Hayati Magufuli aliweza kuwatisha waovu, mifumo iliamka kufanya kazi

Hayati Magufuli aliweza kuwatisha waovu, mifumo iliamka kufanya kazi

Kama wewe ni Magufuli mpya uliyezaliwa jihesabu tu kama kiumbe chenye hasara duniani.
Vijana wakishavuta bangi wakichanganya na energy wanawaza pumba tu.

Nilikutana na mama yake Alfonsi Mawazo mwishoni mwa mwaka Jana. Yule mama ukikaa naye akakihadithia mateso anayopitia kutokana na kifo cha mwanae ,machozi yatakutoka. Maana kwa maelezo yake Alfonsi alikuwa tegemeo lake.

Cha ajabu hao viongozi wa chadema waliokuwa mstari wa mbele kumpamba Alfonsi azidi kupata ujasiri wa kusimama majukwaani kupambana na viongozi wa Serikali akiwemo huyo Magufuli, hawana habari naye yule mama.

Anasema mwaka Jana alitembelewa na T.A.L akiwa na sukari kilo mbili ,Mchele kilo tatu, chumvi na sabuni na waandishi wa habari kwaajili ya kurekodi ziara yake hiyo.

Laiti binadamu tungewekeza akili zetu kwenye maendeleo tungeendelea sana. Badala yake akili zetu tumejikita zaidi kwenye migogoro. Unakutana na mtu barabarani kabla ya salamu anakuuliza mbona umekonda sana?. 😆😆Sijui alitakaje........
 
KAZI za Magu zinaonekana wazi.

Pita pale kijazi flyover utaona alama yake,

Tembea Nchi nzima uone KAZI zake,

Ikiwa aliiba Kisha kwenda kujenga vinavyoonekana,

Wizi wake ni mzuri wenye TIJA.
images (3).jpeg
 
Attachments

  • images (3).jpeg
    images (3).jpeg
    43.1 KB · Views: 1
Salaam, Shalom.

Ili pawe na Amani, huna budi kuwatisha waovu, KAZI hii ya kuhakikisha waovu hawachezei Sharubu za Serikali, Mungu alimsaidia Hayati Magufuli kuifanya kazi hiyo kwa ufasaha.

Maeneo yafuatayo, alidhibiti kwelikweli;

1. MTANDAO WA WIZI WA PESA ZA UMMA

Tumesikia Rais Samia analalamika Badala ya kuamrisha mifumo, asema kuwa umerudi mtandao wa kuiba pesa za umma, yaani pesa inatoka hazina kuja halmashauri, wanatokea watu, wanachepusha pesa hizo zinaingia katika account zao, na pesa hizo ni za mikopo tuliyokopa!

Miradi aliyeanzisha Magu, ilienda kwa kasi sababu ya ufuatiliaji wa karibu na wezi walidhibitiwa hasa.Usingeweza kukwiba pesa ya umma ukabaki salama.

2. UJAMBAZI WA KUTUMIA SILAHA.

Katika kipindi chake, majambazi walienda likizo, hilo litoshe kutupa kujua kazi kubwa aliyoifanya hasa katika kuifanya mifumo ya ulinzi na Usalama kutenda kazi Kwa viwango vya juu.

3. KUDHIBITI MTANDAO WA DAWA ZA KULEVYA

Kabla ya Magufuli kuingia madarakani, Nchi yetu ilikithiri kwa kutapakaa kwa dawa za kulevya, lakini baada ya miaka kadhaa, mateja wengi walijisalimisha katika sobber houses, sababu kuu ikiwa ni kuadimika Kwa dawa za kulevya mtaani. Hilo litoshe kutuonyesha jinsi ambavyo palifanyika kazi kubwa underground.

4. UTAKATISHAJI FEDHA

Pesa haramu, chafu zilizotokana na biashara ovu ya kuiba pesa za umma, uuzaji dawa za kulevya, biashara chafu za ukwepaji kodi, zilidhibitiwa kwa kiasi kikubwa, jambo hilo lilileta mtikisiko kwenye Uchumi kwa kuwa Kwa namna moja au ingine, pesa hizo zilisaidia kutengeneza ajira sekta binafsi.

5. MFUMO WA EFD ULIFANYA KAZI

Vituo vya mafuta kwa Mfano, vyenye kuingiza pesa nyingi, hazikuwa zikitoa EFD, na walipobanwa kutoa risiti, walitishia kugoma.

