Hayawi, hayawi, yamekuwa! Teknolojia imethibitisha tena ukweli wa Biblia!

niulize na mimi siamini dini yaan mda kumuuliza ckuwa nao hata kidogo yaan nilimuona kama chizi flani. Duniani amini unachoamini maisha yasonge.
Umesema huamini dini. Mimi nasema hivi: kukataa dini kwa ujumla sio sahihi. Dini ni njia ya kuunganishwa na ukweli wa maisha.

Nakusihi leo uanze kuchunguza habari za dini, na njia bora zaidi ni kupitia Biblia. Biblia imehakikishwa na maelfu ya watu kuwa ni kitabu cha kweli, kupitia historia na matukio ya maisha ya wanadamu.

Katika Biblia utasoma habari za Yesu ambazo zimehakikishwa pia kuwa ni za kweli: mambo aliyosema Yesu, matendo yake, na wokovu alioleta kwa wanadamu yameandikwa kwa usahihi. Ukiisoma Biblia kwa makini utaupata ukweli unaoweza kubadilisha kabisa maisha yako milele.
 
Biblia ulisema ni Maarifa gani Mkuu?
Kwa ujumla, maarifa yanayozungumziwa hapo kuwa yataongezeka, ni ufahamu wa mambo mengi ya kiroho, ufahamu wa Neno la Mungu na maarifa ya sayansi na teknolojia.
 
Yes huu ndio moja kati ya utabiri ambao naupenda sana ukisoma tafsiri ya globalization ni interaction of people company na growth of technology ambayo ni what exactly Daniel alisema back in 500BC
 
Umesema huamini dini. Mimi nasema hivi: kukataa dini kwa ujumla sio sahihi. Dini ni njia ya kuunganishwa na ukweli wa maisha.

Nakusihi leo uanze kuchunguza habari za dini, na njia bora zaidi ni kupitia Biblia. Biblia imehakikishwa na maelfu ya watu kuwa ni kitabu cha kweli, kupitia historia na matukio ya maisha ya wanadamu.

Katika Biblia utasoma habari za Yesu ambazo zimehakikishwa pia kuwa ni za kweli: mambo aliyosema Yesu, matendo yake, na wokovu alioleta kwa wanadamu yameandikwa kwa usahihi. Ukiisoma Biblia kwa makini utaupata ukweli unaoweza kubadilisha kabisa maisha yako milele.
kunishauri about dini ni kupoteza mda wako bure we amin unachokiamini maisha yasonge. Mim ukianza kunihubiria mimi ndugu yangu mara ya mwisho n kofi za macho utakutana nazo tukiwa karibu. Hizph dini zililetwa kutusumbulia akili
 
Hahaa, ukinipiga kofi shavu la kulia, nakugeuzia na la kushoto unipige ili ujisikie umenipiga vizuri. Halafu subiri sasa siku utakayoondoka duniani na kukutana na aliyekuumba, ndio utajua ulikuwa hujui umuhimu wa dini.

