Hayati Magufuli aliwezaje kutunyamazisha Watanzania milioni 60?

Hayati Magufuli aliwezaje kutunyamazisha Watanzania milioni 60?

Ila kwa miaka mitano tuliufyata kama misukule hata angesema kulala saa mbili tungelala
Si kweli....Hii nchi ina majabali ambayo yenyewe kwa muonekano hayatishi na yana sura za bashasha ila hatari sana. Kuna baadhi ya maeneo alikuwa anapawa ushauri na anaufata au analazimika kuufata.
 
Thread imemtaja Kagame, nchi yake unaiona inavyokata mawinbi ya maendeleo?
Rwanda kagame akifa basi biashara imekufa na sidhani kama wana uchumi mkubwa bali wana civilization tu ambayo inasababishwa na nidhamu ya woga
 
Kwahiyo wewe unataka tuwasikilize westerns na majina yao hayo? Huoni kwamba wanawapa hayo majina na ili uamini ndivyo hao hao ndiyo wanatimiza hayo ya kuvuruga efforts za hao watu?

Mandela pia aliitwa gaidi je ni kweli?

Every story has two sides learn to develop your own third story after hearing from both sides
Western huwezi kuwakwepa wala jeuri hiyo hatuna.
Even our children trying to imitate western
 
Nimefurahi zaidi pale Zitto aliposema Màgufool alizuia mgao wa umeme kwa kupunguza kiasi cha umeme wa viwandani na kukipeleka kwenye matumizi ya majumbani

Yule baba alikuwa ni fundi wa mazingaombwe ukitaka ujue hilo angalia jinsi alivyolipaisha deni la taifa kwa kukopa kwenye vijitaasisi uchwara
Chief, ili nisipunguze kucheka lete ushahidi wa hii nukuu:,[emoji23][emoji23][emoji23]

Màgufool alizuia mgao wa umeme kwa kupunguza kiasi cha umeme wa viwandani na kukipeleka kwenye matumizi ya majumbani
 
Membe kitengo yule alitumwa ili kuonekane kuna upinzani .kinana alikimbilia uvunguni kujificha mpaka leo hajatoka uvunguni
Hakukimbia na ndo mtu aliyeweka jeuri hata kwenye kuomba samahani aliiomba kwa jeuri fulani hivi. Fuatilia msamaha alioomba na namna alivyouomba.



Huwezi mwambia raisi wa nchi aina ya JPM uongozi wake ulikukwaza ukakwazika ukatoa maneno ya kejeli halafu ukaendelea kuachwa tu kama ww si mwamba mzito.

Angekuwa keshafunguliwa kesi na yupo ndani.

Kuhusu Membe mtafute musiba akuhadithie kuwa ni kitengo au la?
 
Tangu nikiwa mdogo nilipenda kufuatilia visa vya viongozi waliotawala kwa mkono wa chuma kama vile Stalin, Mussolini, Lenin, Hitler, Suharto Iddi Amin mobutu ,kagame,bokassa na wengineo.

Nikawa najiuliza hawa wababe waliwezaje kuwanyamazisha wananchi wao kirahisi wasipate watu wa kuwapinga?

Hata nikadhani labda wananchi wao ni mazezeta.

Ila alichotufanya bwana yule nilikuja kuelewa somo kwa vitendo,nilipenda sana story za hawa wababe ila ghafla nilijikuta nabadili mtazamo wangu.

Kiukweli kabisa watanzania wote tuliufyata kasoro mtu mmoja tu Tundu Lissu nadhani kwa sababu alishaonja kuzimu labda akaona kumbe hakutishi kivile, tuliobaki tukubali tuliufyata mpaka wengine kufikia kumuita Mungu, nikikumbuka nacheka mwenyewe

Ukatili mkubwa + Kinyongo/roho ya kisasi + Wasio julikana.
 
Tangu nikiwa mdogo nilipenda kufuatilia visa vya viongozi waliotawala kwa mkono wa chuma kama vile Stalin, Mussolini, Lenin, Hitler, Suharto Iddi Amin mobutu ,kagame,bokassa na wengineo.

Nikawa najiuliza hawa wababe waliwezaje kuwanyamazisha wananchi wao kirahisi wasipate watu wa kuwapinga?

Hata nikadhani labda wananchi wao ni mazezeta.

Ila alichotufanya bwana yule nilikuja kuelewa somo kwa vitendo,nilipenda sana story za hawa wababe ila ghafla nilijikuta nabadili mtazamo wangu.

