Hayati Magufuli ni shujaa anayepigana na walio hai

Hayati Magufuli ni shujaa anayepigana na walio hai

Mashujaa wangu mimi ni wapinzani waliokomaa mpaka dakika za mwisho, bila kujali ushujaa wa Magufuli.
 
jamaa analialia tu sijui aliahidiwa "mavyeo"...pambana kivyako mkuu mambo yamebadilika!.
 
Uzi mrefu na hauna la maana..I feel sorry kwako kwa kupoteza muda wako.
 
Mimi hata picha ya Magufuli sitaki kuiona hata stori zake sitaki kuzisikia.
aoze kwa amani
 
Hata ipite miaka kumi elfu na maelfu yake, bado "MAGUFULI THE GREAT, IN AFRICAN POST- COLONIAL HISTORY", anaendelea kung'ara kwa upekee wake.
kama utakuwepo hiyo miaka 10000. but then ni suala la muda tu.
 
, “Laiti ungalijua hata wewe katika siku hii yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako. Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke, watakuzingira na kukuhusuru pande zote; watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutabua majira ya kujiriwa kwako.”
Ujumbe mujarabu kwa Tanzania huu.
 
Na Mwananchi Mwenye Hasira

1. Umetimiza vyema wajibu
Kwa Mungu na kwa Taifa
Tanzania mpya endelevu
Liijenga kwa moyo wa dhati

1. Takukumbuka Daima
Kwa nidhamu na utu
Kwa kila mwananchi
Alijisikia mwenye nchi

2. Ulikomesha unyonyaji
Uonevu na dhuluma
Rasilimali ukailinda
Dhidi ya beberu na lowezi

3. Afrika na dunia inakiri
Meacha alama ya ukombozi
Ukombozi wa mwafrika
Dhidi ya ukoloni wa kileo

4. Historia itakuandika
Kwa herufi za dhahabu
Miaka mitano na nusu
Itakumbukwa daima dumu

5. Wapo wanaokupuuza
Wakuzodoa kila uchao
Wengine uliowabeba
Wakasimama siasani

6. Sasa wamekuwa Yuda
Mwana yule wa Iscariot
Unafiki umetamalaki
Eti ulofanya si chochote

7. Twasikiliza tukilia
Tukililia Tanzania
Wameshika hatamu
Utamu kwao mekolea

8. Hawajali tena wanyonge
Wakuona wewe kislani
Baba tulia pumzika
Yao dawa twaitokosha

9. Sisi tulokuheshimu kwa dhati
Wananchi wana wa Tanzania
Wazalendo wasiotiliwa shaka
Sisi wachuuzi na machinga

10. Ndiyo takao wahukumu
Siku yao kiwadia
Na haiko mbali vile
Wakae wakijua hilo

11. Watakuja kwenye kura
Swali moja twawauliza
Vipi ‘Legacy’ ya anko Magu
Wewe u pamoja au kinyume?

12. Wengi shajipambanua
Walikuchekea kwa inda
Nyoyoni walijaa husuda
Mahasidi walozea kwiba

13. Sasa wako mbiombio
Kufuta urithi wako wote
Wataka tukusahau mara
Waturudishe ‘utumwani’

14. Hakika wajidanganya
Janja yao ya kupora kibeberu
Tushawajua kwa majina na vyeo
Twaomba 2025 iwadie tutambuane

15. Walizoe wa kunyonga
Vya kuchinja viliwashinda
Sasa wanajua meondoka
Wanataka tena kunyonga

16. Muda wanapoteza bure
Watanzania twajitambua
Tunataka legacy ya anko Mangu
Kulinda rasilimali za umma

17. Atakaye kinyume na aje
Vijana mesimama imara
Tanzania kuilinda vyema
Kuenzi mema yako yote

18. Sisi tumegomboka
Kwa majitoleo yako
Aliye kinyume chako
Yu kinyume chetu pia

19. Tumesimama imara
Wenye kupuuza jueni
Tutakutana sandukuni
Kishafika ishirini ‘shirini na tano

20. Twamuomba Jalali
Akutunze kwake pema
Pepo njema akujalie
Uiombee Tanzania ulioipenda

ASANTE JOHN
 
1618236301909.png
 
Fedha sasa inaingia jana nimeshika Alfu hamsini kutoka kwa jamaa yangu aliyerejea Nchini Tanzania