By the way, dini unaikataa lakini kuku kumi za mwenye dini ulikula
 
Hiyo Koro Syndrome ni shetani anawaonea wanaopuuza nguvu ya maombi.
Wewe hujajua nguvu ya maombi. Paulo na Sila waliomba wakiwa gerezani, milango ya gereza ikafunguka. Soma Matendo 16:25-40
"Karibu na usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakisali na kuimba nyimbo za kumsifu Mungu, huku wafungwa wengine wakiwa wanasikiliza. Ghafla, kulitokea mtetemeko mkuu wa ardhi ambao uliitikisa misingi ya gereza. Mara, milango yote ikafunguka na minyororo iliyowafunga hao wafungwa ikaachana. Askari wa gereza alipoamka na kuiona milango ya gereza imefunguliwa, alidhani kwamba wafungwa wote walikuwa wametoroka, na hivyo akauchomoa upanga wake, akataka kujiua. Lakini Paulo akaita kwa sauti kubwa: “Usijidhuru mwenyewe kwa maana sisi sote tuko hapa.” Baada ya kumwita mtu alete taa, huyo askari wa gereza alikimbilia ndani, akajitupa mbele ya miguu ya Paulo na Sila huku akitetemeka kwa hofu. Halafu aliwaongoza nje, akawauliza, “Waheshimiwa, nifanye nini nipate kuokoka?” Wao wakamjibu, “Mwamini Bwana Yesu nawe utaokolewa pamoja na jamaa yako yote.” Basi, wakamhubiria neno la Bwana yeye pamoja na jamaa yake. Yule askari aliwachukua saa ileile ya usiku akawasafisha majeraha yao, kisha yeye na jamaa yake wakabatizwa papo hapo. [ Halafu akawachukua Paulo na Sila nyumbani kwake, akawapa chakula. Yeye na jamaa yake yote wakafanya sherehe kwa vile sasa walikuwa wanamwamini Mungu]. Kesho yake asubuhi, mahakimu waliwatuma maofisa wao wakisema, “Wafungueni wale watu.” Yule askari wa gereza alimpasha habari Paulo: “Mahakimu wametuma ujumbe ili mfunguliwe. Sasa mnaweza kutoka na kwenda zenu kwa amani.” Lakini Paulo alimjibu, “Ati nini? Ingawa hatukuwa na kosa, walitupiga viboko hadharani hali sisi ni raia wa Roma. Tena, walitutia ndani na sasa wanataka kutufungulia kwa siri! Hata kidogo! Ni lazima wao wenyewe waje hapa watufungulie.” Hao maofisa waliwapasha habari mahakimu juu ya jambo hilo, nao waliposikia kwamba Paulo na Sila walikuwa raia wa Roma, waliogopa. Hivyo, walikwenda kuwataka radhi na baada ya kuwatoa ndani waliwaomba watoke katika mji ule."
Huu ni ujinga mtupu Imani potofu na ujinga.

Dini inakuharibu, inakupumbaza, inakulimit usifikirie nje ya box/mfumo, inakupa kiburi cha kudhani unajua sana kiasi kwamba hukubali ushahidi wa kisayansi, inakufanya unajua mjuaji na kudhani mawazo ya wengi/fact sio sahihi.

Ili tuendelee lazima tukubaliane huu ujinga wa dini, hautufanyi tuendelee Jamii yenye mshikamano ndio jamii inayokua, Jamii inayokubali kujifunza na kuelimika itaendelea, Jamii yenye watu wanafikiri nje ya box ni jamii itakayo endelea.
 
Huu ni ujinga mtupu Imani potofu na ujinga.

Dini inakuharibu, inakupumbaza, inakulimit usifikirie nje ya box/mfumo, inakupa kiburi cha kudhani unajua sana kiasi kwamba hukubali ushahidi wa kisayansi, inakufanya unajua mjuaji na kudhani mawazo ya wengi/fact sio sahihi.
My friend, umeninyoshea kidole kimoja lakini vitatu vinakunyoshea wewe pia. Hivyo na wewe sayansi isikuharibu ukaacha kufikiria nje ya box. Sayansi isikupe kudhani unajua sana kiasi kwamba huna haja ya kukubali ushahidi wa kiroho. Mambo ya kishetani yapo. Na hayo huwezi kuyajua scientifically. Mapepo huwezi kuyaona kwa vipimo vya maabara. Na nguvu ya maombi huwezi kuithibitisha kisayansi. Ugonjwa gani huo eti mtu akuguse bega tu halafu viungo vyako vya siri vinasinyaa. Shetani ni muongo na baba wa uongo. Anawaonea watu lakini hataki watu wajue kuwa ni yeye anayefanya hivyo.

Mimi nina ushahidi wa kutosha kuhusu nguvu za giza na magonjwa yatokanayo na mapepo. Kama ningekuwa mtu wa kukubali upande mmoja tu wa sayansi, nisingekuwepo duniani leo. Najua kuna magonjwa yaliyothibitishwa kisayansi lakini najua pia yapo magonjwa yanayosababishwa directly na shetani na haya huwezi kuyathibitisha kisayansi. Magonjwa ya namna hii utapoteza mali na muda bure kuya-treat with psychotherapy and anxiolytics.

Respectfully, dismissing spiritual causation as ‘foolishness’ does not, in itself, invalidate its possibility. It merely reflects a prior commitment to a purely material framework. Even within modern medicine, there remain conditions whose origins are not fully understood, and whose treatments are often limited to management rather than complete restoration.

Hospitals, for all their advancement, rarely restore a deaf and mute individual to perfect wholeness. Yet in the biblical record, Jesus Christ accomplished precisely that with a word, and the condition was explicitly linked to demonic influence, not merely biology.

