Hayati Mwinyi alivyomgomea Mwalimu Nyerere kuondoa jina lake ili Salim awe Rais 1985, ikawa ukombozi kwa Watanzania

Mtu aliyekuwa anatoa maamuzi ya Mwisho kuhus Zanzibar alikuwa Thabvit Kombo, na Nyerere alikuwa haamui lolote kuhusu watu wa Zanzibar bila kumwuliza Thabit Kombo. Iwapo Thabit Kombo alisema iwe ni Mwinyi kuliko Salim basi itakuwa hivyo, na iwapo Mzee Kombo angesema iwa ni Salim siyo Mwinyi ingekuwa hivyo. Neno la Thabit Kombo lilikuwa likishachukuliwa na Nyerere hakuna wa kumgomea. Unakumbuka yaliyomkuta Jumbe?
 
Sentesi yako ya mwisho ina kitu ambacho kinaonyesha matokeo ya mkakati wa siri (story nzima ya huu uzi ipo hapo) wenye akili wataelewa.
 
Nakubaliana nawe. Wadau mnafungua Code taratibu
 
Uko sahihi mkuu
 
Ni kweli bila Thabit Kombo historia ingekuwa tofauti sana alikuwa anaaminika sana na mwalimu kwenye nani awe nani
 
Aisee !!???? Hivi bila mitumba leo watu wangekuwa si wanatembea uchi kabisa let alone kuvaa viraka..... Production imeongezeka duniani na junks nyingi zinakuja Africa... (Ndio yale yale tunashangilia kuna Namba E nyingi Mtaani wakati watu wanaweka maiti Hospitali kwa kushindwa kuzikomboa)

Soko Huria ndio mpango mzima lakini Mentality ya Self Reliance ndio itatufanya tuwe rulers na sio followers...; Jambo ambalo kwa sasa tumekuwa madalali na wachuuzi...,

Hivi katika Viongozi wote kuna mtu alipata Hardships kama Nyerere (Vita vya Kagera / Mabeberu wa Kweli katika Vita Baridi (Acha wa sasa wa kufukirika); Hati hati ya kupinduliwa (sababu kipindi icho uki-side na Russia USA / CIA wapo tayari kumfadhili mwingine ili akuondoe (Waulize kina Sankara na Patrice Lumumba)...;
 
Nyerere alijenga viwanda sawa ila hakuwa mchumi mzuri na alikuwa aambiliki,sera zake zilikuwa impractical
 
Nyerere alijenga viwanda sawa ila hakuwa mchumi mzuri na alikuwa aambiliki,sera zake zilikuwa impractical
Sera practical za sasa ni zipi ?

Wewe unayeongelea Ubepari ndio wenyewe na ujamaa sio (ngoja nikupe case study ya USA) Mabenki yalifuja pesa na kuzitafuna yakaingia hasara kutaka kufirisika (they are too big to fail) ni kodi za mwananchi ndio zilitumika kuyakomboa hayo mabenki (yaani kwenye hasara mwananchi analipa / faida wanakula wenyewe)

Am all for Free market ndio maana hata socialists wenzetu china sasa hivi wame-adapt wana market socialism (mifumo inabadilika hata sisi tungebadilika kutokana na wakati)

Thatcher na model ya privatization ya UK ambayo waliona kila kitu kiwe privatized ni kwamba walichodhani sicho hadi watu wanaanza kufikiria re-nationalization...

Privatization, The God that Failed (lesson from UK)
 
Bongoman na chakachaka walipikuja nchini kiingilio ilikuwa laki moja .laki moja ndio,
Hii umetupiga cha utosi. Kanda Bongaman alitumbuiza ukumbi wa PTA Saba Saba kiingilio kikubwa kabisa ilikuwa Tsh 6000/-.
 
Naskia hadi kunyoa panki lazima uombe kibali. Wanaume wote lazima wachomekee. Marufuku wanawake kuvaa suruali. Chakula kilichoruhusiwa kuliwa asubuhi ni chai maandaz ana mkate wa boflo. Mchana ugali na mboga na nyama kidogo, usiku ni wali maharage. Ukila vyakula tofauti na hivyo lazima uombe kibali.

Halafu ni yeye pekee alikuwa na TV akiangalia utabiri wa hali ya hewa BBC mvua itanyesha kesho anatangazia umma na kweli mvua inanyesha hadi kina babu zake adriz wakamuita nabii.

Nyerere mgalatia mwenzetu katuangusha sana ila mwinyi Kobaaz akatukomboa.

adriz hydroxo Accumen Mo
 
Sina uhakika kama ni kweli baada ya jumbe kuondolewa kwenye urais wa zanzibar,alilidhiwa na mwinyi.Abdul wakil nombe sijui alimrithi nani?
 
Hajui lolote huyo,ni mshabiki na muongo mwongo tu.
 
Wewe utakufa na hizo chuki zako za kipumbavu.wewe kila kitu ni jpm tu,jadili hoja iliyopo mezani,kama wewe una hoja kuhusu jpm,anzisha mada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…