Hayawi, Hayawi, Yamekuwa! Wakristo wa Uongo Tayari Wametokea

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
1,679
Reaction score
2,123
Wakuu, heshima zenu. Mna habari kwamba unabii huu nao tayari umetimia?
Mathayo 24:24 – "Kwa maana watatokea Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, ikiwezekana, hata walio wateule.”
Marko 13:6 – "Wengi watakuja kwa Jina langu wakidai, ‘Mimi ndiye[Yesu Kristo],’ nao watawadanganya wengi."

Tumezoea kusikia Manabii wa uongo kuliko Makristo wa Uongo. Makristo wa Uongo kwa Kiingereza ni “false Christs.” Hao ni watu wanaodai kuwa wao ni Kristo lakini wanawadanganya watu kwa mafundisho ya uongo na miujiza feki

Hizi ni baadhi ya Sifa/Tabia za Makristo wa Uongo:
  • Wanadai wao ndio Yesu aliyerudi.
  • Wanapotosha mafundisho ya Biblia
  • Wanatenda ishara za uongo kwa kutumia ujanja, miujiza feki au hata kwa kutumia nguvu za giza(mapepo) ili kuwashawishi watu wawaamini
  • Wanajiinua juu ya Kristo badala ya kuwaelekeza watu kwa Yesu. Wanatafuta kuwa na mali, umaarufu, kuheshimiwa na kuwa na “power”
Hawa ni Baadhi ya Makristo wa Uongo Waliopo katika nchi mbalimbali:
Apollo Quiboloy wa Philippines

Anadai kuwa yeye ni "Mwana wa Mungu.” Mwaka 2021, Quiboloy alishtakiwa kwa kosa la kuwalazimisha wasichana na wavulana wajihusishe na ngono na kuwatishia kwamba wasipofanya hivyo wataangamia milele!

Alan John Miller wa Australia
Anadai kuwa yeye ni Yesu aliyerudi katika mwili mwingine. Mke wake Mary Suzanne naye anadai ndiye Mariamu Magdalene(Mary Magdalene).

Inri Cristo wa Brazil
Anadai yeye ni Yesu aliyerudi mara ya pili; na ana wafuasi.

Jung Myung-seok wa Korea Kusini
Anadai yeye ni Yesu aliyerejea mara ya pili, na kwamba yupo ili kukamilisha kazi iliyokuwa haijamalizika. Jung aliwahi kupatikana na hatia ya kubaka na kutumikia kifungo cha miaka 10.

Oscar Ramiro Ortega-Hernandez wa Marekani
Ortega-Hernandez alijitaja mwenyewe kuwa ni Yesu Kristo aliyetumwa kuja kumuangamiza aliyekuwa Rais wa 44 wa Marekani kwa madai kwamba ni Mpinga Kristo. Mwaka 2011 Ortega alikamatwa kwa kosa la kupiga risasi jengo la Ikulu ya Marekani.

Yesu wa Tongaren, Kenya
Hivi majuzi, huko Kenya alijitokeza mtu anayedai kuwa yeye ni Yesu. Wakati fulani wa Pasaka, vijana wa Kenya(Gen Z) walimtaka akubali kusulibiwa msalabani kama kweli yeye ni Yesu!

Ndugu zangu, Biblia ni kitabu cha kweli. Yaliyoandikwa miaka mingi iliyopita, tunaona yakitimia waziwazi katikati yetu. Unabii huo wa kuja kwa Makristo wa Uongo nao umetimizwa. Hiyo ni dalili kuwa Yesu amekaribia kurudi. Yesu atakaporudi, atawanyakua na kuwapeleka mbinguni wale tu waliofanya mambo haya:
  • Waliotambua kuwa ni wenye dhambi (Warumi 3:23).
  • Wanaokiri na Kuamini kuwa Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zao (Warumi 5:8).
  • Waliotubu dhambi zao na kuziacha (Matendo 3:19).
  • Waliompokea Yesu mioyoni mwao kwa imani atawale maisha yao (Warumi 10:10-13).
  • Wanaoishi maisha mapya ya utakatifu katika Kristo (2 Wakorintho 5:17).
Mimi ni miongoni mwao. Wewe je?
Act swiftly before time eludes you. Do not be beguiled by the fleeting pleasures of this world, for they are merely a passing illusion. In heaven awaits an eternal and incomparable bliss.
 