The real question, then, is not whether science has value, it certainly does, but whether it is exhaustive. If you assume only the material exists, you’ve already limited your conclusion; rejecting the spiritual doesn’t prove it false, it only exposes the limits of your framework.
 
coz msabato kwa kufatilia na kuchambua sayansi na dini kwa kutumia vipengele vya bibila hao watu waache tu. Akina Mwampo na akina kitima pamoja na akina abdi hawa huo mda wa kuchambua sayansi. Nakumbuka mwaka 2000 wasabato walitangaza kuwa ndio mwisho wa dunia eti kuna jiwe kubwa huko juu linakaribia kuanguka watu wajipange. Mda huo nilikuwa nafuga kuku nilishangaa ananiletea kuku kumi ati yeye anaenda kukutana na mungu. Tukasubiri hadi wa leo
Wasabato ni mabingwa wa kupotoshwa. Mwaka 1844 pia waliambiwa ni mwisho wa dunia. Na hata miaka ya nyuma waliaminishwa wanaweza kwenda Ulaya kuhubiri injili bila nauli, passport wala visa... wakasumbua sana pale Airport
 
Biblia ilitabiri zamani sana kuhusu siku tunazoishi leo. Katika Danieli 12:4 imeandikwa: “Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie mhuri kitabu, hata wakati wa mwisho. Wengi wataenda mbio huku na huko, na maarifa yataongezeka.”

Unabii huo tumeona ukitimia waziwazi kwa macho yetu. Maarifa yameongezeka kwa kiwango kisicho cha kawaida, na safari za kasi kubwa zimekuwa halisi. Juzi, katika misheni ya NASA - Artemis, chombo cha Orion kilisafiri kwa kasi ya takribani 36,000 km/h kuelekea Mwezini.

Wakati wa Mtume Paulo, hakukuwa na hata wazo la kasi ya namna hiyo. Leo hii mwanadamu anasafiri kwa maelfu ya kilomita kwa saa, kama Danieli alivyotabiri kwamba siku za mwisho “watu wataenda mbio huku na huko.”

Hii sio coincidence. Ni ishara kwamba tunaishi katika nyakati ambazo Biblia ilizitabiri. Hizi ni siku za mwisho. Ndio maana tunakumbushwa tena na tena na Yesu Kristo:
“Kesheni basi, kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.” (Mathayo 24:42)

Ndugu yangu, Yesu yuaja upesi(Ufu 22:10-12). Jiweke tayari kwa kutubu na kuamini kuwa Yesu alikufa msalabani na kufufuka kwa ajili yetu, na ukubali awe Bwana na Mwokozi wako, kisha uanze kuishi maisha matakatifu (Ebr 12:14). Kumbuka Mwana wa Adamu(Yesu Kristo) atakuja siku na saa usiyodhani. Siku Yesu atakapokuja, atawanyakua watakatifu tu na kuwapeleka mbinguni. Wenye dhambi wataachwa katika dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea tangu kuumbwa kwa ulimwengu!

hivi unayajua aliyokuwa anayafanya Nabii Somon kweli?
Solomon aliweza kutuma mtu akaenda bara hindi pengine kwa dakika 2, kuamrisha upepo, wanyama wote na hata ndege walimtii, nk na watu wake wenye AKILI hawakumuita Mungu.
Ninacho maanisha mengi yalishakuwepo ni watu tu, hawazingatii
Ukitaka kumjua Mungu: Anza na kuangaLia mwili wako unavyofanya kazi.... huo ni muujiza tosha hasa kama unauelewa mpana kidogo wa kujua kinachofanyika ndani ya mwili wako...
 
Dah, upo? Nimezimiss comment zako sana.
Pole kwa Wasabato. Anyway, hata wasio na dini wanapotoshwa tu
 
My friend, umeninyoshea kidole kimoja lakini vitatu vinakunyoshea wewe pia. Hivyo na wewe sayansi isikuharibu ukaacha kufikiria nje ya box. Sayansi isikupe kudhani unajua sana kiasi kwamba huna haja ya kukubali ushahidi wa kiroho. Mambo ya kishetani yapo. Na hayo huwezi kuyajua scientifically. Mapepo huwezi kuyaona kwa vipimo vya maabara. Na nguvu ya maombi huwezi kuithibitisha kisayansi. Ugonjwa gani huo eti mtu akuguse bega tu halafu viungo vyako vya siri vinasinyaa. Shetani ni muongo na baba wa uongo. Anawaonea watu lakini hataki watu wajue kuwa ni yeye anayefanya hivyo.

