Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi kuzikwa tarehe 2 badala ya siku ya kesho ndani ya masaa 24 ni kukiuka mazishi ya kiislam. Napendekeza ratiba ibadilishwe

Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi kuzikwa tarehe 2 badala ya siku ya kesho ndani ya masaa 24 ni kukiuka mazishi ya kiislam. Napendekeza ratiba ibadilishwe

Serikali kiasi flani ipo kikristo zaidi hayo mambo ya mud ni huko misikitini huyo ni alikuwa mtumishi wa uma sio shehe wa msiki ko angalia wingi wa utumishi wake upo wakristo sio suruali fupi!
 
Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi kafariki saa 11 na nusu jioni ya leo tarehe 29/2/2024 hivyo kwa taratibu za kiislam inabidi azikwe kesho 01/03/2024 kabla ya saa 11 na nusu jioni, ikipendeza zaidi ilibidi iwe kesho asubuhi au mchana

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayra رضى الله عنه akisema: Amesema Mtume ﷺ : “Harakisheni mazishi! Kwani kama maiti ni mja mwema basi haifai kumchelewesha, na kama ni mja muovu basi ni shari na balaa mnaweka mabegani mwenu.
Muttafaq Alayhi.

951. Imepokewa kutoka kwa Huswayn bin Wahwah akisema: “Aliumwa Twalha bin al-Baraa’ bin ‘Azib akatembelewa na Mtume nyumbani kwake. Baada ya kumuona, alisema: “Naona mwisho wa maisha ya Abu Twalha unakaribia, hivyo akifariki nijulisheni, na harakisheni kumtayarisha kumzika; kwani haifai kuachwa mzoga wa mwili wa Mwislamu kusalia nyumbani na familia yake” Ameipokea Abu Daud.
Hayo yalikuwa hivyo enzi hizo hakuna technology ya kuhifadhi maiti hata makabila yetu zamani hayakuchelewesha mazishi. Siku hizi mambo yamebadilika. Dini inahitaji uwe na akili huru la sivyo unakuwa mtumwa wa vitabu vya kale tu.
 
😂 Presha imepanda mtu akaamua alale kidogo kushtuka yupo shimoni na sanda juu
Huzikwi bila Daktari,kuthibitisha kifo.Na pia toka zamani wapo wanaojua kwa njia za kienyeji,kama mtu ameshafariki au bado.Hata wewe ukifundishwa,unaweza kuelewa.Fikiria wakristo wa zamani,wakati hakuna majokofu,hakuna madaktari wa kisasa,wafu walizikwa vipi.
 
Nyie mtu akizirai tu mnamtia futi sita bora si tunaokaa ktk friji ata wiki
Mtu yoyote,popote akifariki kwa dunia ya sasa,lazima aitwe daktari kuthibitisha kifo chake.Na huko zamani na mpaka sasa,wapo watu wanaoelewa,kama huyu kafariki au yuko hai.Hapo zamani,ilipokuwa hakuna madaktari,walikuwepo watu wanaofahamu,na mpaka leo wapo,wanaoweza kutambua kama huyu mtu,yuko hai au kafariki.
 
Uislam wa siki hizi ,huyo samis alienda makaburini chato kumzika jpm niloshamgaa sana
Vyeo vikubwa kama vile W/Mkuu,Makamu wa Rais na Rais kuna wakati ni lazima mtu akiuke misingi ya dini kwa kuwa Serikali haina dini kuna mambo lazima yaende nje ya utaratibu wa dini.
Rais ni Amiri Jeshi Mkuu, mazishi ya Kiserikali yeye ndiye mkuu wa Serikali anakosekanaje kwenye mazishi ?
 
Kwenye nukuu zako Kuna common phrases zimetumika, "haifai kumchelewesha" na harikisheni maziko", SWALI ni muda gani umeainishwa hapo wa kumchelewesha Marehem? Nadhani suala la kumchelewesha na kuwahisha linaendelana na mazingira pia
 
951. Imepokewa kutoka kwa Huswayn bin Wahwah harakisheni kumtayarisha kumzika; kwani haifai kuachwa mzoga wa mwili wa Mwislamu kusalia nyumbani na familia yake” Ameipokea Abu Daud.
Umepotoka mwili wa Mwinyi uko Hospital sio nyumbani kwa familia yake

Hicho kifungu Kilihusu miaka hiyo ambayo hakukuwa na hospitali wala mortuary maiti zilikuwa zinakuwa nyumbani kwenye familia zao

Kwa Hospital na mortuary muislamu aweza zikwa hata baada ya mwezi hata baada ya mwaka hajakiuka hicho kifungu
 
Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi kafariki saa 11 na nusu jioni ya leo tarehe 29/2/2024 hivyo kwa taratibu za kiislam inabidi azikwe kesho 01/03/2024 kabla ya saa 11 na nusu jioni, ikipendeza zaidi ilibidi iwe kesho asubuhi au mchana

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayra رضى الله عنه akisema: Amesema Mtume ﷺ : “Harakisheni mazishi! Kwani kama maiti ni mja mwema basi haifai kumchelewesha, na kama ni mja muovu basi ni shari na balaa mnaweka mabegani mwenu.
Muttafaq Alayhi.

951. Imepokewa kutoka kwa Huswayn bin Wahwah akisema: “Aliumwa Twalha bin al-Baraa’ bin ‘Azib akatembelewa na Mtume nyumbani kwake. Baada ya kumuona, alisema: “Naona mwisho wa maisha ya Abu Twalha unakaribia, hivyo akifariki nijulisheni, na harakisheni kumtayarisha kumzika; kwani haifai kuachwa mzoga wa mwili wa Mwislamu kusalia nyumbani na familia yake” Ameipokea Abu Daud.
Lakini mbona mtume wenu alikaa zaidi ya siku saba hadi akanuka ikabidi azikiwe chumbani mwake?
 
Back
Top Bottom