Tetesi: Hayawi Hayawi, Diamond kumposa Zuchu Ijumaa!

Tulimjibu huyo anayetaka kuombwa radhi. Mi najua taratibu za ndoa za kiislam vizuri sana.
Kila kinachoendelea napewa taarifa tokea juzi, lakini siwezi kuandika hapa yote.

Inabidi nikae nichambue na tukubaliane namna ya uwasilishaji.

Watu wanafikiri kuwaleteeni habari hapa ni jambo rahisi, sivyo!
 
Uko sahihi sawa tuu
 
Hapa sio chumbani binti...

Ukileta tarifa kwenye jukwaa la wazi kama hili ni lazima ijadiliwe na ipimwe...

Ikijaa kwenye vipimo vya ukweli, wasomaji tunatoa credit na credibility ya mtoa habari inapanda...

Ukileta tarifa ya uongo ni busara kuomba radhi japo sio lazima, lakini ukiomba radhi utapewa credit na credibility yako itabaki juu.
Mbona tokea jana nilisema nitawafahamisha kilichojiri? Uamuzi uko kwangu wa kuleta mrejesho na sio wewe unipangie.

Habari nimeleta mimi, mamlaka yote ninayo mimi.

Sihitaji credibility kutoka kwa yeyote maana hainifaidishi chochote, chil.
 
Habari nimeleta mimi, mamlaka yote ninayo mimi.
Ulikua na mamlaka ya kuileta habari ila kuithibitisha ni sisi tunakulazimisha ili kesho ujifunze kupima tarifa kabla hujaileta humu.
 
Mkuu, nitaendelea kufanya ninachokifanya kama ambavyo nimekuwa nikifanya siku zote.

Kama ambavyo sikushauriana na wewe/nyie kabla, sina cha kusikiliza kutoka kwako hivi sasa.

Kwa vile umeona nilichokileta ni uongo, acha kufuatilia yote ninayoyaleta hapa. Ukifuatilia usilete usumbufu kwa maamuzi yako mwenyewe.
 
Na mimi nakujulisha, habari inakua yako kabla hujaileta humu...

Ukishaipost humu, wadau tuna haki ya kuijadili na kuipima ikiwa ni ya ukweli au lah...

Kama habari uliyoleta ni ya uongo, wadau tuna haki ya kukushauri uachane na habari ambazo hazina ukweli...
 
View attachment 3225842

Hatimaye!
Baada ya sarakasi nyingi, Msanii Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amekata shauri la kumuoa mpenzi wake ambaye ni msanii ndani ya lebo yake ya muziki (WCB) Zuhura Othman Soud ‘Zuchu’

Uamuzi huo umekuja huku kukiwa na sintofahamu nyingi juu ya mahusiano yao ambapo mwishoni mwa mwaka jana Zuchu alitangaza kwa mara nyingine kuachana kwao japo amekuwa akifanya hivyo mara nyingi na baadaye kurudiana.

Safari hii mambo yamekuwa tofauti kidogo baada ya majuzi kuibuka ugomvi ndani ya kampuni upande wa redio kwa Zuchu kuwashutumu wafanyakazi wa Diamond kumvunjia heshima.

Zuchu ameonekana ‘kukaza’, hajacheka na yeyote akiwemo Diamond mwenyewe na pengine hili limesogeza karibu ndoa yao.

Zuchu ameshinda vita iliyowashinda wengi?…
The mother in law from hell, Mama Diamond amekuwa mwiba mchungu takribani kwa kila mwanamke aliyetoka kimapenzi na Diamond.

Amesemekana kikwazo kikuu kwa Diamond kuoa, hivyo posa hii kwa Zuchu inatuacha njia panda kwamba Mama Dangote kapata kiboko yake? Je posa hii ina baraka za mama yake Diamond?

Ndoa ni kabla ya Ramadhani…
Mwezi uliopita Diamond akiwa na msanii mwenzie Nandy katika mkutano mkuu wa CCM, alionekana akisema atamuoa Zuchu kabla ya Ramadhani ya mwaka huu ambayo inategemewa kuanza mapema mwezi Machi.