Ameniambia akaunti zake zimefunguliwa na ameruhusiwa kupiga mzigo

Asante Mama, Bundi katuondokea furaha tele
 
Fedha sasa inaingia jana nimeshika Alfu hamsini kutoka kwa jamaa yangu aliyerejea Nchini Tanzania

Ameniambia akaunti zake zimefunguliwa na ameruhusiwa kupiga mzigo

Asante Mama Bundi katuondokea furaha tele
Hakika MUNGU ameliokoa taifa
 
Na Mwananchi Mwenye Hasira

Mzee wetu Mzee Ally Hassan Mwinyi,alisema "Maisha ni hadithi tu"ewe mwanadamu kuwa hadithi nzuri,Hayati John Pombe Magufuli yeye tayari ameshaandika hadithi yake si jambo rahisi kuifuta unless ubomoe kila kitu alichowaza, alichofanya na alichojenga uanze zahanati 400 alizojenga,Shule zote za sekondari za zamani alizozijenga upya,kuiharibu hadithi ya Hayati Rais John Pombe Magufuli labda uvunje meli 9 kubwa mpya alizojenga ziwa Tanganyika,Ziwa nyasa na ziwa Victoria,uvunje daraja la Busisi la Ziwa Victoria la kilomita tatu na nusu,na daraja baharini la kilomita moja Tanzanite pale Surrender.

Kuharibu hadithi ya Hayati Rais John Pombe Magufuli labda uvunje Ubungo Exchange,uvunje stand za mabati mpya za kisasa alizojenga kila Mkoa katika mikoa yote 30,uvunje masoko makubwa mapya ya kisasa aliyojenga katika mikoa yote 30 ya Tanzania,uyavunje mandege 11,ubomoe reli ya Umeme na reli ya kwenda Moshi na Arusha,ubomoe madaraja na bwawa la Umeme la Rufiji zaidi ya hapo mtu kumchafua ni kupoteza muda tu,kwanza si nidhamu,si hekima,si busara na si Utamaduni wa Mtanzania.

Hayati Rais John Pombe Magufuli ameandika hadithi ya kujenga mradi wa umeme mkubwa,Bwawa la Rufiji (Bwawa la Mwalimu Nyerere) unaozidi uwezo wa umeme wote unaozalishwa tangu mkoloni,Nyerere,Mwinyi,Mkapa na Kikwete na Sasa hakuna tena mgao wa Umeme,tutapata Umeme na kusaza,tutasahau habari ya iptl,dowans,Richmond na Escrow!.

Hayati Rais John Pombe Magufuli ameandika hadithi ya kujenga Reli ya Umeme,Reli ya kisasa yenye uwezo mkubwa wa kwenda kwa haraka na kubeba mzigo mkubwa kuliko Reli zote nchini,Treni ambayo itatumia saa moja na nusu toka Dar hadi Morogoro,na Massa matano tu toka Dar hadi Mwanza,hii itafanya kuharakisha Maendeleo,badala ya kusafiri Masaa 17 toka Dar hadi Mwanza.

Hayati Rais John Pombe Magufuli ameandika hadithi ya kujenga maghala ya kutunzia vyakula kwa mikoa yote inayozalisha vyakula kwa hifadhi za taifa letu,Sasa Taifa litakuwa na hifadhi ya kutosha ya Mazao ya Chakula.!.

Hayati Rais John Pombe Magufuli ameandika hadithi ya kufufua shirika la ndege la atcl na ununuzi wa ndege zake kumi na moja kwa ajili ya kukuza na kuboresha sekta ya Utalii,hivi sasa tunashuhudia Watalii zaidi ya 1,000 wakitua nchini.

Hayati Rais John Pombe Magufuli ameandika hadithi ya kutoa ruzuku ya kielimu ( elimu bure) kwa shule za misingi na sekondari,hivi sasa hakuna mtoto asiyejua kusoma wala kuandika.!.

Hayati Rais John Pombe Magufuli ameandika hadithi ya kujenga hospitali kwa wilaya zote ambazo hazikuwa na hospitali za wilaya na vituo vya Afya zaidi ya 300 nchini baada ya kuvikuta vituo 67 tu!

