Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 1,679
- 2,123
Wakuu, heshima zenu. Mna habari kwamba unabii huu nao tayari umetimia?
Mathayo 24:24 – "Kwa maana watatokea Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, ikiwezekana, hata walio wateule.”
Marko 13:6 – "Wengi watakuja kwa Jina langu wakidai, ‘Mimi ndiye[Yesu Kristo],’ nao watawadanganya wengi."
Tumezoea kusikia Manabii wa uongo kuliko Makristo wa Uongo. Makristo wa Uongo kwa Kiingereza ni “false Christs.” Hao ni watu wanaodai kuwa wao ni Kristo lakini wanawadanganya watu kwa mafundisho ya uongo na miujiza feki
Hizi ni baadhi ya Sifa/Tabia za Makristo wa Uongo:
Apollo Quiboloy wa Philippines
Anadai kuwa yeye ni "Mwana wa Mungu.” Mwaka 2021, Quiboloy alishtakiwa kwa kosa la kuwalazimisha wasichana na wavulana wajihusishe na ngono na kuwatishia kwamba wasipofanya hivyo wataangamia milele!
Alan John Miller wa Australia
Anadai kuwa yeye ni Yesu aliyerudi katika mwili mwingine. Mke wake Mary Suzanne naye anadai ndiye Mariamu Magdalene(Mary Magdalene).
Inri Cristo wa Brazil
Anadai yeye ni Yesu aliyerudi mara ya pili; na ana wafuasi.
Jung Myung-seok wa Korea Kusini
Anadai yeye ni Yesu aliyerejea mara ya pili, na kwamba yupo ili kukamilisha kazi iliyokuwa haijamalizika. Jung aliwahi kupatikana na hatia ya kubaka na kutumikia kifungo cha miaka 10.
Oscar Ramiro Ortega-Hernandez wa Marekani
Ortega-Hernandez alijitaja mwenyewe kuwa ni Yesu Kristo aliyetumwa kuja kumuangamiza aliyekuwa Rais wa 44 wa Marekani kwa madai kwamba ni Mpinga Kristo. Mwaka 2011 Ortega alikamatwa kwa kosa la kupiga risasi jengo la Ikulu ya Marekani.
Yesu wa Tongaren, Kenya
Hivi majuzi, huko Kenya alijitokeza mtu anayedai kuwa yeye ni Yesu. Wakati fulani wa Pasaka, vijana wa Kenya(Gen Z) walimtaka akubali kusulibiwa msalabani kama kweli yeye ni Yesu!
Ndugu zangu, Biblia ni kitabu cha kweli. Yaliyoandikwa miaka mingi iliyopita, tunaona yakitimia waziwazi katikati yetu. Unabii huo wa kuja kwa Makristo wa Uongo nao umetimizwa. Hiyo ni dalili kuwa Yesu amekaribia kurudi. Yesu atakaporudi, atawanyakua na kuwapeleka mbinguni wale tu waliofanya mambo haya:
Act swiftly before time eludes you. Do not be beguiled by the fleeting pleasures of this world, for they are merely a passing illusion. In heaven awaits an eternal and incomparable bliss.

- Wanadai wao ndio Yesu aliyerudi.
- Wanapotosha mafundisho ya Biblia
- Wanatenda ishara za uongo kwa kutumia ujanja, miujiza feki au hata kwa kutumia nguvu za giza(mapepo) ili kuwashawishi watu wawaamini
- Wanajiinua juu ya Kristo badala ya kuwaelekeza watu kwa Yesu. Wanatafuta kuwa na mali, umaarufu, kuheshimiwa na kuwa na “power”
Apollo Quiboloy wa Philippines
Anadai kuwa yeye ni "Mwana wa Mungu.” Mwaka 2021, Quiboloy alishtakiwa kwa kosa la kuwalazimisha wasichana na wavulana wajihusishe na ngono na kuwatishia kwamba wasipofanya hivyo wataangamia milele!
Alan John Miller wa Australia
Anadai kuwa yeye ni Yesu aliyerudi katika mwili mwingine. Mke wake Mary Suzanne naye anadai ndiye Mariamu Magdalene(Mary Magdalene).
Inri Cristo wa Brazil
Anadai yeye ni Yesu aliyerudi mara ya pili; na ana wafuasi.
Jung Myung-seok wa Korea Kusini
Anadai yeye ni Yesu aliyerejea mara ya pili, na kwamba yupo ili kukamilisha kazi iliyokuwa haijamalizika. Jung aliwahi kupatikana na hatia ya kubaka na kutumikia kifungo cha miaka 10.
Oscar Ramiro Ortega-Hernandez wa Marekani
Ortega-Hernandez alijitaja mwenyewe kuwa ni Yesu Kristo aliyetumwa kuja kumuangamiza aliyekuwa Rais wa 44 wa Marekani kwa madai kwamba ni Mpinga Kristo. Mwaka 2011 Ortega alikamatwa kwa kosa la kupiga risasi jengo la Ikulu ya Marekani.
Yesu wa Tongaren, Kenya
Hivi majuzi, huko Kenya alijitokeza mtu anayedai kuwa yeye ni Yesu. Wakati fulani wa Pasaka, vijana wa Kenya(Gen Z) walimtaka akubali kusulibiwa msalabani kama kweli yeye ni Yesu!
Ndugu zangu, Biblia ni kitabu cha kweli. Yaliyoandikwa miaka mingi iliyopita, tunaona yakitimia waziwazi katikati yetu. Unabii huo wa kuja kwa Makristo wa Uongo nao umetimizwa. Hiyo ni dalili kuwa Yesu amekaribia kurudi. Yesu atakaporudi, atawanyakua na kuwapeleka mbinguni wale tu waliofanya mambo haya:
- Waliotambua kuwa ni wenye dhambi (Warumi 3:23).
- Wanaokiri na Kuamini kuwa Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zao (Warumi 5:8).
- Waliotubu dhambi zao na kuziacha (Matendo 3:19).
- Waliompokea Yesu mioyoni mwao kwa imani atawale maisha yao (Warumi 10:10-13).
- Wanaoishi maisha mapya ya utakatifu katika Kristo (2 Wakorintho 5:17).