Hayati Magufuli aliweza kuwatisha waovu, mifumo iliamka kufanya kazi

Hayati Magufuli aliweza kuwatisha waovu, mifumo iliamka kufanya kazi

Mama Samia ni kama anahujumiwa au wahuni wamemzidi ujanja.

Kwa sasa hata mifumo ya GePG inasumbua balaa mpaka nahisi wahuni wanafanya kusudi kukwepesha fedha mbona kipindi cha Jiwe haikuwa hivi?

Ishu za umeme ni kama wahuni wanamhujumu Mama

Cha ajabu Mama hachukui hatua naye analalamika kama mimi tu
 
No,

Vyama vya upinzani ni vyama mbadala, jawapasi kupinga Kila kitu,

Jambo lenye maslah ya umma lazima tuwe kitu kimoja,

Walipasa kukubali HOJA ya ujenzi wa HOJA ya BWAWA la JNHP, upinzani wao ungejikita katika kushauri Serikali kutafuta wakandarasi Bora na wenye Kutoa Bei nzuri chini ya wale Serikali iliyowaabgazia,

Huo ndio upinzani wenye TIJA,

Lakini huu upinzani wa kusema ndege hizo ni pangaboi, bazifai chochote,

Kesho yake tunamuona Lissu aliyepinga ununuzi wa ndege akiziita pangaboi, mtu huyo huyo anazipanda,

Upinzani wa aina hiyo Si mzuri.

Upinzani mzuri ujengwe katika Truth, Truth.

Waliendelea na upinzani wa aina hii, Si Rahisi kuaminika na kupewa Nchi.
Ndugu yangu. Naona unahama kutoka ktk nilipo kurejea pale juu.
Itoshe kusema kwamba
1)Haitatokea upinzani ukosekane, whether nzuri au wa hovyo kwa kipimo Chalo.
2)Utatuzi wa changamoto tulizonazo kwa sasa focus ikielekezwa kwa wapinzani eti ndo zitatatuka, ni sawa na kujilisha upepo. ( Hawateui wala kutenguwa, ni wachache, hawajajiri wala kufukuza, hawaelekezi wala kuagiza,.......) Uliowapa mamlaka wamezingua waondoe/ wawajibishe baraka! na si kulalamika.......
3) Kwa Tz, mwenye dola anashape upinzani kama itakavyo mpendeza.
 
Mama Samia ni kama anahujumiwa au wahuni wamemzidi ujanja.

Kwa sasa hata mifumo ya GePG inasumbua balaa mpaka nahisi wahuni wanafanya kusudi kukwepesha fedha mbona kipindi cha Jiwe haikuwa hivi?

Ishu za umeme ni kama wahuni wanamhujumu Mama

Cha ajabu Mama hachukui hatua naye analalamika kama mimi tu
KATIBA imempa nguvu kubwa sana Rais, asipoamua, hakuna kinachosonga,

Umeletewa taarifa na vyombo kuwa pesa zimechotwa pale, Kisha unawaambia nendeni mkalitizame!!

Wao wameshalitizama, ndipo ukaletewa taarifa mezani.

KATIBA ingebadilishwa haraka, akifariki Rais, mchakato wa uchaguzi uanze mara Moja.

Hizo pesa za mikopo zitalipwaje ikiwa zimeibwa kabla ya kupelekwa panapostahili?
 
Kama Magu alikuwa anaiba pesa Kisha anakwenda kujengea Flyovers, mabarabara, Mji wa Magufuli Dodoma na IKULU, Masoko ya kisasa na Bus terminals,SGR,daraja la Busisi, ununuzi wa ndege Kwa pesa alizoiba,

Basi kiongozi Mwizi wa aina hiyo ndiye tumtakaye.

Niliambiwa na mmoja wa watu waliobambikiwa kesi za uhujumu uchumi, wakati wa malipo yale yaliyolazimishwa na marehemu kuwa washtakiwa wote wakiri kosa, ndipo nilipoamini kuwa nchi hii hakuna wa kumwamini!!

Jamaa aliambiwa kuwa ameisababishia Serikali bilioni 1. Kwenye bargain ili aachiwe akaambiwa alete milioni 600. Akaandika cheque, Mganga akaikataa, akadai lazima iletwe pesa cash taslim (lengo lilikuwa isitambulike pesa iliingia kwenye account gani). Akaileta milioni 600, ikapokelewa. Kwenye karatasi aliyosainishwa iliandikwa milioni 400. Yaani Muganga, aliiba palepale milioni 200, na iliyobakia milioni 400, hiyo ndiyo iliyopelekwa Chato.

Pesa yote ya plea bargain, hakuna hata shilingi 1 iliyoingizwa Serikalini. Yote ilinufaisha watu wawili binafsi.

Kuna mambo mazuri alifanya, lakini pia kuna maovu mengi aliyatenda. Funzo ni kubwa sana: unawapora watu mabilioni ya pesa, lakini hupewi muda hata mfupi wa kufurahia uporaji ulioufanya.
 
Huo ni Uzi mwingine kabisa.

HOJA hapo juu ziko wazi kabisa.

Tujikite hapo🙏
 
Mbona sa100 anamlalamikia wizi wa watumishi wanachepusha pesa za miradi zinazotoka hazina Kisha wanahamishia Kwa AC zao? Kwann hachukui hatua?
itakua ndio walimmalizia mzee anaogopa yasijemkuta sometimes tunamlaumu mama bure but behind a scene kuna watu wananguvu sn na hii nchi kuliko raisi mwenyewe
 
Back
Top Bottom