Kama muujiza shirikisho la mpira nchini TFF likapokea bilioni kadhaa sio nyingi sana ili kuendeleza program za michezo nchini. Vigogo wa chama kubwa wakazinusa,kesho yake mbio mpaka ilala karume zilipo ofisi za TFF ,wimbo ukiwa uleule tuazimeni pesa tutarudisha after uchaguzi. Jamal akagoma akiogopa ma auditor wa FIFA endapo wangetua nchini ghafla wakakuta akaunti haina pesa itakuwaje.

Vigogo wakaondoka mikono.mitupu.
Tarehe 28 june 2017 Nissan Patrol nyeupe inatinga viwanja vya karume wanashuka wanaume wanne wanawatia pingu Jamal Malinzi na katibu wake Mwesigwa Celestine na maofisa wengine wawili wa TFF.

Hawakuliona jua mpaka tarehe 10 dec 2019 miaka miwili na nusu,walishtakiwa kwa uhujumu uchumi,utakatishaji fedha,forgery,matumizi mabaya ya fedha na kutia hasara kuasi cha dola 375,418 sawa na milioni 847 wakati huo.

Uchunguzi ulipofanyika ikaonekana hizo pesa zipo au zilifanya kazi ya TFF ila kulikuwa tu na makosa kidogo ya kiuhasibu,kuna nyaraka hazikukamilika na zilihitaji maelezo ili zikamilike.

Bwana mkubwa hakuelewa hilo akasisitiza plea bargain ,pesa zilipwe.si mlikataa kuchangia kampeni.

Akaunti ya Jama Malinzi ikakutwa na Milioni zisizozidi 100. Celestine Mwesigwa milioni 19 Wale maofisa wawili Nsiande mwaya mhasibu ,na karani Flora kwa pamoja walikutwa na milioni kama tano tu kwenye akaunti.

Jamal akataka kuvimba kama mbwai mbwai tu acha nifungwe, Damu nzito kuliko maji,ndugu zake Jamal walikuwa wanajiweza wakachangishana wakalipa plea bargain ifisi ya DPP.Milioni 847

Kesho yake wakaenda mahakamani akapigwa faini ya shilingi laki tano tu na kuachiwa huru. Milioni 847 sio pesa ndogo,baadhi ya biashara za zimekufa kwa kukosa mtaji na zilizobaki zinayumba. Jiulize wewe na familia yako mtauza nni kupata milioni 800 kumtoa ndugu yenu jela
Wewe mzushi na huna lolote unalojua. Hapa hata Fifa waliingilia lakini mbona walirudi nyuma wakaacha mchakato wa kimahakama uendelee?

Hakuna unachojua kuhusu hili la TFF na Simba na chama cha ngumi Tanzania
 
Tutauza figo mojamoja woooote isipokuwa bibi figo yake inashida
 
Muwe mnatumia akili kidogo, uchaguzi wa 2015 ulifanyika tarehe 25 October, na akatangazwa mshindi tarehe 30 October 2015, kwahiyo kutoka November 2015 alipoapishwa JPM hadi June 28 2017, walikuwa wanamuogopa Malinzi wasimkamate?

Vitu vingine kama hamna data muwe mnakaa kimya. Malinzi alifanya ufisadi mkubwa sana, kama unabisha waulize ndugu zake, kwanza jiulize ni ndugu gani wa Malinzi mwenye uwezo wa kutoa milioni 847, Ili kumtoa Malinzi ndani huku nyuma akifilisika?,mtaje hapa maana ndugu zake wanafahamika wote.
Dioniz Malinzi alikuwa na uwezo wa kutoa hizo milioni 800 na ushehe, ana ukwasi wa kutosha I mean billions za pesa za madafu.
 
Labda yule binti take aliyeolewa na Sangoma alitoa.
Muwe mnatumia akili kidogo, uchaguzi wa 2015 ulifanyika tarehe 25 October, na akatangazwa mshindi tarehe 30 October 2015, kwahiyo kutoka November 2015 alipoapishwa JPM hadi June 28 2017, walikuwa wanamuogopa Malinzi wasimkamate?

Vitu vingine kama hamna data muwe mnakaa kimya. Malinzi alifanya ufisadi mkubwa sana, kama unabisha waulize ndugu zake, kwanza jiulize ni ndugu gani wa Malinzi mwenye uwezo wa kutoa milioni 847, Ili kumtoa Malinzi ndani huku nyuma akifilisika?,mtaje hapa maana ndugu zake wanafahamika wote.
 