yesu wa Kenya akiwa mahakamani, wakili wake alinukuliwa akisema.."Kama mteja wangu sie yesu, basi ninyi mnaomkataa mleteni huyo yesu wa kweli"..

Yale mamtu yalichora kimya kimya...

Atakaporejea. Tutamtambuaje na kumtofautisha na hao wahuni?
 
Appolo.jpg

Apollo Quiboloy claims to be the "appointed son of God" and "owner of the universe", who also says he stopped an earthquake from hitting the Philippines in 2019!
 
Wakuu, heshima zenu. Mna habari kwamba unabii huu nao tayari umetimia?
Mathayo 24:24 – "Kwa maana watatokea Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, ikiwezekana, hata walio wateule.”
Marko 13:6 – "Wengi watakuja kwa Jina langu wakidai, ‘Mimi ndiye[Yesu Kristo],’ nao watawadanganya wengi."

Tumezoea kusikia Manabii wa uongo kuliko Makristo wa Uongo. Makristo wa Uongo kwa Kiingereza ni “false Christs.” Hao ni watu wanaodai kuwa wao ni Kristo lakini wanawadanganya watu kwa mafundisho ya uongo na miujiza feki

Hizi ni baadhi ya Sifa/Tabia za Makristo wa Uongo:
  • Wanadai wao ndio Yesu aliyerudi.
  • Wanapotosha mafundisho ya Biblia
  • Wanatenda ishara za uongo kwa kutumia ujanja, miujiza feki au hata kwa kutumia nguvu za giza(mapepo) ili kuwashawishi watu wawaamini
  • Wanajiinua juu ya Kristo badala ya kuwaelekeza watu kwa Yesu. Wanatafuta kuwa na mali, umaarufu, kuheshimiwa na kuwa na “power”
Hawa ni Baadhi ya Makristo wa Uongo Waliopo katika nchi mbalimbali:
Apollo Quiboloy wa Philippines

Anadai kuwa yeye ni "Mwana wa Mungu.” Mwaka 2021, Quiboloy alishtakiwa kwa kosa la kuwalazimisha wasichana na wavulana wajihusishe na ngono na kuwatishia kwamba wasipofanya hivyo wataangamia milele!

Alan John Miller wa Australia
Anadai kuwa yeye ni Yesu aliyerudi katika mwili mwingine. Mke wake Mary Suzanne naye anadai ndiye Maria Magdalena.

Inri Cristo wa Brazil
Anadai yeye ni Yesu aliyerudi mara ya pili; na ana wafuasi.

Jung Myung-seok wa Korea Kusini
Anadai yeye ni Yesu aliyerejea mara ya pili, na kwamba yupo ili kukamilisha kazi iliyokuwa haijamalizika. Jung aliwahi kupatikana na hatia ya kubaka na kutumikia kifungo cha miaka 10.

Oscar Ramiro Ortega-Hernandez wa Marekani
Ortega-Hernandez alijitaja mwenyewe kuwa ni Yesu Kristo aliyetumwa kuja kumuangamiza aliyekuwa Rais wa 44 wa Marekani kwa madai kwamba ni Mpinga Kristo. Mwaka 2011 Ortega alikamatwa kwa kosa la kupiga risasi jengo la Ikulu ya Marekani.