Diamond amekuwa akitoa ahadi nyingi hivyo wengi hatukuchukulia tamko lile kwa uzito, nimeshtuka baada ya kupewa taarifa za uhakika kuwa ni kweli na posa hiyo itapelekwa nyumbani kwa Bi Khadija Kopa Ijumaa ya kesho kutwa tarehe 7.

Haya jamani, mambo ndio yako hivyo na hii ni habari endelevu nitakuwa hapa kuwajuza mapema kadiri nitakavyopokea taarifa.

Straight From The Horse’s Mouth,

Nifah.
Ijumaa si ni jana? Au ulitaka kutuambia habari za Jux
 
Ulikua na mamlaka ya kuileta habari ila kuithibitisha ni sisi tunakulazimisha ili kesho ujifunze kupima tarifa kabla hujaileta humu.
Kwani umealazimishwa kuifuatilia mkuu mbona umemshupalia dada? Wasiotaka umbea wala kujua ni wa kweli au la wanasoma kimyakimya wala hawacomment na wengine hawapiti kabisa jukwaa hili. Kama wewe ni mpenda umbeya kaa kwa kuulia
 
Siku ukiletwa umbeya unaokushutumu kwa uongo wewe au mtu wako wa karibu ndio utajua athari za habari za uongo.
 
A quick update…

Kuna mvutano mkubwa katika familia juu ya posa ya Naseeb kwa Zuhura, familia yote ya Naseeb haimtaki kabisa Zuhura.

Uamuzi wa kwenda kutoa posa aliufanya mwenyewe Naseeb na watu wake wachache wa karibu bila ya kumfahamisha yeyote katika familia yake, hivyo hii ilikuwa taarifa nyeti kwangu mimi kuipata maana hakuna yeyote katika familia yake aliyekuwa akifahamu hili.

Taarifa ya kama posa ilipelekwa au lah itawajia tu, maana taratibu nyingine za mahari na ndoa zitafuata ambazo nitapewa taarifa pia.

Binafsi nimewaonea huruma sana, hii vita ni kubwa kwao kuivuka salama na kufanikisha kufunga ndoa.

Nasisitiza, nitawaletea taarifa pindi nitakapopata uhakika. Mkiona kimya endeleeni kusubiri hili sio jambo la haraka na siwezi kuwapa taarifa nisizo na uhakika nazo.

Cheers
 
View attachment 3225842

Hatimaye!
Baada ya sarakasi nyingi, Msanii Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amekata shauri la kumuoa mpenzi wake ambaye ni msanii ndani ya lebo yake ya muziki (WCB) Zuhura Othman Soud ‘Zuchu’

Uamuzi huo umekuja huku kukiwa na sintofahamu nyingi juu ya mahusiano yao ambapo mwishoni mwa mwaka jana Zuchu alitangaza kwa mara nyingine kuachana kwao japo amekuwa akifanya hivyo mara nyingi na baadaye kurudiana.

Safari hii mambo yamekuwa tofauti kidogo baada ya majuzi kuibuka ugomvi ndani ya kampuni upande wa redio kwa Zuchu kuwashutumu wafanyakazi wa Diamond kumvunjia heshima.

Zuchu ameonekana ‘kukaza’, hajacheka na yeyote akiwemo Diamond mwenyewe na pengine hili limesogeza karibu ndoa yao.

Zuchu ameshinda vita iliyowashinda wengi?…
The mother in law from hell, Mama Diamond amekuwa mwiba mchungu takribani kwa kila mwanamke aliyetoka kimapenzi na Diamond.

Amesemekana kikwazo kikuu kwa Diamond kuoa, hivyo posa hii kwa Zuchu inatuacha njia panda kwamba Mama Dangote kapata kiboko yake? Je posa hii ina baraka za mama yake Diamond?