Mimi nina ushahidi wa kutosha kuhusu nguvu za giza na magonjwa yatokanayo na mapepo. Kama ningekuwa mtu wa kukubali upande mmoja tu wa sayansi, nisingekuwepo duniani leo. Najua kuna magonjwa yaliyothibitishwa kisayansi lakini najua pia yapo magonjwa yanayosababishwa directly na shetani na haya huwezi kuyathibitisha kisayansi. Magonjwa ya namna hii utapoteza mali na muda bure kuya-treat with psychotherapy and anxiolytics.

Respectfully, dismissing spiritual causation as ‘foolishness’ does not, in itself, invalidate its possibility. It merely reflects a prior commitment to a purely material framework. Even within modern medicine, there remain conditions whose origins are not fully understood, and whose treatments are often limited to management rather than complete restoration.

Hospitals, for all their advancement, rarely restore a deaf and mute individual to perfect wholeness. Yet in the biblical record, Jesus Christ accomplished precisely that with a word, and the condition was explicitly linked to demonic influence, not merely biology.

The real question, then, is not whether science has value, it certainly does, but whether it is exhaustive. If you assume only the material exists, you’ve already limited your conclusion; rejecting the spiritual doesn’t prove it false, it only exposes the limits of your framework.
Naona how you think inside the matrix. Una Imani za kidini, ni ugonjwa gani wa kipepo? Mbona maombi hayatibu waliopata ajali na jeurika?

Ukinwu
hivi unayajua aliyokuwa anayafanya Nabii Somon kweli?
Solomon aliweza kutuma mtu akaenda bara hindi pengine kwa dakika 2, kuamrisha upepo, wanyama wote na hata ndege walimtii, nk na watu wake wenye AKILI hawakumuita Mungu.
Ninacho maanisha mengi yalishakuwepo ni watu tu, hawazingatii
Ukitaka kumjua Mungu: Anza na kuangaLia mwili wako unavyofanya kazi.... huo ni muujiza tosha hasa kama unauelewa mpana kidogo wa kujua kinachofanyika ndani ya mwili wako...
Kwahiyo Mungu ndio anaua watu kwa magonjwa?

Mungu ndio anaeua watoto wadogo, kuruhusu walemavu wazaliwe?

Ndiye anaye wabariki watoa sadaka, na watu flani kuwa matajiri huku maskini wakiahidiwa ufalme wa mbingu wakiishi kwa kuteseka?

Kuna màan gani ya maisha kama anaishi kwa kujificha hivyo?
 
Biblia ilitabiri zamani sana kuhusu siku tunazoishi leo. Katika Danieli 12:4 imeandikwa: “Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie mhuri kitabu, hata wakati wa mwisho. Wengi wataenda mbio huku na huko, na maarifa yataongezeka.”

Unabii huo tumeona ukitimia waziwazi kwa macho yetu. Maarifa yameongezeka kwa kiwango kisicho cha kawaida, na safari za kasi kubwa zimekuwa halisi. Juzi, katika misheni ya NASA - Artemis, chombo cha Orion kilisafiri kwa kasi ya takribani 36,000 km/h kuelekea Mwezini.

Wakati wa Mtume Paulo, hakukuwa na hata wazo la kasi ya namna hiyo. Leo hii mwanadamu anasafiri kwa maelfu ya kilomita kwa saa, kama Danieli alivyotabiri kwamba siku za mwisho “watu wataenda mbio huku na huko.”

Hii sio coincidence. Ni ishara kwamba tunaishi katika nyakati ambazo Biblia ilizitabiri. Hizi ni siku za mwisho. Ndio maana tunakumbushwa tena na tena na Yesu Kristo:
“Kesheni basi, kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.” (Mathayo 24:42)

Ndugu yangu, Yesu yuaja upesi(Ufu 22:10-12). Jiweke tayari kwa kutubu na kuamini kuwa Yesu alikufa msalabani na kufufuka kwa ajili yetu, na ukubali awe Bwana na Mwokozi wako, kisha uanze kuishi maisha matakatifu (Ebr 12:14). Kumbuka Mwana wa Adamu(Yesu Kristo) atakuja siku na saa usiyodhani. Siku Yesu atakapokuja, atawanyakua watakatifu tu na kuwapeleka mbinguni. Wenye dhambi wataachwa katika dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea tangu kuumbwa kwa ulimwengu!
Huku na huko ndiyo mwezini, kwanini hakuwa specific kwamba watu wataenda mwezini? Kuna sehemu watu hao wa kale walizungumzia cloning, AI, plastic surgery, DNA, quantum mechanics?
 