Yesu wa Tongaren, Kenya
Hivi majuzi, huko Kenya alijitokeza mtu anayedai kuwa yeye ni Yesu. Wakati fulani wa Pasaka, vijana wa Kenya(Gen Z) walimtaka akubali kusulibiwa msalabani kama kweli yeye ni Yesu!

Ndugu zangu, Biblia ni kitabu cha kweli. Yaliyoandikwa miaka mingi iliyopita, tunaona yakitimia waziwazi katikati yetu. Unabii huo wa kuja kwa Makristo wa Uongo nao umetimizwa. Hiyo ni dalili kuwa Yesu amekaribia kurudi. Yesu atakaporudi, atawanyakua na kuwapeleka mbinguni wale tu waliofanya mambo haya:
  • Waliotambua kuwa ni wenye dhambi (Warumi 3:23).
  • Wanaokiri na Kuamini kuwa Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zao (Warumi 5:8).
  • Waliotubu dhambi zao na kuziacha (Matendo 3:19).
  • Waliompokea Yesu mioyoni mwao kwa imani atawale maisha yao (Warumi 10:10-13).
  • Wanaoishi maisha mapya ya utakatifu katika Kristo (2 Wakorintho 5:17).
Mimi ni miongoni mwao. Wewe je?
Act swiftly before time eludes you. Do not be beguiled by the fleeting pleasures of this world, for they are merely a passing illusion. In heaven awaits an eternal and incomparable bliss.
Allan.jpg

Australian Couple Who Say They’re Jesus and Mary
 
Whoever you are, GOD bless you ❤️
 
Hapana. Yesu hakuoa. Mary Magdalene(Mariamu Magdalene) alikuwa mmojawapo wa kinamama waliomfuata Yesu na kumhudumia(Luka 8:1-3). Biblia inasema kwamba Yesu alimtoa pepo saba(Luka 8:2, Marko 16:9).
Okay
 
Naomba kujua wapi napata maamdiko ya maisha ya YESU alipokua Egypt kabla ya kurudi Nathalet na kuaanza kuubiri ,injili
 
Maandiko yanaeleza tu katika Mathayo 2:13-15 kwamba baada ya kuzaliwa kwa Yesu, Yusufu aliambiwa na malaika aende Misri na familia yake ili kumlinda Yesu dhidi ya Herode.

Na pia katika Mathayo 2:19-23, baada ya Herode kufa, Yusufu aliambiwa na malaika arudi Israeli, lakini kwa kuwa mwana wa Herode, Arkelao, alikuwa anatawala Yudea, Yusufu alienda Nazareti.

Hakuna Maandiko mengine ya moja kwa moja katika Biblia kuhusu maisha ya Yesu akiwa Misri.

Maandiko ya Apokrifa (yasiyo sehemu ya Biblia) kama vile "The Infancy Gospel of Thomas," "The Gospel of Pseudo-Matthew" na "The Arabic Infancy Gospel" ndiyo yanayotoa hadithi za maisha yake akiwa mtoto, zikieleza miujiza aliyofanya akiwa mdogo.

Kwa mfano, hadithi ya "The Arabic Infancy Gospel" inasema kwamba Yesu na familia yake walipofika Misri, waliingia katika mji uliokuwa umejaa waabudu sanamu. Mara tu mtoto Yesu alipowekwa ndani ya mji huo, sanamu zote zilianguka chini na kuvunjika vipande vipande. Watu wa mji walishangaa na kuogopa sana, wakajiuliza ni nani huyu mtoto mwenye nguvu kubwa kiasi hiki.

Na pia kuna simulizi kwamba wakati wa safari yao, walifika sehemu ambayo haikuwa na maji. Mtoto Yesu aligusa ardhi kwa mkono wake, na chemchemi ya maji safi ilitiririka, ikawapa maji ya kunywa kwa ajili ya safari yao.

