Hayati Magufuli ni shujaa anayepigana na walio hai

Hayati Magufuli ni shujaa anayepigana na walio hai

"Eti shujaa anayepigana na waliokuwa hai" hivi kweli umekosa dhihaka nyingine mpaka ukaona utumie hiyo?..bado najiuliza nyie mnaoibuka kumtetea shujaa wenu nani anakuwa nyuma yenu kwa sasa
 
Mtoa mada utashambuliwa kinoma , jukwaa la siasa wapo wenyewe waliofurahia kifo cha mpendwa wetu.

Wana ID's za kutosha kwa kazi hii maalumu.
 
Nimekuwa kimya kwa siku mbili tatu ili kujipa muda kuifuatilia na kutafakari FILAMU inayochezwa na CAG akishirikiana na wanamapinduzi wanaopambana usiku na mchana kuifuta LEGACY ya MWAMBA HUYU KUTOKA CHATO...
Kafa. Kwisha habari yake. Kwishnei. Yupo 6m deep. Powerless. Helpless. Ubabe-less. Jeshi-less. Bodyguardless.

Hakuna yeyote anayepigana na mtu aliye katika hali hiyo. Watu tupo bize kuondoa uchafu na takataka alizoziacha. Basi.
 
Kwani bado mnalipwa zile buku saba na Chakubanga?

Usisahau kuweka namba zako... Kuna teuzi zinakuja
 

Ngaliwe

Story ndeefu hata hujataja miradi ya kijiji cha Chato eti iwe Mkoa
Mwinyi tu kashangaa hicho kijiji hakikumbuki wakati kina traffic light akachepusha barabara ya Biharamulo mara tu alipoukwaa unaibu waziri wa Ujenzi.
Ndio leo uje ujue kwanini alikuwa hapandi ndege kwenda nje ya nchi, maana huko taka usitake utapitshwa kwenye ukaguzi km umebeba metal mwilini mwako (maana yake ulikuwa na umeme mwilini mwake.
Ni ujinga kubomoa miradi iliyokuwa ya waanzilishi wake yeye kaja malizia
siku za mwendazake zimeisha hebu tumsahau sasa utawala wa kidekteta
 

Ngaliwe

Story ndeefu hata hujataja miradi ya kijiji cha Chato eti iwe Mkoa
Mwinyi tu kashangaa hicho kijiji hakikumbuki wakati kina traffic light akachepusha barabara ya Biharamulo mara tu alipoukwaa unaibu waziri wa Ujenzi.

Ndio leo uje ujue kwanini alikuwa hapandi ndege kwenda nje ya nchi, maana huko taka usitake utapitshwa kwenye ukaguzi km umebeba metal mwilini mwako (maana yake ulikuwa na umeme mwilini mwake.

Ni ujinga kubomoa miradi iliyokuwa ya waanzilishi wake yeye kaja malizia. siku za mwendazake zimeisha hebu tumsahau sasa utawala wa kidekteta
 
Nani alikuambia eti ukipanda mchicha unaweza vuna mahindi?

Mwendazake mliwabagua watu wazi wazi, wapinzani walionekana kama sio raiya wa nchi hii, Tundu Lissu alipopigwa risasi mchana kweupe mliona kama ni kuku na sio binadamu hivyo hamkujali.
Nyerere alisema Dhambi ya Ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu, ukishaitenda hii Dhambi lazima ikufuate mpaka nyumbani kwako.

Kingine hili taifa ni Mungu ndio analilinda hivyo usiwe na wasiwasi eti ccm ikisambaratika hili taifa nalo litasambaratika. Naomba nikutie moyo kuwa kwa sasa Mungu analiangalia taifa lake Tanzania hivyo tunapaswa kufanya maombi ya shukrani kwa kila badiliko analolifanya kwa nchi hii.

Mwana ccm ni ngumu kujua ni kiasi gani cha maumivu waliyoyapata watu wasio wanaccm Hususani viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani kipindi cha Mwendazake.
Watu wameumizwa, watu Wamelia pasipo kumsikiliza ila siku zote chozi la mnyonge aliendi bure.

Ngoja nikupe mfano mdogo,mwaka jana 2020 tulikuwa na uchaguzi mkuu na toka zoezi la uchukuaji form na hadi kuridisha form mpaka kampein na siku ya upigaji kura na mpaka kutangaza Matokeo mgombea kupitia upinzani hakuna rangi aliacha kuona.
 
