Hayati Magufuli ni shujaa anayepigana na walio hai

Hayati Magufuli ni shujaa anayepigana na walio hai

Nimekuwa kimya kwa siku mbili tatu ili kujipa muda kuifuatilia na kutafakari FILAMU inayochezwa na CAG akishirikiana na wanamapinduzi wanaopambana usiku na mchana kuifuta LEGACY ya MWAMBA HUYU KUTOKA CHATO.
Nilichokibaini kwenye report ile ya ndugu kichele ni kwamba ,inajaribu kutengeneza taswira mbaya mno kwa JPM kuwa.

1.Katika uongozi wa JPM serikali ilianzisha miradi isiyo na tija kwasababu inaipa hasara kwa mfano SGR , STEND ZA MABASI NA STIGLER,S GORGE NA ATCL.

SGR
Yaani unafurahia ujenzi wa bandari ya Bagamoyo
Itakayokufanya tuwe watazamaji lakini wanufaika ni wachina zaidi ya miaka 50.Unaambiwa ikijengwa bandari ya bagamoyo itakuwa kubwa kuriko zote Afrika mashariki na kati ,Lakini itafanya bandari ya tanga ,dar na mtwara kufungwa .Na zikifungwa hizi pato la bandar ya Dar tunakosa, tunaanza kutegemea fashila za wachina kutukadiria watugawie ngap ? Just imagine.

Yaani unafurahi kujengwa nyumbani kwako nzuri harafu ,ww unakuomba omba kwwnye ardhi yako ,ilihari ungejenga ya kwako ukawa huru.SGR inaunganisha Dar to mwanza, Rwanda ,burundi na kongo kuiondoa au kuisitisha ni kutuingiza kwenye mgogoro mkubwa wa kiusafirshaji.

Lakini pia SGR inaenda kutuingiza kwwnye maisha ya kisasa ,masaa matatu Dar to dodoma, Kenya wanayo mombasa to Nairobi na wanampango wa kuetend mradi sisi tunajadili kusitisha ,ni ajahu sana.

STEND ZA MABASI
Kiuhalisia wkt wa JPM ndo tumeshuhudia stend za kisasa kama uwanja wa ndege ,mathalani stend ya ubungo ilikuwa imezeeka sana haijaendana na jiji lenyewe ,angarau hii stendi ya mbezi.Madai ya kwamba itasababisha foleni yananiwazisha sana.Kwahy tuihamishe? Au tuishie kusema hivo tuchafue baadae tuitumie vivo hivo??

STIGLERs Gorge
Mradi huu ni mkubwa wa pili Afrika unatarajia kuzalisha umeme mara mbili ya uliyopo,na kumaliza kabisa changamoto ya umeme, hizi ni harakati za mtu mwenye nia njema na watu wake.Kuusitisha huu mradi ni kujirudisha nyuma mno.Changamoto za kiutafiti jpm aliZITOLEA MAJIBU.

ATCL
nashangaa sana watu wameanza kusahau mapema hivi ,shirika letu lilikuwa limekufa ,kuanza upya ni juhudi za jpm, kuingia sokoni si suala la siko moja kuanza kutengeneza faida.Wafanyabiashara wanafahamu huwez anzisha biashara leo kubwa kesho ukatengeneza faida ,Its imposible.Hivo atcl ndio ilikuwa inasaka wateja na ruti , bado kabisa lilikuwa shirika changa.

2.JPM hajafanya lolote la maana zaidi ya kupiga hela (ufisadi) ,
Haya ni maajabu ya mwaka ,yaani miradi yote hii ndani ya muda mfupi hajafanya lolote zaid ya kuiba? Jpm aliyekataa kwenda ulaya ili peaa hizo Itumike kwenye maendeleo ya wananchi unasema mbaya?

3.JPM alitumia kisingizio cha kuwaita watanzania wanyonge na kudai nchi imeliwa kumbe yeye ndiye mpigaji mkubwa.
Mambo mengine tunaambiwa yakuambiwa changanya na zako ,kma alikuwa mpigaji kiwango hicho hela za miradi yote hii ilitoka wapi?
Miradi ya maji, mahospitali, madawa ,umeme,elimu bure , sgr, stiglers ,madaraja ,viwanja vya ndege , meli ,ikuku dodoma,,vivuko nk.

