Hayati Magufuli aliwezaje kuwa Waziri kwa miaka 20 bila kutumbuliwa?

Hayati Magufuli aliwezaje kuwa Waziri kwa miaka 20 bila kutumbuliwa?

Kwa watoto wadogo na wasiojua mambo wanadhani hayati Magufuli alianza kuwa mkali alipokuwa rais wa nchi tu wakati ukweli ni kwamba Magufuli alikuwa mkali na mfuatiliaji tangu akiwa naibu waziri, waziri na baadae rais wa nchi.

Katikati ya mafisadi wakubwa wa awamu za Mkapa na Kikwete lakini walimwogopa Magufuli na aliwashughulikia kila wizara aliyopelekwa, kwa waliokuwepo kwenye wizara ya uvuvi, aridhi na ujenzi enzi za waziri Magufuli watakwambia moto wake.

Swali la kujiuliza aliwezaje kutekeleza bila kutumbuliwa? Je kwenye baraza la mawaziri la sasa kuna waziri anayevaa viatu vyake? Hata baada ya kuwa rais na kufariki dunia mpaka leo miaka 2 imeisha si Chadema , ACT Wazalendo wala CCM waliokuja na ushahidi usiotia shaka juu ya ufisadi wake licha ya kwamba waliahidi pindi tu atakapotoka madarakani basi watakuja na mikataba ya ufisadi na rushwa kubwakubwa zilizosainiwa na yeye.

Mwezi march 2023 imetimia miaka miwili tangu atutoke duniani lakini mahasimu wake ikiwemo ,Lisu, Lema , Nape ,Makamba, Kigogo bado hawajawaletea watanzania ufisadi wa Magufuli.

kinyume chake wanaendeleza mafanikio na miradi ya awamu ya tano kwa kasi kubwa, walipinga kila kitu lakini sasa wanatumia kila kitu walichokipinga! Mbowe akimaliza kutukana anakimbilia kupanda ndege mpya ya Dreamliner impeleke KIA.

Walioahidi kuifunika legacy kumbe hawana uwezo kuifunika hata kidole chake tu!!

Muda utawaumbua zaidi.
Umesahau jinsi alivyolitia hasara taifa kwa kukamata meli ya uvuvi ,bila kufuata sheria za kimataifa!!wataalam wa maritime laws walimshauri wapi,yeye anataka sifa aliwasikia!!leo kuna deni kama la trilioni 3!!
 
Alipochukua mamlaka isiyo yake ya kutoa roho katika miili ya walioumbwa na Mungu, ndipo yote mema yalipofutika juu yake. Kamwe Mungu anapokuinua usijaribu kumpinga Kwa kutoa roho zisizo na hatia kisa tu wanapinga Kwa maneno matendo yako.
Pumbavu
 
Lini unapeleka ushahidi mahakamani?
 
Alikoswakoswa kutumbuliwa.
Nakumbuka nilikuwa Mara naongea na Radio moja nasema,"Haya mambo Magufuli asamehewe. "
Nilikuwa nina mambo mawili ya kusema siku ile;Magufuli asamehewe na yule Sheikh Ponda atolewe jela kule Morogoro.
Asamehewe nini? Hata sikumbuki kulikuwa na ubishi gani.
 
Kisa cha Daniel nyakati za Dario mmedi, ni relevant sana na stori ya Magufuli, huyu Bwana pamoja na kwamba anatafutiwa ubaya hata angali amekufa, atazidi kung'aa.

Sikuwahi kuona baya lake aisee, ni binadamu ndiyo na hakosi madhaifu kama binadamu, lakini alikuwa na nia thabiti ya kuliponya na kuliokoa taifa, alikuwa na maono na ninajua tungekuwa mahali tunakopaswa kuwa kama angalikuwapo.

Tutamkumbuka hata baada ya miaka mingi huyu kiongozi hodari.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kweli mkuu inaumiza sana
 
Alipochukua mamlaka isiyo yake ya kutoa roho katika miili ya walioumbwa na Mungu, ndipo yote mema yalipofutika juu yake. Kamwe Mungu anapokuinua usijaribu kumpinga Kwa kutoa roho zisizo na hatia kisa tu wanapinga Kwa maneno matendo yako.
Hii weakness yake kubwa ya kutopenda kupingwa ili m cost pamoja na dhamiri yake njema...
 
Back
Top Bottom