Huu ni mtazamo wako mnufaika? Hali ni tofauti Sana huku ground kwani Ile furaha iliyokosekana kwa miaka 6 imerejea kwa kasi ya ajabu!Spidi aliulypkuwa nayo Marehemu Magufuli ya kufanya mambo yaende na kufanyika kwa kasi inayoonekana wazi kwa kila mtu, ichallenge kwa waliopo iwe serikalini au bungeni au Mahakamani.
Matarajio ya wananchi ni kuwa spidi itakuwa kubwa kuliko ile au itabaki ile ile.
Sasa hivi Marehemu anapondwa sana kuwa ohh alikuwa dikteta mara ohh alikuwa fisadi mara ohh staili yake haifai
Hakuna shida; cha msingi wananchi wanataka mambo yaende. Tukaneni matusi yote ila mwisho wa siku wananchi watalinganisha output yenu watukanaji na ya Magufuli kwenye kugusa maisha ya wananchi wanyonge
Marehemu Magufuli kila kona anakuwa attacked siyo kesi ila mambo yaende yasipoenda wananchi watawazomea kila kona Kila mtakakopita wadhalilisha Magufuli. Mtazomewa na kuambiwa Magufuli angekuwa hai hili lingefanyika na watawazomea.
Chuki kweli ni wazi mno Sasa hivi hasa kwa waajiriwa wa kada mbalimbali za serikali morali ya kazi imeongezeka mno baada ya kufanya kazi kwa tension bila maslahi yao kujaliwa!
Wananchi wamemchukia zaidi baada ya ripoti ya cag kuwekwa hadharani na ufisadi wa serikali yake kupitia miradi kanjanja! Yaani watu wanamponda mno kitaa!