Ila kuna watu wana roho ngumu nyie ,mali za Mbowe zilizoharibiwa ni billion kadhaa za shilingi ila yupo tu anapambana ,aisee kwa mtu mwenye roho fupi angepigwa na stroke ,kuanzia miradi yake ya greenhouses farms za mboga na matunda Kule Machame ,uje club billcanas ,bank accounts kuwa freezed , hoteli za kitalii zake kule Arusha na moshi kupigwa ban ,nyie
Magufuli ni zaidi ya ibilisi
Kina Mbowe sio wenzenu, wafadhili/wanaowatuma wanawapa pesa nyingi sana
 
Kila mama akienda kulia kwa wanasiasa akasikilizwa nani atafungwa?
Kabendera alikua na kosa gani??

Mama alijua mwanae anaonewa ndio maana alikua anaomba msaada wa wanasiasa. Jambo la mwanae lilikaa kisiasa.

Na hata upepo wa kipindi kile ndivyo ulivyokua, ukinyeyekea unafanyiwa utakalo, mama akapita kwenye chaki bahati mbaya mwanae alimkasirisha sana mkulu.
 
Duh...!. Japo sina any facts for or against to substantiate the facts of this story, but I seriously doubt the correctness of these facts presented here kwasababu familia ya Malinzi tunaifahamu, milioni 800 ni kama punje tuu ya mchele kwa familia hiyo, ni familia ya wacha Mungu wanao mtanguliza mbele Mungu kwenye kila kitu, hivyo Jamal hakutoka kwa plea bargain, kwasababu ya uadilifu.
Sorry siamini hii story!.

Naendelea kusisitiza JPM hakuwa malaika, ila pia hakuwa shetani kama watu wanavyo mdemonise sasa, naomba niendelee kuwajulisha mahali JPM alipo sasa Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani, msiendelee kuhangaika bure na kujichumia dhambi za bure kumsingizia marehemu.

P
Kwa hakika kwa mambo tuliyoshuhudia na kuyasikia Mungu atukuja kutupa siku ya kujua alikuwa nani zaidi: malaika au shetani? Haiwezekani kuwa katikati ya malaika na shetani! Lakini muhimu zaidi kuliko umalaika au ushetani wa uongozi wowote mamlaka za nchi kuweka mazingira huru na kuwawezesha Watanzania kujifunza kutokana na historia ya nchi yao kwa ukamilifu badala ya kuendekeza utukuzaji wa viongozi wa kisiasa!
 
Iliitwa "timu ya ushindi"; ilitembelea watu wengi muhimu wakiwemo CEOs wa parastatals na kuwataka "support" kama wanataka kuendelea kuwa ndani ya ulingo, that's it. Waliosita wanajua kilichowakuta - baadaye - when the going started being nasty.
Leo kinana na nape waliohusika hawatajwi, ni watakatifu, laana zote anapelekewa magu, ndio maana ni hatari kulaani, sababu laana zitaanzia kwako, na hasa kumlaani mkuu wa watu
 
Kuna watu humu wanalazimisha kila mtu awe anamkumbuka JPM kwa mazuri tuu

Ukija kuzungumzia tu mabaya yake utaitwa majina ya kila aina wewe subili utaona
Hayati Magufuli alale pema peponi. Siri yote wanaijuwa wenye siri zao na kwakuwa muda haugandi siku zina kuja mtatafuta nakuzodowana na hii ni baada yakujuwa ukweli.., rudisheni hizo pesa kama kweli ni mtu alipanga...
 
Kuna watu humu wanalazimisha kila mtu awe anamkumbuka JPM kwa mazuri tuu

Ukija kuzungumzia tu mabaya yake utaitwa majina ya kila aina wewe subili utaona
Hayati Magufuli alale pema peponi. Siri yote wanaijuwa wenye siri zao na kwakuwa muda haugandi siku zina kuja mtatafuta nakuzodowana na hii ni baada yakujuwa ukweli.., rudisheni hizo pesa kama kweli ni mtu alipanga. Hakuna haja yakupiga kelele nakumsema mtu alie lala. Kama alikuwa peke yake kwenye hayo maamuzi rudisheni hizo pesa wapelekeni mahakamani walio fanya hayo maovu na uchaguzi uwe wa uhuru na hakituone Kama atarudi mtu. Bora Tukae kimya na tuchutame.
 
Back
Top Bottom