Hayati Magufuli anashambuliwa kila kona. Siyo kesi, ila mambo yaende; yasipoenda wananchi watawazomea kila kona

Huu ni mtazamo wako mnufaika? Hali ni tofauti Sana huku ground kwani Ile furaha iliyokosekana kwa miaka 6 imerejea kwa kasi ya ajabu!
Chuki kweli ni wazi mno Sasa hivi hasa kwa waajiriwa wa kada mbalimbali za serikali morali ya kazi imeongezeka mno baada ya kufanya kazi kwa tension bila maslahi yao kujaliwa!
Wananchi wamemchukia zaidi baada ya ripoti ya cag kuwekwa hadharani na ufisadi wa serikali yake kupitia miradi kanjanja! Yaani watu wanamponda mno kitaa!
 
Mwenda zake alikuwa hapendwi ndio maana kampeni zake alifanya mchana tofauti ilivyozoeleka ili watumishi wa umma na wanafunzi wakajaze uwanja na Mataga wakasombwe kutoka mbali ...Mama shika hapo hapo mpaka wataelewa ...
 
Kijana shirikisha ubongo na akili kwa pamoja kwenye ku reason mada zako. Hakuna mtu anamu attack Marehemu Magufuli. Ni vitu vinajitokeza au vinatokelezwa na sasa vinaonekana. Bahati mbaya wakati wa utawala wake hakuruhusu hii.

Nikuulize kitu kirahisi kabisa, hivi unajua huyu CAG yeye Marehemu ndio alimleta baada ya kumtoa wa mwanzo? Sasa unahisi huyu CAG anamzunguka Marehemu?

Kwa uelewa wako, Marehemu alisema ATCL imepata faida ya bilioni 28 na huyu mtaalam wa ukaguzi anasema tumekula hasara ya mabilioni hapa unapendekeza tumuamini nani?

Unaamini Marehemu alikuwa ni binadamu wa kawaida na hence sio perfect au unawaza alikuwa Mungu ambae hakosei? Kama ni binadamu wa kawaida kwann unasumbuka kusikia anakosolewa?

Nikushauri kitu, kila uongozi una namna yake ya kutawala, utawala wa Magufuli ulishapita jifunze ndani ya moyo wako kuamini kuwa Magufuli amekuja na ameondoka sasa ni mama Samia. Nae atakuwa na mazuri yake na mapungufu yake na hazimiki kufuatisha mtindo wa utawala wa Magufuli. Yeye ni Rais kamili na ana uhuru kupanga serekali yake anavyoona yeye inamfaa
 


Mmesikia serikali ya wanyonge? Serikali takatifu ya shujaa wa Afrika, tuliyeambiwa amefuta ufisadi? Ngoja nikutajie machache;
Ujenzi wa SGR umesababisha hasara ya 3.5Bil kwa kuajiri wafanyakazi wa kigeni wasiokua na vibali.

Kigwangala alitumia 172M kuandaa Kili challenge lakini pesa hizo hazijulikani zilitumikaje (hazina risiti).

Akaunti ya jeshi la zimamoto ilitumika kupitisha 261M. Yani watu walipiga "mchongo" wakakosa akaunti ya kupitishia, wakatumia akaunti ya zimamoto. Zilipoingia wakazitoa wakasepa. Just imagine watu wana ujasiri wa kupitisha pesa chafu kwenye akaunti ya jeshi? Halafu tunaambiwa mwendazake alinyoosha nchi.
Wasafi walipewa 140M, TBC 201M na Clouds 629M kutangaza tamasha la Urithi Festival. Lakini hakuna mkataba wala risiti yoyote ya kujustify malipo hayo.
18Bil zilizokusanywa ktk wilaya 135 hazikufika serikalini. Yani zilikusanywa lakini wajanja wakalala nazo mbele.

3.9Bil zilitolewa kukarabati ndege ya ATCL iliyopaki tangu mwaka 2015, lakini hela imeliwa na ndege haijakarabatibwa. Yani watu walitafuna milioni 3,900 halafu hawakupaka hata rangi.Hayo ni baadhi tu ya "madudu" ya serikali takatifu ya mwendazake. Sijaongelea HESLB, TANAPA, TANROADS, SGR, Stligler's gorge, Stand ya Magufuli. Huko kuna madudu ya kutisha.

