Sidhani kama kuna 'aliyemgeuka' au 'aliyemgomea' mwenzake. Ikumbukwe mpaka wanaenda katika vikao vya juu, jina la kutoka Zanzibar lilikuwa la Mzee Salim A. Salim. Na pia ndani ya CCM kuna Kamati Kuu (ndogo) ya CCM Zanzibar ambayo wana maamuzi kuhusu jambo mahususi linalohusu Zanzibar; hawa ndiyo waliopendekeza kuondoa jina la SAS. Na ikumbukwe pia Mzee AHM alikuwa tayari Rais wa SMZ na hakuwaza kuwa Rais wa JMT. Sasa kwa vile u-Rais uishanukia kwa Wazanzibar, ilibidi wao wapendekeze jina; na wakaona Mzee AHM tayari ameonesha uzoefu kwa miezi michache aliyoongoza SMZ. Jina lake lilipofikishwa vikaoni, kwa mshangao Mzee Kawawa naye akajitoa, likabaki jina moja!