Hakuna anayempaka matope. Hiyo ni rangi yake halisi.
Yalikuwa maendeleo ya vitu bila kujali watu.
Kuhamia Dodoma kwa hoja za 1973, enzi za Analogia, leo enzi ya digitali wala hapakuwa na haja. Unajenga ikulu mpya wakati tayari unayo, watu wako wanateketea katika ufukara?
Unaanzisha tuuu kwa ushamba wako, eti mradi wa ndege. Mwaka mmoja tu zimeliwa Bilioni 60. Hapo gharama za kununua bado. Hiyo pesa inatoka wapi?
Miradi yako inatia hasara kila uchao. Unaziba vyombo vya habari watangaze mazuri tu. Wakusifu na kukuabudu, umekuwa mungu?
Tunataka maendeleo ya watu. Hii kuacha watu waseme kwa uhuru tayari ni maendeleo.