Thomas Sankara wa Bukinabe ambaye leo hii mabaki yake yamezikwa upya kwa heshima ya kijeshi ni kiongozi bora kuwahi kupatikana barani Afrika. Alifanya makubwa kwa taifa lake. Alipigania maslahi ya wanyonge na kulinda rasilimalinza taifa lake.
Kwa Tanzania ni hayati Magufuli pekee aliyefanya kama Thomas Sankara. Alidhibiti upatikanaji wa mapato na kuhakikisha mali za umma zinatumika vyema. Kwa miaka mitano tu alionyesha makubwa. Hii ni sababu alifanana kwa kila kitu na Thomas Sankara.
Naomba nichukue aya ya mwisho!
Alidhibiti au alihakikisha:?
Jibu Ni kwamba alihakikisha uoatikanaji wa mapato kwa njia yoyote haramu na halali ili awafurahishe wasioweza kufikiri na kujua athari zake
-Plea Bargaining
-Ujambazi wa kidola (kuna watu wengi walifungiwa account zao na hela kuchukuliwa licha ya kutoa maelezo namna gani walizipata fedha hizo)
-Aliunda Task force au kikosi kazi kilichotumika kupora kweenye maduka pamoja na bureau de-change (Bwana Sabaya alikiri mahakamani kwaba ujambazi wakes alifanya kwa maelekezo ya mamlaka iliyomteua) hali iliyofanya HAI ikapanda chati katika ukusanyaji mapato mpaka nafasi ya sita Jambo ambalo lilifanya Mbowe aonekane fala utadhani Mbowe alikua na dhamana ya kukusanya Kodi au alikua mkuu wa wilaya!
-Alikopa fedha kwa Siri kwenye mabenk ya biashara Tena ya ribs kubwa bila kulijulisha bunge mpaka IMF na world Bank wakamuandikia barua atoe maelezo na pamoja hatari kwenye uchumi kutokana na madeni anayotengeneza kwa siri! Huku akitudanganya Ni fedha za ndani.
-Alitengeneza na kuuza vitambulisho vya machinga akakusanya hela ambazo mpaka Leo hii Mimi na wewe hatujui ni Tsh Ngapi na zilitumika wapi na kwa maana hiyo zilikua zake!
-Report ya CAG ikaonesha zimekusanywa 1.5 trillion lakini hazijulikani au hazionekani (pole pole akawa mwalimu wetu) zilipotumika, na CAG akafukuzwa kazi Mara moja baada ya kuliweka Hilo wazi! Mahakama imethibitisha Hilo kupitia kesi aliyofungua ZITO
-MO DEWJ aliachiwa kwa ransom ilivyotolewa ambayo Mimi na wewe hatuzijui ! ...ndio Mana case closed completely!
Baba akitumia vibaya fedha akawaletea mkate na nyama haihalalishi uovu wake!