Mtu aliyetamka hadharani hatapeleka maendeleo kwa majimbo ya upinzani, anapataje watu wa kumtetea? eti mpasuko! acheni watu watoe sumu ili utafutwe muafaka wa kuwaunganisha
 
Wanao muunga mkono Samia hawataki ya magufuli yajirudie
 
Kwa wiki sasa naona trend ya namna mijadala inavyoendelea kwenye mitandao na vikundi vya WhatsApp vimenifanya nifikirie sana na nimeona nitoe mchango wangu kidogo tu ili kujitahadharisha na kuwahatadharisha wenzangu wasiingie kucheza kwenye ngoma wasiyoijua vizuri kama ni ngoma ya jando au ya kumtoa mwali...
Aisee, unahangaika sana Mzee.

Hizo hela za Doto James (mtoto wa dada) zikimkaukia tu, mtatoweka wenyewe hapa jukwaani.

Maana naona una "bank file" la post za kujaribu kumsafisha Mwendazake.

Ukimaliza kupost hii, unarudi tena na kuja na nyingine..

Pole sana. The Magufuli Chapter has been closed....
 
Nimekuwa kimya kwa siku mbili tatu ili kujipa muda kuifuatilia na kutafakari FILAMU inayochezwa na CAG akishirikiana na wanamapinduzi wanaopambana usiku na mchana kuifuta LEGACY ya MWAMBA HUYU KUTOKA CHATO...

Maeneo aliyopatia mno ni haya....

1. Kurejesha Nidhamu kwa Watumishi
2. Kutupa Ujasiri Watanzania
3. Kutuchangamsha Kifikra
4. Kujituma kwa Maendeleo yetu
5. Kutuvumbua Wabongo tusiyoyajua
6. Kujiamini kwa Watanzania
7. Kukusanya Kodi kwa Uwingi

Maeneo aliyoharibu sana ni haya....

1. Ukabila wa wazi kwa Wasukuma
2. Ufisadi wa Kimkakati
3. Kuminya Uhuru wa Habari
4. Kuisigina Demokrasia ya Tanzania
5. Kukurupuka katika Miradi mingi
6. Kutoheshimu Professionalism
7. Visasi na Ukatili wa Kimakusudi

Hivyo Kwangu nampa tu 50 / 50 pekee.
 
Ni vizuri kuwa na akiba ya maneno,kuna wakati babu aliniambia hivi ukichukua bia ukaimiminia kwenye chupa ya soda halafu ukawaambia watu unakunywa bia hv watakuamini.

Lengo hapa ni kuitoa CCM madarakana na kuipumzisha tu ndio dawa pekee iliyobakia kwa TANZANIA hii hizi ngonjela nyingine za minyukano ya kusifu na kuponda viongozi wa CCM wakati tunajua CCM ilishaoza zamani hazina maana yoyote na hatuna cha kutarajia kutoka kwa viongozi wa CCM zaidi ya UFISADI na wizi wa mali za umma.

Tuungane watanzania tuipumzishe CCM na wala tusichezewe akili tukaanza kucheza ngoma ya CCM tutakwisha tusijaribu kabisa ni wakati wa kuweka mikakati madhubuti bila woga wala hofu.
 
Nimekuwa kimya kwa siku mbili tatu ili kujipa muda kuifuatilia na kutafakari FILAMU inayochezwa na CAG akishirikiana na wanamapinduzi wanaopambana usiku na mchana kuifuta LEGACY ya MWAMBA HUYU KUTOKA CHATO...
Wanaomchafua JPM hawafai kuitwa watanzania
 
Mbaya zaidi wizi na uhuni wake umeibuka wakati ambao hawezi tena kujisafisha isipokua kuhangaika na adhabu kabri
 
Acha watu waongee wanachokiamini.

Hakuna mpasuko wala nini hiyo ni hofu yako tu, kama yapo yataongelewa na kujadiliwa kwa kina. Kama mtu kapendelea ukanda fulani tusiseme kisa kuogopa huo mpasuko ilhali ni kweli jambo lipo.

Hakuna mpasuko utakaotokea ni kawaida kwa kila awamu kuibuka watu wenye fikra tofauti na ndio ubinadamu, usitegemee kukawa na kundi moja tu, lazima wawepo waliotofauti na kundi la kwanza, waliotofuti na makundi yote 2, wasio na upande wowote na wasiojua kinachoendelea kabisa. Kila mtu atachangia kulingana na kundi alilopo kwenye kila mada itakayoletwa mezani.
 
Back
Top Bottom