Hayati Magufuli (R.I.P), Hivi Aliwezaje kufanya yote haya?

Hayati Magufuli (R.I.P), Hivi Aliwezaje kufanya yote haya?

🤣🤣🤣🤣.
Embu fuatilia historia ya JK. Usimdharau yule mzee.

Halafu Hawezi kukaaa akala pension, nchi inamtegemea sana sasa hivi si unajua ndiye mstaafu hai mwenye nguvu aliyepo.
Alikosa nguvu akiwa rais wanna CCM wakamwimbia tunaimani na Lowassa,leo nyuma ya pazia ataweza?
Tatizo mtu akiwa Hana uwezo yeye huwa hajui.
 
Legacy ya Mzee ipo chapter ya ngapi? - tunaisubiri.
 
Jpm namkubali ktk mambo mengi tu na simkubali ktk machache sana.tatizo la nchi hii lipo ktk unafki wa kidini.ktk maraisi wote waliowahi kuongoza nchi hii hakuna aliegusa kila idara kuifanyia mambo mazuri kama jk. Ingawa ni ukweli ktk uongozi wake wizi mwingi sana na ukwepaji kodi umefanyika.

Mpaka anaondoka deni la taifa lilikua 50+tl na halizidi 55tl sikumbuki wakati anaingia lilikua ngapi,jpm miaka 5 tu! Deni la taifa 70+tl na tunaaminishwa hakukuwa na wizi wala mikopo

Mwanza basi zilikuwa zinapitia kenya jk akatatua tatizo la miundo mbinu kigoma huwendi bila treni jk akatatua kusini ndio usiseme hadi tunduru,katavi,babati,umeme vijijini maboresho muhimbili shule za kata, udom,chuo cha Mandela,majengo ya polisi

Baboresho ya barabara hadi zile zikazokua na lami tangu zamani kama kipande cha unapoanzia mkoa wa iringa hadi kuelekea njombe na mbeya.jk ndeye raisi pekee alienunua meli kubwa za vita. Mambo mengi kayafanya jk alafu kuna wajingawajinga wanamponda hayupo raisi hata 1 tangu tupate uhuru aliefanya hata nusu ya jk.

Ingawa kwa mbaaaali jpm kwamwendo wake ule angemaliza miaka yake 10 angemsogelea lakini sio kumfikia
huyu baba baada ya kuiba uchaguzi kwa 100% sikuwa na hamu naye kabisa, bora uibe pesa haiumi sana kuliko kuiba haki.
 
Ndio maana hakumaliza awamu zote ...

Huwezi ishi kwenye hii dunia kipumbavu namna hio ...

Lazima uondolewe tu ,wewe ni Nani hasa kwenye hii dunia ya damu na jasho[emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4]
Kwa hiyo mlimuua? Siku zote damu ya binadamu huwa haiendi bure na nyie mtakufa kifo kibaya zaidi.
 
Matumizi mabaya ya Madaraka kunyamazisha na kudhalilisha watu

Ila Mungu Mkali sana
Alhamdullilah
 
Kweli, alipenda "ON THE SPOT", On the spot ilonekana alipozuia uchaguzi wa serikali za mitaa wasichaguliwe wengine ila Chama chake tu. On the spot nyingine ikaonekana kwenye uchaguzi wa October 2020 pale mifuko ya kura bandia iliyosimamiwa na Polisi na TISS ilipoingizwa na KUFANYA bunge liwe la Chama kimoja. On the spot nyingi tu alizisimamia. Kweli naungana na wewe JPM alipenda ON THE SPOT!
JPM alikuwa pale kwa masilahi mapana ya Watanzania wengi, siyo masilahi ya wanasiasa wachache.

Hayo yote uliyoyataja ni masilahi ya wanasiasa wachache whom hawakumweka madarakani wala hakuwa pale kwa manufaa yao.

You are just proving his being man of the people.
 
Ndio maana hakumaliza awamu zote ...

Huwezi ishi kwenye hii dunia kipumbavu namna hio ...

Lazima uondolewe tu ,wewe ni Nani hasa kwenye hii dunia ya damu na jasho[emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4]
wala usiwaze sana mkuu maana we mwenyewe lazima uondolewe wala sio ombi
 
Kilaza ni aliyeibiwa 1.5T na asijue mpaka sasa iliko.
Ila jamaa alikuwa laana kwa Tanzania, kuongoza familia tu alishindwa eti akataka kuwa mpaka kiongozi wa malaika
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ila jamaa alikuwa laana kwa Tanzania, kuongoza familia tu alishindwa eti akataka kuwa mpaka kiongozi wa malaika
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Jamaa alikuwa kiongozi bora wa wakati wetu! Apumzike kwa amani mbinguni.
 
Alikosa nguvu akiwa rais wanna CCM wakamwimbia tunaimani na Lowassa,leo nyuma ya pazia ataweza?
Tatizo mtu akiwa Hana uwezo yeye huwa hajui.
Hakukosa nguvu na alijua hilo suala aliaddress vipi na amtumie nani sababu anaowaongoza hawakumuogopa wakawa wanafunguka wanalotaka kwa kumuimbia.

Kutokuimba tuna imani na Lowasa haimaanishi kuwa imani haipo. Unadhani wangenyamaza kwa kumuhofia ndo ingemaanisha hawana imani na Lowasa?