Hayati Rais John Pombe Magufuli ameandika hadithi ya kumalizia miradi iliyoanzishwa na watangulizi wake ambayo ilikwama kuendelea baada ya pesa kupigwa ama ujenzi usioridhisha kama barabara,Madaraja,Viwanja vya ndege vya zamani na Vipya,Kujenga barabara za juu na zile za kukatisha bahari ya hindi na kule ziwa Victoria na vivuko mbalimbali.

Hayati Rais John Pombe Magufuli ameandika hadithi ya kuendelea kujenga miundombinu ya bandari na ujenzi wa meli mpya kwa maziwa ya Nyasa,Victoria na Tanganyika!.

Hayati Rais John Pombe Magufuli ameandika hadithi ya kuwa Mzalendo na ayafanyayo yapo damuni,ukimchana hivi damu yake ilikuwa inasema Mimi ni Mtanzania,nitapenda kuiona Tanzania ikiwa Taifa kubwa kama China.

Hayati Rais John Pombe Magufuli ameandika hadithi baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuanza miradi mingi nchi nzima,miradi inayoonekana kwa macho na sio miradi hewa ama ya kitapeli kama miradi tuliyowahi kuisikia siku za nyuma,Miradi inayofanyika sasa na inayoonekana wazi na Wananchi wanapata faraja,ni miradi ya barabara nchi nzima,meli,vivuko,umeme,maji,afya,utalii,bandari,na viwanja vya ndege,Siku za nyuma tulikuwa tunaambiwa maneno tu ama kuishia kuona ujenzi usioridhisha.

Hayati Rais John Pombe Magufuli ameandika hadithi mwaka 2016 pale alipoanza kwa vitendo na watu waliita nguvu ya soda,lakini siki zilivyozidi kwenda watu waligundua si povu wala nguvu ya soda bali mtendakazi yupo kazini.Ujenzi ulioanza na kumalizika ulitoa picha ya utendaji wa kutukuka katika awamu hii ya tano,Mwaka 2016 tulianza kuona matunda halisi ya maneno,ahadi na utendaji kazi wa Awamu ya tano.

Hayati Rais John Pombe Magufuli ameandika hadithi kwa kujenga hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza,Kota za Magomeni takribani ghorofa 30 zenye ghorofa 10 kwenda juu,Hayati Rais John Pombe Magufuli ameandika hadithi kwa
Ununuzi wa Ndege 11 Boeing,Airbus na Bomberdier
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dar es Salaam.
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.

Hayati John Pombe Magufuli ameandika hadithi mwaka 2017 pale tulipoona ujenzi mkubwa miradi mbalimbali ukianza.

Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba

Hayati Rais John Pombe Magufuli ameandika hadithi kwa ukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

Hayati Rais John Pombe Magufuli ameandika hadithi kwa Ujenzi wa barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

Hayati Rais John Pombe Magufuli ameandika hadithi ya miradi Mikubwa ya Maji,Dar,Morogoro,Dodoma,Kigoma,Tabota,na Shinyanga.

Hayati Rais John Pombe Magufuli ameandika hadithi ya uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga na hivi leo siku 25 baada ya kifo chake Rais Samia Suluhu Hassan anasaini kuanza kwa Ujenzi wa bomba hilo baada taratibu zote kukamilika.

Hayati Rais John Pombe Magufuli ameandika hadithi ya kila upitapo sasa hivi ni ujenzi unaendelea.

Dar es Salaam kila kona Barabara ya Tandale-Sinza- Mawasiliano barabara imejengwa,Mitaa ya Kinondoni hivi ina lami,Ubungo Interchange inajengwa
Madaraja yanajengwa

Upanuzi wa barabara kuu ya Ubungo hadi chalinze unafanywa kwa kiwango cha barabara nane.

Daraja Kilombero miaka yote wapigaji walikuwa wanakula hela za wananchi kuwavusha ila sasa limejengwa,

Hayati Rais John Pombe Magufuli ameandika hadithi ya ujenzi wa Flyovers zinajengwa pamoja na barabara za ziwani na baharini.

Hayati Rais John Pombe Magufuli ameandika hadithi kwa kuisimama vyema miradi ya umeme inajengwa na miradi mingi ni kwa hela za watanzania wenyewe,Miradi wa Umeme wa Gas wa Kinyerezi,na mradi wa Bwawa la Umeme la Rufiji (Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere)

Miaka yote maeneo ya Mbezi na kimara walikuwa hawapati maji japo yanapita njia hiyo hiyo lakini sasa maji yamefika mbezi, na bado wanaendelea kutandaza mabomba ili kupeleka maji.

