Hayawi hayawi sasa yamekuwa, hatimae Yanga SC yapata ushindi kwa mara ya kwanza baada ya miaka 80

Hayawi hayawi sasa yamekuwa, hatimae Yanga SC yapata ushindi kwa mara ya kwanza baada ya miaka 80

Ndugu zangu vifijo na nderemu vimetawala mitaa ya jangwani baada ya klabu ya yanga kujipatia ushindi kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo.

Ikumbukwe mapema leo klabu hiyo ilikuwa ikipepetana dhidi ya timu kibonde kutoka Ghana medeama fc kisha kuichabanga magoli matatu kwa mtungi.

Baada ya kuibuka na ushindi huo sasa kumeibua matumaini ya kusonga mbele zaidi katika michuano hiyo huku ikiiombea mabaya CR Belouzdad ya algeria.

Watanzania wote kwa ujumla tunaipongeza yanga sc kwa hatua hiyo kubwa waliyoifikia toka kuanzishwa kwa klabu hiyo.
1703135759131.png


2023 -80 = 1943..!!
 
Ndugu mbumbumbu lazima utambue mambo ya makundi yameanza hivi karibuni, mwaka 1998 wakati Yanga Alisha cheza robo fainali ya klabu bingwa Afrika mara 2.
Haina mantiki yoyote kufananisha hatua za makundi wakati timu imecheza robo mara 2.
Tena iyo hatua ya makundi ya mwaka 1998 ili husisha timu 8 zilizo anza na timu zaidi ya 50, kukawa na Makundi mawili A,B ambayo yalikua na timu 4 Kila kundi maana yake ilikua ni hatua ya robo fainali.
Robo usifananishe na Makundi.
Mbona mnabishia kitu kilichowazi!!? Ni kweli nakundi yalianza 1998. Na Yanga alicheza kwenye ligi hiyo. Hakushinda hata mchezo mmoja. Kama ambavyo inasemwa, na ndivyo ukweli ulivyo kuwa ni zaidi ya miaka 20 Yanga haijaingia makundi ACL, ndivyo hivyo inaeleweka ilikuwa haijawahi kushinda kwenye huu utaratibu wa makundi, na jana, ndiyo mchezo wake wa kwanza kushinda!
Kama sivyo hivyo, si ielezwe!!!?
 
Yanga ina bahati ya kukutana na timu vibonde


Hata tarehe 5/11/2023 ilikutana na timu kibonde ikaibonda 5:1😂😂😂
Wakicheza wao Champions league huwa inakuwa haina vibonde, wakicheza Yanga ndiyo vibonde hutokelezea.
Msimu uliopita walidai vibonde wapo shirikisho, this time wameshaisahau kauli yao, wanadai vibonde wapo Champions.

Wanampamba Wydad aonekane ni giant, wakati kwenye kundi lao, point pekee alizo nazo Wydad alizipata kwa kuwafunga Simba na mechi pekee aliyoshinda Simba hadi sasa ni aliyowafunga Wydad
 
Back
Top Bottom