Hata kama alikopa lakini kwa wingi na ukubwa mirad hii asingetoboa , hebu angalia JK hakutoboa miradi mingi ilikuwa imesimama amekuja kuihusha jpm.

Haingii akilini.

Baada ya kusoma na kufuatilia wachambuzi na maoni(comments) facebook kama vile :malisa ,kigogo, Magoiga, Ole mushi, veronica na Dr wiliamu nimebaini mambo yafuatayo:

1. Kundi la watu linashangilia report hii kwamba iko sahihi hasa kwasababu mzee hakuruhusu kukosolewa.Kundi hili ni lile la wale wanaotoka vyama vya upinzani.Hapa wapinzani wanachekelea tu na kujaribu kuonesha wako ipande wa SSH , lakini kiuhalisia wanamtumia kujiimarisha.
Maana ipo siku wataitumia kwa watu kuwa "ccm si chama cha kuaminika ,kimeoza JK alioza na yule mliyeamini yuko smart naye kumbe alioza" .kwahiyo ni Credit kubwa kwa UPINZANI.

2. Kundi la watu wanaokataa kata kata kuwa report hii imepikwa na JK na mafisadi kumchafua mzee kwa kuwa alimharibia biashara zake haramu.Hili limejaa wanaccm na wananchi wa kawaida.Hapa kumezuka timu "MaTAGA na MARTHA" .Mataga wanamwona mama ni msariti mkubwa ,na ya kwamba hataweza kumfikia jpm katika kuiletea maendeleo Tanzania

3.Kundi la watu ambao liko katikati linaamini report ni ya kweli lakini linaamini kuwa mzee hahusiki na huu ufisadi .Hawa wanaimani na SAMIA SULUHU kuwa ataendeleza aliyoachiwa na JPM.Hili nalo ni la wanaCCM ambao wao wanajipa moyo kuwa wampe muda mama huenda akafanya vizuri zaidi.

4. Kundi la watu ambao wanaona hamna umhimu wa kuendelea na CCM kwa kile alichokifanya mama, yaani hawa wanaona yale aliyofanya jpm ni makubwa zaidi kuriko hata CCM ,hivo kuyabeza ni kuwakosea pakubwa.

TWENDE SAWA.

BAADA YA KUYAONA HAYO MASWALI MENGI YAKANIJIA.
-Kwanini nguvu nyingi zimekezwa katika kumlaumu au kumkashifu jpm ,ili hari hata wakati wake ufisadi ulikuwepo ,ulibainika na kurekebishwa?

Yaani hii inataka kutengenezwa sura kwamba report za nyuma zilikuta serikali iko clean kwa 100%, ilihari nakumbuka hata za nyuma zilionyesha ubadhilifu polisi , TAKUKURU, CCM NA KWENYE MIRADI MBALIMBALI.

-Huyu kichele aliyesema hakuna tatizo kwenye atcl ndiye anatuambia kuwa kuna hasara Ya 150b atcl.Kama ni mtu mkweli angetuambia mwka jana hio hasara kuriko kusubiri rais aliyemteua hayupo ndipo aseme.Huyu ni tofauti na Prof Assa aliyesema bila kumng'unya maneno bunge la sasa ni dhaifu.Kama aliogopa kusema ukweli kqa hofu ya kupoteza kibarua hata leo anaweza kusema uongo ili kulinda kibarua

-kauli nyingi tata alizozitoa mama zinamaanisha nini? Kwa mfano suala la chanjo tusiwe kama kisiwa , madini yanatoloshwa kama awali , wafanya biashara wamekimbia nk
KUHUSU CHANJO

Kulingana na kauli ya mama kwamba TZ kutokubali chanjo ni kujitenga na dunia, kauli hii inatupa picha kwamba maamzi ya jpm hakuwa anayaunga mkono ya kukataa chanjo.

Kwa mkitadha huo mama anaonyesha kwamba haoni kuwa aliyoyakataa mtangulizi wake ndiyo yamekuja kutokea.Nchi nyingi za ulaya zimekataa chanjo zikiwemo uingereza,uholanzi na dernmak.Kama nchi hizi kubwa zimesitisha chanjo hii yeye anapata wapi ujasiri wa kuona kuwa Tz tumejitenga?
KUHUSU MADINi KUTOLoSHWA.