Lakini tuliaminishwa serikali ya mwendazake haikua na doa. Watu waliokosoa waliitwa vibaraka. Serikali takatifu haikutaka kunyooshewa kidole.
Tujifunze kutofautisha mtu msafi na anayeficha uchafu. Mwendazake hakua msafi bali alijua kuficha uchafu. Ndio maana akaminya uhuru wa habari. Hatukusikia skendo kama za Escrow tukadhani serikali yake ni safi, kumbe kuna skendo kubwa zaidi ya Escrow lakini zimefichwa uvunguni.Ndio maana nasema afadhali JK aliruhusu media ziwe huru. Skendo za Richmond, EPA, Escrow aliacha wananchi wajue. Lakini mwendazake alifunika skendo zisifike kwa wananchi.


Ndio maana watu wamemtania CAG atoe pia ripoti aliyopanga kumpa mwendazake, maana angekua hai asingethubutu kusema ATCL imepata hasara ya mabilioni, au SGR imeleta hasara, au mradi wa Stigler's umejaa madudu. Angeficha kwa sababu ndivyo mwendazake alivyopenda.

Tunahitaji viongozi wasafi, sio wanaojua kuficha uchafu.!

By Malisa Godlisten
 
 
NAONA BAADA YA KUFIKA CHATO NA KUKOSA UONGO WABAYA WAKE WANATU'MIA RIPOTI T YA CAG KUMCHAFUA.


ALIPOKUWA HAI WALIMUITA "MSHAMBA"

KABLA TULIAMINISHWA CHATO IMEJENGWA MAHEKALU KWA MABILLION, KILA KITU KIPO CHATO. WATANZANIA WAMEFIKA NA WAMEIONA CHATO NA MAKAZI YA JPM

KUIZIMA NYOTA YA JPM ITAKUWA NGUMU SANA
 
Ule uporaji wa kura ndo unaita uchaguzi!!
 
NAONA BAADA YA KUFIKA CHATO NA KUKOSA UONGO WABAYA WAKE WANATU'MIA RIPOTI T YA CAG KUMCHAFUA.






KUIZIMA NYOTA YA JPM ITAKUWA NGUMU SANA
Pambaneni na ripoti acheni kutupigia makelelr
Mbona mliamini maripoti yake ya makinikia ya akina Mruma wakati ni ya kupika kabisa!
 
Kweli kabisa

Report imesomwa jumapili
 
NAONA BAADA YA KUFIKA CHATO NA KUKOSA UONGO WABAYA WAKE WANATU'MIA RIPOTI T YA CAG KUMCHAFUA.






KUIZIMA NYOTA YA JPM ITAKUWA NGUMU SANA
Nani anaizima? Tatizo la ukweli huwa unashinda tu. Kama hakuna ufisadi itakuja kujulikana tu. Ila kama ulikuwepo basi wakati wa ukweli umefika. SSH amepewa nchi lazima aeleze wananchi amepewa nchi iliyo katika hali gani. Kama ni muongo ni suala la muda tu ukweli utakuwa wazi.
 
Usimtishe SSH. Hao kska zako wakikosea wasisemwe? Ukweli usisemwe? Kumbuka hata mjomba wako alikuwa akisisitiza.."msema kweli ni mpenzi wa Mungu" [emoji1787][emoji1787] au nasema uongo ndugu zangu?
 
Mtu mnyonge wa chini haangalii Makaburasha ya CAG wala hata hamjui CAG ndio nani na hahitaji kumjua .Yeye anaangalia mwanawe anaenda shule bure msingi hadi sekondari ? Vituo vya afya vipo? barabara zipo? Maji yapo? Machinga na mama Ntilie mazingira yako mazuri yapo? Hayo Magufuli alihangaika nayo na wanyonge wakamkubali hayo ya CAG mbaki nayo nyie msio wanyonge
 
Unahisi mambo gani yalikua yanaenda kwa kasi wakati wa Magufuli na yatakwama baada ya wakati wa Magufuli?
 

Mkuu Serikali ya wanyonge ilikuwa imemaliza ufisadi ,sasa "SIEIJII" mbona analeta mshikoror mageni?
 
Ni mti wenye matunda mengi, hivyo pia mawe yanayopigwa Ni mengi.
Hapa viongozi wenzake wanaotawala muda huu waongeze umakini.
Kama ulivyosema mwandishi, mawe yote yapigwe lakini ile kasi ya maendeleo tuionayo wananchi
Iendelee.
Naona vyama vya upinzani wanna matumaini makubwa kushinda uchaguzi ujao kupitia mdundo huu wa muziki.
Kila la kheri , huenda mkashinda kiulaini saana..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…