Ujasiri wa Magufuli, ulisaidia wafanyabiashara hao kurudi mezani na kukubali kutoa EFD bila masharti.

6. UFANISI KATIKA MIFUMO YA UTOAJI MIZIGO BANDARINI

Ni katika uongozi wa Hayati Magufuli, document za kutoa Mzigo bandarini zilipungua, mwanzoni palikuwa na utitiri wa karatasi na mizunguko iliyochelewesha ufaulishaji mizigo bandarini.

Scana ya ukaguzi wa vitu vinavyopita bandarini ULIFANYA KAZI utawala wa Magufuli, alipambana kweli kweli na ufanisi ulionekana.

HITIMISHO

Pamoja na mapungufu wa kibinadamu na makosa kadhaa aliyoifanya Hayati Magufuli, itoshe kusema, Mungu alimwezesha kukaa katika KITI cha maamuzi sawasawa na kuhakikisha mifumo inafanya KAZI. Magufuli hakulalamika, alichukua hatua.

OMBI: Wananchi tunaomba atokee kiongozi atakayefuta BETTING nchini, hivi sasa, vijana wa CCM+ CDM na wasio na vyama wametekwa na jinamizi hili, HAYATI Magu hakuliweza hili. Maisha hayajawahi kuwa Bahati nasibu.

Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya Rais Magufuli.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo Tanzania🇹🇿.

Amen.
Hata ukichunguza sasa hivi wanaomchukia Magu, ni wale wanyonyaji aliowakata mirija yao.
 
Vijana wakishavuta bangi wakichanganya na energy wanawaza pumba tu.

Nilikutana na mama yake Alfonsi Mawazo mwishoni mwa mwaka Jana. Yule mama ukikaa naye akakihadithia mateso anayopitia kutokana na kifo cha mwanae ,machozi yatakutoka. Maana kwa maelezo yake Alfonsi alikuwa tegemeo lake.

Cha ajabu hao viongozi wa chadema waliokuwa mstari wa mbele kumpamba Alfonsi azidi kupata ujasiri wa kusimama majukwaani kupambana na viongozi wa Serikali akiwemo huyo Magufuli, hawana habari naye yule mama.

Anasema mwaka Jana alitembelewa na T.A.L akiwa na sukari kilo mbili ,Mchele kilo tatu, chumvi na sabuni na waandishi wa habari kwaajili ya kurekodi ziara yake hiyo.

Laiti binadamu tungewekeza akili zetu kwenye maendeleo tungeendelea sana. Badala yake akili zetu tumejikita zaidi kwenye migogoro. Unakutana na mtu barabarani kabla ya salamu anakuuliza mbona umekonda sana?. 😆😆Sijui alitakaje........
Sasa mbona huwaongelei waliomkata mapanga huyo mawazo?

Umeambiwa alichokuwa akipigania mawazo kimeachwa, au kinaendelezwa?
 
Sasa mbona huwaongelei waliomkata mapanga huyo mawazo?

Umeambiwa alichokuwa akipigania mawazo kimeachwa, au kinaendelezwa?
Pambania familia yako maana maisha ya Duniani ni mafupi, vinginevyo umeamua kujikita vilivyo kwenye siasa ambazo wengi wa waliofanikiwa kupitia njia hiyo ni wale walio sambamba na mfumo na si kinyume
 
Pambania familia yako maana maisha ya Duniani ni mafupi, vinginevyo umeamua kujikita vilivyo kwenye siasa ambazo wengi wa waliofanikiwa kupitia njia hiyo ni wale walio sambamba na mfumo na si kinyume
Siasa ndizo huamua Kodi kiasi Gani itumike kulipa mishahara ya makamanda wa vyombo vya ulinzi na USALAMA.
 
Magu sikumkubali ila ktk kuchukua maamuzi nilimpa 100%.
Huyu wa sasa hata haeleweki lipi analimudu...kwenye kuchukua maamuzi ndio zero kabisaaa!.
 
Kulikuwa na Shirika la Bahati Nasibu la Taifa na hawa Akina Tarimba wanaowabetisha Leo ndio wametokea kule 😂😂🔥
Wanawabetisha na wanachaguliwa Ubunge pia !
Duh 🙄 lakini No peace of mind 🙏🙏
Dunia rangilangire !
 
Back
Top Bottom