Kauli hii nayo ni tata ,utata unaanzia kwenye maneno "madini yanatoloshwa kama mwanzo" hii kauli inatuaminisha kuwa ukuta ule merelani hauna maana yotote.Lakini report zinamkatalia mama ,kabla ya ukuta kujengwa kenya na SA zilikuwa vinara kuuza tanzanite kuipita nchi yetu lakini leo hii sisi ndio vinara wa kuuza madini haya.

KUHUSU wafanyabiashara KUKiMBIA NCHI.

Hapa napo panautata mtupu, nikiangalia wafanyabiashara waliokimbia hawafiki hata wanne.
Maana bado:Mo ,bakheresa, kitana, kishimba nk wapo ambaye amekimbia ni Manji na MBOWE
Swali linakuja kwanini manji akimbie? Mbona wenzake hawakukimbia?
Kwahiyo kauli hii imejaa ukakasi mtupu

-Kama JPm alikuwa mbaya kiasi hixho na yeye mama akawa anamsapoti basi ni ishara kwamba hatoshi kuwa rais.Kule uingereza waziri mkuu aliamua kujiuzulu kwasababu ya kushikilia msimamo wake kuwa hawezi kuiruhusu uingereza ijitenge na ulaya.
Mama angekuwa mcha Mungu ,mtu wa swala tano tunategemea angekuwa amejiudhuru au hata kukataa ugombea mwenza, lakini miaka 5 imeisha ikaja mingine bado akakubali kumsaidia JPm basi ni dhahiri haya yanayotokea si yake bali ANAONGOZWA.

-hivi kweli stend ya mbezi itaongeza foleni ?? Yaani kuna mambo mengine mpaka yanachekesha , yaani wivu si wivu , ushwetani si ushwetani .Na kwa mkutadha huu ,tutegemee miradi ya maji ,umeme,viwanja vya ndege ,madaraja vitakuwa aidha hasara au havina tija.

HITIMISHO
Kama kweli dhamira yao ni KUIFUTA LEGACY YA JPM BASI WAFANYE YAFUATAYO.

1.UZA ndege zote , meli zote ,vivuko vyote
2.bomoa bandari ya dar , tanga ,na mtwara zilizoboreshwa.
3.Nyanganya migodi wazawa ,gawa kwa mabeberu ,futa kampuni la twiga.
4.Binafisisha milima, mapori na maziwa
5.Simamisha ujenzi wa stiglers gorge
6.Bomoa SGR , uza vyuma spea.
6.Vunja ,bomoa daraja la busisi, tanzanite
7.Rudisha ada na michango shuleni.
8.Vunja masoko ya madini nchini na ruhusu makinikia kwenda nje ya nje
9.Ruhusu uhuru wa mshoga na ndoa za jinsia moja.
10.Chalaza bakora machinga, mwaga wali wa mama lishe
11.Sitisha ujenzi wa masoko ya kisasa.
12.Vunja ukuta wa merelani
13.tengeneza sheria za madini
14.amuru lockdown na chanjo.

MAMA UNANAFASI MBILI TU FUATILIA UZI HUU KWA MAKINIView attachment 1749507View attachment 1749508
Wizi hauna cha afadhali
 
Jna lenyewe unalojiita ngaliwe. Ngaliwe kwa kabila langu maana yake ni tahira.

Sa tutegemee toka kwako kama si pumba tu.
 
Sawa
Screenshot_20210411-180847.jpg
Screenshot_20210411-180902.jpg
Screenshot_20210411-180913.jpg
Screenshot_20210411-180743.jpg
 
Na Mwananchi Mwenye Hasira Kali.

WENGI tunaendelea kukuombea pumziko la amani. Hatuwezi kukuhukumu kwa lolote hasa sasa wakati huu ambapo uko mbele ya Mhukumu mwenye haki. Tunachoweza kufanya ni kumuomba Mwenyezi akupatie taji la haki ambalo amewawekea watumishi wake, waliomtumainia na kumwamini.

Tunakuombea siyo kwa sababu tunataka kujifurahisha au kujifariji bure, sisi wengine tulikuamini kwa dhati, tunaendelea kuamini ulivipiga vita vilivyo vizuri, na hata ulipomaliza mwendo, kazi njema ya kutukuka umeiacha nyuma yako, haya uliyoyafanya yataendelea kusimulia uzalendo wako usiotiliwa shaka kwa Tanzania, ushujaa wako wa kusimama kidete na bila kuyumbishwa na mataifa ya nje, ulilinda na kutetea rasilimali zetu kwa dhati, ukatupa tafsiri sitahaki ya taifa huru.

