..nimekutolea mfano wa mfalme Sauli watu walimpenda kwa sababu alikuwa hodari kupigania watu wake..PRIDE/KIBURI kilimponza..maneno aliambiwa ya mwisho, KUTII NI BORA ZAIDI YA KUTOA DHABIHU..Mungu aliondoa ulinzi wake kwake mfalme hata Nabii Samwel alipomtetea kwa kuugua sana, aliambiwa NIMEMKATAA SAULI..!
Pamoja na mazuri yote Magufuli alifanya na kupendwa sana..KIBURI cha kusifiwa kilimponza Mungu akachora mstari, na alishaambiwa hakusikia, uchaguzi wa 2020 ulionyesha kiwango cha juu cha kiburi cha madaraka..yuko wapi sasa!
Kifo kipo kwa kila mtu, lakini jifunze kutenda mema kwa wote! na hasa unapokuwa kiongozi..! Hayo aliyokuwa anayakataa, wizi, ufisadi, uzembe nk yote yamerudi mara 5 zaidi na hao aliowafukuza kuwa hawafai kuwa viongozi wote wamerudi..wewe huyaoni hayo? unamsifu kwa lipi hasa km Mungu aliamua kumtoa kwenye hiyo kazi? Sasa kwa vile wewe ni kipofu kiroho huwezi kuona na kutafsiri matukio..usidhani na wengine ni km wewe.