REJESHO HURU
JF-Expert Member
- Mar 6, 2014
- 5,283
- 11,558
- Thread starter
-
- #41
Uyo haelewi kitu yupo kuimba iyena iyena watunahoji vitu vya msingi yeye analeta porojoIla ameandika ukweli, ccm imeiba mali za serikali kuanzia viwanja vya mipira, kumbi za starehe, maeneo ya wazi lakini leo wapo mlimani city kukamua watanzania, huoni kama Magufuli alikuwa sahihi?
The man, the myth, the legend.Tunakumbuka uliposhika uenyekiti wa chama uliunda tume ikatembea inchi nzima kukagua mali za chama na ukataka chama kijiendeshe kwani kina vyanzo vingi vya mapato na hilo tuliliona wale wote waliopanga maeneo ya chama walilipa kwa control number ili kuepuka mambo tuliyaona jamaa pale kwenye harambee kuepuka kundi fulani fulani kuhodhi chama na kuendesha mambo yao.
Tusamehe Magufuli tulikukosea sana.
Leo hii CCM yakuitisha harambee na kuchangiwa mali za chama zinafanya nini mapato ya mali ya chama yanaenda wapi inasikitisha sana tena sana.
Tusamehe Magufuli tumeanza kumbuka kauli yako nchi hii tajiri na tumeona mtu anachangia bilion kumi, milion mia tano uyu ni mtu mmoja mmoja.
Magu alikua na Mabaya yake ila Mazuri yalikua mengi sana Magu akutaka ubabaishaji ukajanja ndo maana wakandarasi kipindi cha Magu hawawezi kumsahau. Unafanya kazi yako nzuri unalipwa wahuni wahuni wazee wa short cut Magu ndo alilala nao mbele na ndo wengi wanaomchukiaDangote ana sign mkataba wa kujenga kiwanda cha Mbolea kitakacho gharimu $3 billion na serikali ya Ethiopia kabla week hii aijaisha.
Kiwanda ambacho aliahidi kwa Magufuli atakijenga Tanzania. Lakini baada ya wahuni na umeme wa uhakika kupotea kabadilishia gia angani.
Kiwanda ambacho kitakuwa mzalishaji mkubwa wa mbolea Africa nzima. Sasa imagine costs ambazo nchi ingeokoa kuagiza mbolea.
Kiwango cha gas ambacho nchi ingeuza kwa Dangote ni bidhaa muhimu kwenye uzalishaji, ajira na si ajabu angeteneza umeme wake na ziada kuuza kwenye gridi ya taifa.
Walichofanya hadi Dangote kwenda Ethiopia wanajua wenyewe huko serikalini; mradi tu watu wabaki na tender zao za kuagiza mbolea.