Ukautafsiri utajiri wetu wa rasilimali kwa vitendo, Tanzanite ikaanza kuwa mali ya Tanzania, masoko ya dhahabu yako kila mkoa wenye madini, Taifa sasa linajivunia msimamo wako, Afrika itaendelea kukumbuka kama kiongozi uliyeonyesha njia kwa vitendo namna ya kulinda na kuzifanya rasimali za Afrika ziwanufaishe waafrika wenyewe, wengine wamekuwa wajuzi wa maneno zaidi kuliko vitendo.

Miaka yako mitano tu ya Urais wa Tanzania umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutuonyesha wazi kwamba kale tulikokuwa tunaambiwa ni kasungura kadogo (keki ya taifa) kumbe siyo tu ni sungura bali ni nyati aliyenona. Ndiyo maana miaka yako mitano umeweza kuihamishia serikali yote Dodoma, umepeleka umeme vijijini karibu vyote, umejenga hospitali za rufaa, hospitali za wilaya na mikoa, vituo vya afya na zahanati kuliko wakati mwingine wowote na mambo mengi tu ambayo awali yalikuwa ya kusadikika.

Ndani ya chama umekijengea uwezo wa kujitegemea, umeweza kukikomboa kuondokana na utegemezi wa fedha za matajiri ambao walikiweka mfukoni, kimejikwamua kiuchumi, mali zake ambazo zilikuwa zinafujwa hovyo hovyo, umeziratibu vyema na sasa chama kinajua kinamiliki nini na wapi na kinapata mapato yanayokiwezesha kujitegemea ndiyo maana, kimeweza kuendesha shughuli za uchaguzi ndani ya chama kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2020, ukiwa Mwenyekiti wake bila kutembeza bakuli kwa wafadhili.

Siandiki haya ili kukutetea kwa wanaokubeza leo, mimi ni nani hata nijipe kazi iliyotukuka hivyo leo, sistahili kuwa mtetezi wako, mtetezi wako wa haki ni Mwenyezi Mungu aliye hai, ambaye ukingali tumboni mwa mama yako alikutakasa na kukufanya kuwa mtumishi wake kwa watu wa Tanzania uwatumikie kwa utumishi uliotukuka, lakini pia kazi zako njema zinakutetea na historia itakuwa shuhuda wa haya toka kizazi hiki hata cha tano na saba cha Mama Tanzania. Ninaandika kuililia Tanzania na kukisikitikia Chama Cha Mapinduzi.

Naililia Tanzania kwa namna ile ile Bwana Yesu alivyoulilia Mji wa Yerusalem, “Laiti ungalijua hata wewe katika siku hii yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako. Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke, watakuzingira na kukuhusuru pande zote; watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutabua majira ya kujiriwa kwako.”

Hayati Rais Magufuli hakuwa mtakatifu na wala hakujinasibu hivyo, alikuwa binadamu kama sisi na yapo mapungufu yake kama binadamu na pengine kama kiongozi. Lakini mzaha, kejeli na dharau anazofanyiwa leo na watanzania hawa hawa, wengine viongozi aliowaamini ni hakika zitarigharimu taifa hili.

Uamuzi wake wa kutetea rasilimali za watanzania, kulinda maslahi ya taifa lake, kwa ajili ya watanzania wenyewe, leo umegeuzwa dhihaka kwake, majitoleo yake ya kuijenga Tanzania mpya yanafanywa kuwa dharau iliyotukuka, kila anayejua kuandika na kutukana au kukejeli, anamwandika kumzodoa na kumfanya dhalili kadiri anavyoweza, hakika hii ndiyo sura ya Tanzania ambayo sikuwahi kuifikiria itafika hapa.