Mtu anayeogopwa siku zote huangushwa kirahisi sana kwa sababu huzungukwa na wanafiki.
 
Nimeangalia kinachoendelea sasa katika nchi na kujikuta nalazimika kumuuliza yafuatayo kuhusu mpendwa wetu Magufuli (r.i.p);

1. Hivi aliwezaje kuwafanya watu wamuogope vile? hofu ile ni kutumbuliwa tu au?!!! namkumbuka mkuu mmoja wa mkoa (nikifanikiwa nitaitupia clip) alivyokuwa anatetemeka siku ile aliyokuwa anasaini kitabu cha wageni...aisee lile tetemo si la kawaida! raisi alikuwa anasaini kitabu huku mkuu wa mkoa akiwa anajiandaa kukaa chini, ghafla raisi akainua macho kupeleka upande ule aliokuwepo mkuu wa mkoa (nafikiri ilikuwa katika kuangalia tu kawaida) aisee mkuu huyo wa mkoa aliinuka ghafla huku anaendelea kutetemeka vibaya sana. akiiona ile clip huko aliko atajisikia vibaya sana.

2. Mabarabara yote aliyoyajenga Kikwete (ndiye aliyejenga zaidi ya wote) sifa zinaenda kwa Magufuli. Kikwete hatajwi na ukimtaja kuna waaokasirika, aliwezaje kufanya hivi?!!

3. Kuna baadhi ya vitu alivianzisha mtangulizi wake (Kikwete) katika kuvijenga kama vile flyovers, lakini imeaminishwa kuwa ni JPM tu aliyefanya hivyo. wakati huo huo aliyemfuatia jpm (mama Samia) akiendeleza aliloliacha JPM kama vile kuongeza kile kipande cha SGR kule Mwanza (ambacho hakikuwepo), hatajwi kabisa mama; anatajwa JPM tu na ukimtaja mama basi kuna watakaokushambulia. aliwezaje kufanya hivi?!!!!!

4. Aliagiza machinga waachwe na wajipangie tu mabarabarani. alisema hayo huku akiwa amezungukwa na wasaidizi kibao wakiwemo wataalamu wa mipango miji, wataalamu wa masuala ya population growth, mazingira n.k lakini wote walishindwa kusema chochote juu ya athari kubwa inayoweza kuzaliwa baadae (kwa watakaomfuata). aliwezaje haswa kufanya hivi?!!!!

5. Leo hii Kikwete na ukoo wake hawaishwi kutajwa tajwa kuwa ni wezi huku yeye akitajwa kuwa ni msafi, aliwezaje mwendazake kuwaaminisha watu hivi?!!!!

6. Wakati wake, ukifanyika mradi wowote wa maendeleo ilikuwa inasemwa kwa sauti kubwa, RAISI AMEFANYA HIVI AU VILE. ajabu ni kuwa leo hii mama Samia akifanya jambo na ikitolewa taarifa kuwa 'Raisi kafanya hivi', aisee utapata mashambulizi kutoka kwa watu 'KWANI FEDHA ZAKE AU KODI NA TOZO ZETU?!!'. JPM aliwezaje?!!! Kawaida hii kweli?!!

7. Wakati wa utawala wake, inasemekana wateule wake walikuwa wakristo na watu wa kwao. ajabu ni kuwa watu walikuwa kimya na kusifia tu. kama kuna aliyejaribu kulisema ilo alikutana na hii kauli, 'RAISI HAANGALII DINI BALI UCHAPA KAZI'. cha kushangaza kipindi cha Kikwete, akichagua waislamu wawili tu basi kelele zake si za nchi hii. mama nae, ateue waislamu wawili tu katika teuzi 5 alizofanya basi haraka utasikia kauli hizi 'ZAMU YAO WAVAA VIPEDO!', 'ANATEUA WAZANZIBAR WENZIE' n.k. huyu JPM aliwezaje hili?!!!

8. Kwake (Chato) ilienda kila aina ya miradi; uwanja wa ndege wa kimataifa, nasikia uwanja wa mpira pia, mbuga, hospitali ya kanda, n.k huku kwa waziri mkuu barabara ya km 86 tu ipo vumbini hadi leo hii na mazao yote yategemewayo na wananchi wa kule (mbaazi, korosho na ufuta) yakifilia mbali huko. mawaziri mpaka manaibu mawaziri na wakuu mbalimbali wa taasisi walikuwa wanapishana na kushindana kubuni miradi ya kupeleka kule. aliwezaje huyu mtu kufanya hivi huku watu wakishangilia kinoma?!!!!!!!!!!

9. Kununua ndege 11 kwa keshi. aliwezaji ilhali nasikia hata mashirika makubwa yananunua kwa awamu?!!!

Yapo meeengi sana lakini hayo yatoshe kuwakilisha.

Najiuliza sana kama hii kawaida au kuna sehemu inapatikana 'busta' ya kukusaidia kuwa hivi. Kama ipo basi naamini kina mkuu Mshana, kama itampendeza, anaweza kuchangia ili tukujue na ikiwezekana tufanye maamuzi ya kwenda kwa ajili ya kuzimudu familia zetu tu (kwani huko siasani hatupo na hakuna dalili ya kuwepo).
Propaganda na kuwatisha watu,hii nchi wakati mwingine ina mifumo ya hovyo yaani kinyago yoyote anaweza fanya lolote analojiskia,too bad
 
Back
Top Bottom