Awali waliokuwa wanakula hela za wananchi ni wenye miradi ya kuuza maji kwa magari. Ila sasa wananchi wamekombolewa.

Hayati Rais John Pombe Magufuli ameandika hadithi ya kusimamia utendaji kazi na kufanya performance appraisals, Utendaji kazi umeimarika, sasa hivi kila mmoja anaona cheo akipewa ni kama kakalia kaa la moto.Yale mambo ya kupiga hela na kukaa ofisini kupiga usingizi yameisha watu ni kazi la sivyo unawajibishwa.

Madawa sasa yanapatikana hospitali, ile hali ya madawa ya hospitali yanapelekwa katika Pharmas binafsi imeisha.

Hospitali sasa za serikali ukienda mgonjwa anajaliwa sio kama ilivyokuwa awali.

Hayati Rais John Pombe Magufuli ameandika hadithi ya kuleta Uwajibikaji,Taasisi za serikali wafanyakazi wamekuwa wanawajibika,hakika nidhamu imeimarika.

Hayati Rais John Pombe Magufuli ameandika hadithi ya usimamizi madhubuti wa mapato ya Serikali, sasa taasisi za serikali zinajiendesha kibiashara na si kihasara kama ilivyokuwa awali, ilikuwa ni ulaji tuu wa hela, upigaji dili, taasisi zinakufa, hakuna gawio kwa serikali, ila sasa zinatoa gawio.

Hakika kila kitu ni usimamizi imara, ukicheka na kima utavuna mabua.

Hayati Rais John Pombe Magufuli ameandika hadithi ya kujenga nidhamu kazini,Awali watu walikuwa wanaulilia uongozi, hata wasio kuwa na elimu walikuwa wanagombea kupata uongozi, sasa uongozi umekuwa mgumu sababu kama wewe si muwajibikaji una ndoto za kupiga tuu, hupati nafasi, Uongozi umekuwa una hadhi kwa sasa.

-Tujikumbushe hadithi za Marais wengine wa Tanzania.

Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliandika hadithi kwa kuifanyia kazi taifa la Tanzania kwa miaka 23 na hadithi yake ipo mioyoni mwa Watanzania hata sasa.

Mzee Ally Hassan Mwinyi alihudumu miaka 10 ambapo alifanikiwa kupata stimula kwa ajili ya kufufua uchumi ulioharibiwa na Vita vya Uganda na Taifa likaanza kusimama tena baada ya athari ya vita vya Uganda.

Hayati Benjamin William Mkapa aliandika hadithi kwa kuhudumu miaka 10 alifanikiwa kuondoa gharama zisizobebeka za mashirika yaliyoleta hasara kwa kushindwa kuleta Gawio kwa Serikali tuliona taasisi za Serikali zikijengwa,na hadithi yake ipo mioyoni mwa Watanzania hata sasa.

Mzee Jakaya Kikwete ameandika hadithi ya kuhudumu kwa miaka 10,alifanikiwa kuanza kulipa Watumishi wa Umma baada ya kutaifishwa kwa mashirika ya Umma yaliyoitia hasara Serikali katika awamu ya tatu,Awamu ya nne ikaanza kusimama kwa miguu yake,hadithi yake ipo hata sasa.

Na sasa tunae Rais Samia Suluhu Hassan nae anaandika hadithi yake itakayoishi mioyoni mwa Watanzania.

JPM kaingia madarakani kakuta kuanzia 1995-2015 yaani miaka 20 ya watangulizi wake ni vijiji 2018 tu ndo vimewekewa umeme(REA mradi wa umeme vijijini) tena kwa gharama kubwa kuanzia 450,000/ mpaka 377,000/ lakini mwamba JPM alipoingia yeye na Mama Samia 2015 mpaka alipofariki 2021 yaani kwa miaka 5 tu ameweza kusambaza umeme kwenye vijiji 9750 tena kwa gharama ndogo ya 27,000/ tu...
Nimalizie kwa nukuu ya Mzee wetu na Rais wa Awamu ya pili,Ally Hassan Mwinyi kuwa "maisha ni hadithi" kila mtu anapaswa kuandika hadithi yake itayokaa mioyoni mwa Watanzania.
 
Back
Top Bottom