Tuliomsoma Walter Rodney katika How Europe Undeveloped Africa, walau ilisaidia kututambulisha kwamba Afrika limefanywa shamba la mataifa ya ulaya, wanakuja kuvuna wanavyoweza wanakwenda, kinachotokea ni kubadilisha tu mbinu za uvunaji lakini malengo na shamba ni vile vile. Ilianza biashara ya utumwa, ukaja ukoloni, ukaja ukoloni mambo leo ukiambatana na ubeberu, ukaitikiwa vyema na utandawazi. Nawapongeza kwa umakini huo, wenzetu wanajua wanachokitafuta kwetu, sisi hatujielewi ni akina nani tunataka nini kutoka kwa nani.

Ndiyo maana wakitokea watu aina ya kina Magufuli, wanabezwa, wanatwezwa, wanavikwa kila aina ya sifa chafu na mbaya ili tu ipatikane sababu ya kuwapuuza na kushusha hadhi ya mbele ya jamii. Kwao kuendelea kumsifia mtu aina ya Magufuli ni sumu kwa maslahi ya mataifa yao, kwa sababu atakuwa mfano na anaweza kuzalisha akina Magufuli wengine wa kutosha, hawataki hiyo.

Ndiyo maana sasa wamefanikiwa kwa muda mfupi sana, hata kabla majembe na makoleo yaliyotumika kumzika hayajapukutisha udongo wote wa kaburi, tayari kishaanza kuonekana hafai, hakuwa na maana na anageuzwa kichekesho. Sasa hivi kwa kuwa tu alikuwa anatumia sana maneno uzalendo na ubeberu, maneno haya yanatumika kama kielelezo cha bezo na kejeli, kutumia neno ubeberu sasa hivi unaonekana wa kizamani, huna nafasi katika Tanzania ya sasa, ukijiita mzalendo unaonekana kituko na kioja.

Natokwa na machozi kwa ajili ya Mama Tanzania, watu wako wanacheza ngoma wasiyoijua, wanitikia kibwagizo cha wimbo wa kigeni. Wayahaudi walipokuwa kando ya Mto Babeli, wakiwa utumwani waliowachukua mateka walitaka wawaimbie nyimbo za Sayuni, walikataa kata kata, wanawezaje kuimba wimbo wa Bwana katika nchi ya ugeni? Wakaapa bora ulimi ugandamane na kaa la kinywa kuliko kuikubali fedheha hiyo. Leo Watanzania tunaimbishwa wimbo wa kujitukanisha, kumkashfu Rais Magufuli katika nchi yetu wenyewe, aibu gani hii, Mungu atusamehe tu.

Spika wa Bunge Job Ndugai aliyekuwa akisisitiza kwamba Rais Magufuli “atake asitake tumauongezea muda”, ili aendelee kutawala kinyume na Katiba leo amekuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kabisa kabla hata suti aliyokwenda nayo Chato kuzika hajairudia kuivaa, kukejeli na kuonyesha miradi ya kimkakati iliyoanzishwa chini ya Rais Magufuli ni ya hovyo, haina manaa, kweli ubinadamu kazi.

Kwamba ndege hazihitajiki tena, huyu huyu aliyekuwa mstari wa mbele kusifia kwamba alikuwa Rais shujaa ametufuta aibu ya Taifa kutokuwa na ndege, kwamba Bandari ya Bagamoyo ina maana sana tena baada ya Rais kufariki, kweli?

Kwamba Rais alishauriwa vibaya, kisa? Mpendwa Spika wetu alipatiwa wasilisho kuhusu Bandari hiyo akiwa ziarani China, kwa nasibu tu, alikwenda kwa kazi nyingine ikatokea wakawapatiwa wasilisho hilo. Kama ilikuwa kazi nyingine na wasilisho hilo lilitolewa by the way, kiongozi wetu huyu wa mhimili anataka tumuelewe vipi kuhusu mradi huo. Anafikia hitimisho kwamba rais alishauriwa vibaya kuhusu mradi, Rais alielezwa kwa kina athari zake kwa taifa, halafu eye kukutana na bodi hiyo anataka tumuamini zaidi kuliko Rais aliyepata taarifa kamili na za kina?

Kama anajua ulikuwa na faida hizo na kama kiongozi wa mhimili muhimu kama Bunge, alishindwa nini kuteta na Rais hata faragha, ili kumweleza msimamo wake na uzuri wa mradi huo kwa maslahi ya taifa, kwanini asubiri mpaka Rais Magufuli afariki dunia? Huyu kweli ana dhamira njema na taifa hili?!

