Kikwete umejitosa JF kujitetea?
Nchi ilikushinda mjomba,kaa tu ule pensheni.
Hata ukipewa urais Tena mziki wa sukumagang huuwezi,Labda ule wa fitina unaweza na kuuza sura Ulaya.
Yaani Kikwete uwa anaangaika speech zake toka Magufuli yupo ni kudai hiki nilianzisha mimi, Tatizo Kikwete aliona yeye ndo anapendeka, akapewa nchi ikamshinda kwa kuendekeza Urafiki na kujuana. Alio waweka wakamuangusha.
Kikwete alimchukia Nyerere hakumpenda toka Nyerere alipomkataa na kumweka Mkapa. Aliposhika madaraka akawafitini Nyerere Foundation, akina mzee Butiku. Ili aonekane yeye ni yeye. Hata hivyo hawa wazee wameuwa Nyerere foundation hatuoni wanafanya nini. Nao waachie madaraka kwa wengine wanataka kufa na Nyerere foundation?
Ndo maana kuna vita kubwa na Magufuli, mtu wa watu katangulia, lkn anavyotukanwa, utadhani wao hawatokufa. Utadhani wataishi milele. Kikwete bado hajaridhika.
Mie nitamke kueni makini Mungu ndiye ajuae kwa nini Magufuli ilikuwa aondoke mapema. Msidhani ndo upande wa Kikwete mmeshinda! Chochote chaweza tokea.
Magufuli anatajwa wizi, lakini hawaweki wazi kaiba nini? Ni uongozi upi ulijaa kashifa za wizi? Wanasema mauaji, hivi wakati wa Kikwete wangapi walitekwa na kuteswa, acha hii ya Mo katekwa ati anarudi bila kovu lolote.
Dr. Ulimboka, Mwandishi wa habari alietobolewa macho, Mawazo wa Chadema, Dr. Mvungi wa NCCR, Mwandishi wa habari huko Iringa alie uwawa kwa bomu, Mkurungezi wa usalam wa Taifa msitaafu Kombe alie uwawa huko Arusha, mbona haya hayatajwi anasingiziwa magufuli. Mauaji Zanzibar katika chaguzi za 2000, 2005, 2010. Ni wakati gani Zanzibar ilichafuka zaidi? Tuache propaganda na ushabiki usio na mantiki.
Kwanza mimi sioni kuna haja gani kulinganisha viongozi na wote wanatoka chama kimoja. Tunachotaka ni viongozi wenyekuleta maendeleo. Atoke upinzani sawa. tuache ujinga wa kulinganisha Magufuli na Kikwete. Kikwete sasa hayupo muda wake ulipita. Magufuli alishatangulia mbele za haki, hata hajui kinachoendelea. Japo ni kiongozi alie fahamika duniani kwa ungozi thabiti na kuwa na misimamo.
Wana Kikwete kubalini kuwa kila zama na kitabu chake Kikwete alimaliza mwacheni apumzike, Magafuli na mwacheni apumzike huko aliko.
Tumwangalie mama yetu SSH nae atatufikisha wapi.