Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Biblia ilitabiri zamani sana kuhusu siku tunazoishi leo. Katika Danieli 12:4 imeandikwa: “Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie mhuri kitabu, hata wakati wa mwisho. Wengi wataenda mbio huku na huko, na maarifa yataongezeka.”
Unabii huo tumeona ukitimia waziwazi kwa macho yetu. Maarifa yameongezeka kwa kiwango kisicho cha kawaida, na safari za kasi kubwa zimekuwa halisi. Juzi, katika misheni ya NASA - Artemis, chombo cha Orion kilisafiri kwa kasi ya takribani 36,000 km/h kuelekea Mwezini.
Wakati wa Mtume Paulo, hakukuwa na hata wazo la kasi ya namna hiyo. Leo hii mwanadamu anasafiri kwa maelfu ya kilomita kwa saa, kama Danieli alivyotabiri kwamba siku za mwisho “watu wataenda mbio huku na huko.”
Hii sio coincidence. Ni ishara kwamba tunaishi katika nyakati ambazo Biblia ilizitabiri. Hizi ni siku za mwisho. Ndio maana tunakumbushwa tena na tena na Yesu Kristo:
“Kesheni basi, kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.” (Mathayo 24:42)
Ndugu yangu, Yesu yuaja upesi(Ufu 22:10-12). Jiweke tayari kwa kutubu na kuamini kuwa Yesu alikufa msalabani na kufufuka kwa ajili yetu, na ukubali awe Bwana na Mwokozi wako, kisha uanze kuishi maisha matakatifu (Ebr 12:14). Kumbuka Mwana wa Adamu(Yesu Kristo) atakuja siku na saa usiyodhani. Siku Yesu atakapokuja, atawanyakua watakatifu tu na kuwapeleka mbinguni. Wenye dhambi wataachwa katika dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea tangu kuumbwa kwa ulimwengu!