Kwa CCM, hapa sitalia, nawasikitikia tu, bila shaka mnakumbuka enzi za kuficha sare za chama chenu mnapokwenda kwenye mikutano yenu, mlikuwa hamuwezi kuthubutu kupita na sare za chama Kariakoo, leo mnaona fahari kukatiza na kijani na njano kila mahali tena kwa heshima, nadhani hayo yameletwa na pepo za kusi au kaskazi tu, hakuna mtu asijidai kwamba amekijengea chama heshima, tena Magufuli ndo kabisa asithubutu kujinasibu kwa hili, kwanza alikuwa mchanga kwenye chama.

Kama ndivyo na kama Magufuli alikuwa mbaya kiasi hiki tunachokishuhudia leo kwa baadhi ya viongozi wa serikali na CCM, kiasi kwamba makada wote sasa mnamuona hafai na hana maana tena, aliwachelewesha na mipango yake ya ‘kishamba’, ninao ushauri huu kwenu.

Ili chama kiwe salama, futeni legacy yote ya Magufuli ili chama kiwe cha kisasa, anzeni na kuandika upya ilani, muachane na ile ya kishamba ya kurasa 303, achaneni na elimu bure, msijenge tena hospitali na vituo vya afya, umeme vijijini umetosha, watimueni wamachinga barabarani, achaneni na yote aliyoanzisha Magufuli.

Badala yake, ruhusuni yote aliyoyazuia, waiteni wachina wajenge bandari Bagamoyo na sisi tuwe wa kisasa kama Sri Lanka (si mnajua kinachoendelea kwao baada ya kujengewa bandari kama hii na China), naona mnatamani tufuate njia yao, ni kama tumechoka kuwa huru, wapeni wamiliki kwa miaka na masharti wanayotaka.

Halafu muandae ilani ya yenye jina, Anti- Magufuli Manifesto, ili tutembee nayo katika uchaguzi wa 2025, kwa kuwa Magufuli aliwaudhi na kuwakera sana Watanzania, kwa kuwa serikali yake ilikuwa ya kidikteta, bila shaka ilani yetu itapokelewa vyema na wananchi na kutupa ushindi wa asilimia 90.

ASANTE JOHN
 
Watambeza Magu lakini watashindwa tu.

Alivyovisimamia vinaishi, na vitaendelea kuwasuta wanaombeza.

Na kwa sababu aliyoyasimamia yanaungwa mkono na watanzania wengi wapiga kura, bado wataibuka wanasiasa kuhubiri mambo aliyoyasimamia.
 
Hii ni aina mpya ya Falsafa iliyoanzishwa katika Karne ya 21 haswa mwaka 2021 kutokana na falsafa za aliyekuwa rais wa awamu ya tano wa Tanzania Dr. John Pombe Joseph Magufuli aliyeishi kati ya 1959-2021. Katika Falsafa ya Magufulism tutaangazia mitizamo ya mwanafalsafa huyu katika nyanja za Kiuchumi, Kisiasa, Kijamii, Kidini, Kiutamaduni, Kielimu na Kisayansi. Falsafa hii imeandikwa na kubuniwa na Josias Charles, mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma katika Elimu ya Saikolojia ya Watoto na mbobezi katika Historia kwa Ujumla.

MAGUFULIST
Hawa ni watu wote wanaoamini , wanaoishi na kuenenda katika falsafa ya Magufulism. Magufulist siku zote wanaamini kuwa maendeleo ya Taifa ama mtu binafsi yanatokana na kulinda raslimali tulizo nazo kwa nguvu zote na Kufanya kazi kwa uadilifu bila kutegemea misaada kutoka nje.

Hapa chini tutaichanganua falsafa ya MAGUFULISM katika nyanja mbalimbali ambapo tutaangalia Dr. John Pombe Magufuli alikuwa na mitizamo na falsafa gani kuhusu mambo mbalimbali:

MAGUFULI NA UCHUMI:( MAGUNOMICS)

Dr. John Pombe Joseph Magufuli aliamini uchumi imara hutengenezwa kwa kutumia raslimali zilizotuzunguka kwa uaminfu na uadilifu. Dr, Magufuli aliamini pia kuwa endapo kila mmoja akitimiza wajibu wake wa kufanya kazi kwa bidii na kulipa Kodi kwa uaminifu basi uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla ungeimalika sana. Dr. Magufuli alipinga uwekezaji wenye masharti ya Unyonyaji kutoka kwa mataifa ya Nje hususani katika Sekta ya Madini, Bandari nk.