Kiukweli kabisa watanzania wote tuliufyata kasoro mtu mmoja tu Tundu Lissu nadhani kwa sababu alishaonja kuzimu labda akaona kumbe hakutishi kivile, tuliobaki tukubali tuliufyata mpaka wengine kufikia kumuita Mungu, nikikumbuka nacheka mwenyewe
Kuna idadi kubwa ya watu miongoni mwetu wanaopenda utumwa (subservience) mbele ya mtu mbabe na katili wakiamini ndio fursa ya kujipatia upendeleo, ulaji na kushindana usnitch ili kukubalika zaidi na mtemi huyo. Watamnyenyekea na kumtukuza kwa majina kama mwamba, jiwe, chuma - bila aibu. Wakifokewa na kutukanwa hadharani na mtu wa aina hiyo wanaona sawa. Ndio asili ya wengi wetu hasa waliojaa kwenye chama tawala. Wachache wasiokubaliana na hali hiyo watapata tabu sana kupambana na hilo jeshi la misukule.

Historia ya utumwa na ukoloni Afrika inafichua kuwa waafrika weusi ndio walikuwa watu rahisi sana kukamatwa na kuuzwa utumwani na pia kufanywa makoloni, kwa vile kwa kiasi kikubwa, mbele ya wavamizi walikuwa na hulka ya "kusarenda" kirahisi na kushindana kujipendekeza kama njia ya kuepuka maafa na kujipatia upendeleo. Hata watawala wao wa jadi wengi walikuwa wakinunuliwa kirahisi ili wawauze watu wao utumwani. Hii nimeisikia mara nyingi kwa washirika wangu hasa wa Afrika magharibi na kaskazini kwa waarabu. Ingawa siioni mantiki yake lakini inafikirisha sana na haifuraishi.

Tofauti, waarabu na watu waliochanganya damu kama wasomali na wahabeshi hadi leo ni wapambanaji hadi kifo linapokuja suala la uhuru na haki zao. Walikuwa wakisumbua sana huko zamani. Haikuwa rahisi kuwafanya watumwa wala kuwatawala kirahisi kama koloni. Ndio maana kwenye nchi hizo, hadi leo hakuna kulala. Huku kwetu tunaambiwa "amani" ndio kila kitu. Eti bila amani, haki haiwezi kupatikana! Kubisha ni kujitakia tabu ya bure. No overt support from fellow citizens. Lissu tangu mwishoni mwa miaka ya 1990 ameteseka sana kupigania haki za wanyonge kwenye migodi na bungeni anaishia kushambuliwa kwa kauli za kizuzu za "kuunga mkono ushoga"!
 
Ni kweli ila katiba hiyo hiyo ilikuwepo tangu 1977 wenzake pia waliitumia ila tulipumua kidogo
Inahitaji busara sana ndugu... vinginevyo Rais akiwa mshenzi hata huyo JPM atakuwa na nafuu kwa jinsi katiba ilivyompa mwanya wa kufanya lolote atakalo. Na kibaya hashtakiwi kwa makosa yake wakati akiwa kiongozi
 
Sasa kuhusu picha za mababu zetu kuwabeba wakoloni niliwaza baada ya kugundua kuwa wale wakikuwa wakilipwa ujira,ile ilikuwa kazi ya heshima kama kumuendesha kiongozi kwa sasa,kuna marupurupu kwa madereva,wale walikuwa madereva tu tusiwalaumu
Kwamba kwa sasa wao ndio wangekuwa madereva wa magari
 
Unadhan sabaya, makonda na mahta walikuwa na kaz gan?

Nchi nzima alikuwa anaadinda lisu!
Muulize nape alivoufyata hadi kuomba kolabo.

Sio kweli humu JF watu walikuwa wanamsagia kunguni sana mpaka akataka kumfunga MUBYAZI!! Kwenye platforms Nyingine kulikuwa na mahasimu wake kama Shangazi, Maria Sarungi na Prof.Mwandosya mpaka akadukua simu zao!!!
 
Dah hawa wazee wetu walitusaliti sana
Kama JPM hakuzigusa mali na utajiri wa hao wazee, ulitaka wafanye nini? Wao wanaangalia maslahi yao binafsi na familia zao usiwategemee. Ni Sokoine peke yake ndiye aliyekuwa na jeuri ya kugusa maslahi ya untouchables wa nchi hii na kilichompata ulikiona.
 
Familia ya Kim inawezaje kunyamazisha Korea yote?

Unadhani mababu walikuwa hawana akili hadi kuwabeba Waarabu kwenye mabega yao?

In fact ni rahisi Sana,kila sekta hasa vyombo vya Dola unaweka watu royal kwako na wawe wakatili, lazima watu waufyate..

Ila unaowaweka lazima uwalipe vizuri na baadhi ya dili haramu na upigaji unapotezea.

Pia unakuwa na vitengo vya propaganda kila sehemu ni nyimbo zako tuu,hata Nyerere ndivyo alikuwa.

Hapo lazima wote iwe hivi 👇

View attachment 2109240


Miaka 60 ondoa ya JPM imemsaidia nini mtanzania wa kawaida….
 
Back
Top Bottom