Naona how you think inside the matrix. Una Imani za kidini, ni ugonjwa gani wa kipepo? Mbona maombi hayatibu waliopata ajali na jeurika?
Tayari nimeishakupa mfano mmoja wa magonjwa ya kipepo. Soma Biblia utaona mifano mingi zaidi. Halafu usifikiri mimi napingana na kazi wanazozifanya madaktari. Hata mimi huwa nakwenda hospitali kutibiwa. Lakini kuna wakati tiba za hospitali zinafeli, hapo ndipo ninapoweka gia ya pili: Natamka jina la Yesu. Hata hivyo maombi hayapingani na matibabu ya hospitali, vinaweza kwenda pamoja.

Kama hujasikia waliopata ajali wamepona kwa maombi, usiseme mbona maombi hayatibu. Hudhuria ibada za makanisa yanayoamini nguvu na miujiza ya Yesu, utasikia shuhuda nyingi za uponyaji. Mimi nimejeruhika mara nyingi tu na nimepona kwa maombi.
 
Huku na huko ndiyo mwezini, kwanini hakuwa specific kwamba watu wataenda mwezini? Kuna sehemu watu hao wa kale walizungumzia cloning, AI, plastic surgery, DNA, quantum mechanics?
Unabii haukutolewa kama kitabu cha sayansi au orodha ya teknolojia. Lengo lake lilikuwa kuonyesha mwelekeo wa jumla, sio kutaja kila kitu kwa majina ya kisasa.

Kitabu cha Daniel hakisemi watu wataenda mwezini, bali kinasema ‘wataenda huku na huko, na maarifa yataongezeka.’ Hiyo ni kauli pana inayobeba ongezeko la usafiri na maarifa kwa ujumla wake.

Kudai angepaswa kutaja “AI, DNA, au kwenda mwezini” ni kusahau pia kuwa: lugha ya wakati huo haikuwa na maneno hayo. Hivyo watu wa wakati huo wasingeelewa dhana hizo. Unabii unatoa picha kubwa, sio maelezo ya kiufundi.

Kwahiyo nguvu ya unabii huo iko kwenye usahihi wa mwelekeo wake, sio kwenye kutaja majina ya teknolojia. Na ukweli ndio huo, leo hii, watu wanaenda kila mahali duniani na maarifa yameongezeka kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea. Cloning, AI, drones, nk ni sehemu ya ongezeko la maarifa.
 
Kujua kuwa maarifa yanaoengezeka/yataongezeka wala haihitaji nabii, mbumbumbu yoyote analifahamu hilo. Kama mtu amejaaliwa 'upeo special' kama unavyopambana kuaminisha watu hizo terms angezujua tu kwa kufunuliwa 'kimiujiza', mtu kusema kwenda huku na huko uioanishe na safari ya mwezini huo ni utapeli kama ulivyo utapeli mwingine wowote. Kwenda huku na huko ni sawa na kuzurura randomly ukichoka unarudi ulipoanzia, astronauts wanachofanya ni discovering and adventuring na si kwenda huku na huko(kuzurura).
 
Unajikanyaga tu kwa maneno mengi. Plan ya NASA wakitoka mwezini wanaenda Mars. Hiyo inatofauti gani na kusema huku na huko?

Unabii ni muhimu, unapotimia unatusaidia kujiandaa na Ujio wa Yesu. Hizi ni dalili ambazo kutimia kwake kunatufanya tukae mkao wa kunyakuliwa. Yesu alisema myaonapo hayo yote inueni nyuso zenu kwakuwa ukombozi wenu umekaribia
 
Mungu katupa akili wanadamu, lakino haitatuwezesha kujua namna uqezinkujua ulimwengu huu ulivyoubwa. Anatuona tunavyofurukuta lakini upeo tumenyimwa.
 
Akili gani mkuu everything you see around us is a result of curiosity.
 
Dah, upo? Nimezimiss comment zako sana.
Pole kwa Wasabato. Anyway, hata wasio na dini wanapotoshwa tu
Wewe ni miongoni mwa watu mliofanya nijawe na huruma na kuamua kusitisha uamuzi wa kujitoa humu JF. Kama ningeondoka JF kungeboa sana. Hizi nyuzi zingekosa kabisa wasomaji... Kimsingi JF ingeangamia.
 
Back
Top Bottom