MAGUFULI NA SIASA:(MAGUCRACY)

Katika upande wa Siasa Dr. Magufuli aliamini katika uwepo wa Vyama vya siasa vyenye mlengo wa kuleta ushindani wa hoja na sio vyama vinavyotumiwa na mataifa ya Kigeni kutaka kuvuruga amani na mshikamano wa Taifa. Dr Magufuli alividhibiti kwa nguvu kubwa vyama vilivyokuwa vikitumiwa na mataifa ya Kigeni kupenyeza agenda za mataifa ya kigeni. Katika Upande mwingine Dr. Magufuli aliamini kuwa Maendeleo hayana chama. Katika kuonyesha kuwa maendeleo hayana chama , Dr. Magufuli aliwateua viongozi wengi wa Vyama vya Upinzani katika nyadhifa tofauti tofauti katika Serikali yake.

MAGUFULI NA JAMII

Dr. John Pombe Magufuli aliamini katika ustawi wa jamii na kupinga aina zote za unyanyasaji toka kwa watu wenye madaraka na matajiri. Katika kipindi chake cha uongozi ndipo jina "WANYONGE" lilipata umaarufu. Wananchi walipoona Msafara wa Dr. Magufuli waliukimbilia na kuona mtetezi wao amefika, naye Dr. Magufuli aliwapa nafasi ya Kuwasikiliza.

*MAGUFULI NA DINI"

Dr. Magufuli aliamini kuwa tunamuamini Mungu mmoja hivyo alihimiza usawa, upendo na mshikamano kati ya watu wa madhehebu yote. Alichangisha fedha za Kujenga Misikiti katika makanisa mbalimbali, na pia pesa za kujenga Makanisa kutoka misikiti mbalimbali. Dr. John Pombe Magufuli aliamini kuwa hakuna jambo linaloshindikana mbele za Mungu. Hata katika kipindi ambacho Dunia ilikuwa ikihangaika na janga la Corona Dr Magufuli alichukua msimamo tofauti na mataifa mengine, aliwahimiza watanzania kumuomba Mungu maana yeye hashindwi na jambo lolote lile.

MAGUFULI NA MAHUSIANO YA KIMATAIFA

Dr John Pombe Magufuli aliamini katika ushirikiano usio na chembe za unyonyaji kati ya Taifa lake na mataifa ya Kigeni. Dr Magufuli allikuwa tayari kusitisha uhusiano na Taifa lolote ama taasisi yoyote yenye lengo la kufanya unyonyaji kwa Taifa lake. Kwa Lugha rahisi Dr Magufuli hakuwa muumini wa Kujipendekeza kwa Taifa tajiri ama Taasisi za Kimataifa kwani aliona kuwa watu wote ni sawa hivyo hakuna sababu ya kuwanyenyekea wanyonyaji kutoka katika mataifa ya Kigeni.

MAGUFULI NA RUSHWA/UFISADI

Dr. Magufuli alichukia Rushwa na Ufisadi kwa dhati ya moyo wake. Alikuwa tayari kuvunja urafiki na mtu yeyote aliyetetea ama kufanya vitendo vya rushwa. Katika Kipindi chake cha Uongozi neno "KUTUMBUA MAJIPU" lilimaanisha kuondoa viongozi wote wasio waadilifu na kuwachukulia hatua.

Hii ni sehemu ndogo kati ya Historia ndefu na ya kusisimua kuhusu Kiongozi na mwana falsafa huyu aliyeishi katika Karne ya 21.

IMG-20210410-WA0024.jpg
 
No body can challenge, him, "the late Magufuli".
 
Mleta mada ni vema ujue hakuna anayembeza magufuli. Watu wanaongea maoni na mawazo yao. Ni haki yao kikatiba hata kama wanachoongea kinamkosoa au kumuumbua magufuli.

In fact marehemu alikosea sana kuziba midomo wakosoaji wake na hata kutesa na kutweza utu wa wengineo.

Waache wenye mawazo waseme mawazo yao na wewe yakikuuma sema yako. Mradi tuheshimu sheria za nchi.

AU NASEMA UONGO NDUGU ZANGU?
 
Back
Top Bottom