Ndoa ni kabla ya Ramadhani…
Mwezi uliopita Diamond akiwa na msanii mwenzie Nandy katika mkutano mkuu wa CCM, alionekana akisema atamuoa Zuchu kabla ya Ramadhani ya mwaka huu ambayo inategemewa kuanza mapema mwezi Machi.

Diamond amekuwa akitoa ahadi nyingi hivyo wengi hatukuchukulia tamko lile kwa uzito, nimeshtuka baada ya kupewa taarifa za uhakika kuwa ni kweli na posa hiyo itapelekwa nyumbani kwa Bi Khadija Kopa Ijumaa ya kesho kutwa tarehe 7.

Haya jamani, mambo ndio yako hivyo na hii ni habari endelevu nitakuwa hapa kuwajuza mapema kadiri nitakavyopokea taarifa.

Straight From The Horse’s Mouth,

Nifah.
Ijumaa ipi iyo
 
A quick update…

Kuna mvutano mkubwa katika familia juu ya posa ya Naseeb kwa Zuhura, familia yote ya Naseeb haimtaki kabisa Zuhura.

Uamuzi wa kwenda kutoa posa aliufanya mwenyewe Naseeb na watu wake wachache wa karibu bila ya kumfahamisha yeyote katika familia yake, hivyo hii ilikuwa taarifa nyeti kwangu mimi kuipata maana hakuna yeyote katika familia yake aliyekuwa akifahamu hili.

Taarifa ya kama posa ilipelekwa au lah itawajia tu, maana taratibu nyingine za mahari na ndoa zitafuata ambazo nitapewa taarifa pia.

Binafsi nimewaonea huruma sana, hii vita ni kubwa kwao kuivuka salama na kufanikisha kufunga ndoa.

Nasisitiza, nitawaletea taarifa pindi nitakapopata uhakika. Mkiona kimya endeleeni kusubiri hili sio jambo la haraka na siwezi kuwapa taarifa nisizo na uhakika nazo.

Cheers
Sio vema kupika habari mdogo wangu. Umaarufu wa jamiiforum usitafutwe kwa kupika habari za uongo. Hakuna kitu kama hiki kinaendelea. Mama Dangote asijue kijana wake wa pekee kuwa anaenda kutoa posa ujue wewe chakubimbi?
 
Diamond kuwa mwanaume fanya maamuzi magumu, posa uoe, familia yako inadhani ukioa utashindwa kuendelea providing for them, hivyo kila mwanamke watamuona ni THREAT, ukiwaendekeza huoi ng'o
 
This time naona kaamua kweli, hataki tena ujinga wa kumsikiliza mama yake.

Ameamua kufanya jambo lake na marafiki. Kila mwanamke familia haimtaki!

Sijui ndoa itakuwaje? Watamsusia?
Hebu ngoja tuone.
 
A quick update…

Kuna mvutano mkubwa katika familia juu ya posa ya Naseeb kwa Zuhura, familia yote ya Naseeb haimtaki kabisa Zuhura.

Uamuzi wa kwenda kutoa posa aliufanya mwenyewe Naseeb na watu wake wachache wa karibu bila ya kumfahamisha yeyote katika familia yake, hivyo hii ilikuwa taarifa nyeti kwangu mimi kuipata maana hakuna yeyote katika familia yake aliyekuwa akifahamu hili.

Taarifa ya kama posa ilipelekwa au lah itawajia tu, maana taratibu nyingine za mahari na ndoa zitafuata ambazo nitapewa taarifa pia.

Binafsi nimewaonea huruma sana, hii vita ni kubwa kwao kuivuka salama na kufanikisha kufunga ndoa.

Nasisitiza, nitawaletea taarifa pindi nitakapopata uhakika. Mkiona kimya endeleeni kusubiri hili sio jambo la haraka na siwezi kuwapa taarifa nisizo na uhakika nazo.

Cheers
Hawezi kufanya lolote bila Wazazi wake kujua, nikishaanza kuona mtu anaweka "ninge ange Inge" jua anatuuzia masaro

Beautiful liar
 
Back
Top Bottom