Hadithi kutoka "The Gospel of Pseudo-Matthew" inasema kwamba wakati Yesu, Mariamu na Yusufu walipokuwa wakisafiri kupitia jangwani, walihisi njaa na kiu. Wakafika kwenye mtende mrefu, wenye matunda yaliyokuwa juu sana. Mariamu alimwomba mtoto Yesu awasaidie. Yesu aliuamuru mtende uiname ili Mariamu apate matunda. Baada ya Mariamu kula matunda, Yesu akauamuru mtende urudi katika hali yake ya kawaida.

Hadithi hizo hazikubaliwi kuwa sehemu ya Maandiko Matakatifu.
 
Atakaporejea. Tutamtambuaje na kumtofautisha na hao wahuni?
Kwa sasa tunamtarajia Yesu kuja kuwanyakua watu wanaomwamini na ambao wanaishi maisha matakatifu. Atakapokuja ataishia mawinguni. Unyakuo huo utafanyika ghafla, kufumba na kufumbua, hivyo sio kila mtu atamwona Yesu wakati huo. Kitabu cha 1 Wakorintho 15:51-52 kinasema:
"Angalieni! Nawaambieni siri; hatutalala sote[hatutakufa wote], lakini sote tutabadilika, kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa tarumbeta ya mwisho; maana tarumbeta italia, na wafu watafufuliwa..."

Katika kitabu cha 1 Wathesalonike 4:16-17 tunasoma tena hivi:
"Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko wa kutisha, pamoja na sauti ya malaika mkuu, pamoja na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele."

Katika tukio hilo la unyakuo, waliookoka tu ndio watakaonyakuliwa na kwenda na Yesu mbinguni. Watu wa dunia watashangaa kwa sababu ghafla wataona kuna watu wametoweka. Watakaoachwa watabaki katika dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea tangu kuumbwa kwa ulimwengu.

Baadaye Yesu atakuja tena duniani pamoja na watakatifu wake kwa wazi na utukufu, na kila jicho litamwona. Katika Mathayo 24:30 tunasoma hivi:
"Ndipo itaonekana ishara ya Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya dunia watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na uweza na utukufu mwingi."

Kitabu cha Ufunuo 1:7 kinasema pia kwamba:
"Tazama! Anakuja na mawingu, na kila jicho litamwona, na hata wale waliomchoma; na kabila zote za dunia zitamlilia kwa uchungu. Naam, Amina."

Nimeeleza kwa muhtasari tu. Kuna matukio mengine zaidi ya hayo. Lakini tukio muhimu sana kwa sasa ni hilo la unyakuo. Ukikosa kunyakuliwa na Yesu utalia na kusaga meno.

Confess your sins, today, repent, believe in Jesus Christ, accept Him as your Lord and Savior, and live according to His Word. Siku ya unyakuo ikifika utakuwa miongoni mwao watakaonyakuliwa na kuurithi uzima wa milele. Ubarikiwe🙏
 
yesu wa Kenya akiwa mahakamani, wakili wake alinukuliwa akisema.."Kama mteja wangu sie yesu, basi ninyi mnaomkataa mleteni huyo yesu wa kweli"..

Yale mamtu yalichora kimya kimya...

Atakaporejea. Tutamtambuaje na kumtofautisha na hao wahuni?
biblia imeweka wazi kumtambua Yesu wa kweli
 
Tanzania tumekuwa na manabii na mitume wengi feki mpaka tumewazoea, bado hawajatoke makristo ya uongo tuone nao watakuja na miujiza gani wadangnye watu. Kuna mama mmoja huko mwanza yeye alitaka sifa zote anazopewa Yesu wa ukweli apewe yeye kwa jinsi anavyowafanyia waumini wake, huyo mama alikamatwa na kuwekwa mahabusu kwa muda mrefu baadae walimuachia na aliendelea na mambo yake kudanganya watu
 
Hapa Tanzania wapo manabii na mitume wanataka wao ndio wasifiwe zaidi ndio wanaponyesha magonjwa. waumini wanasema mungu wa geo kaniponya, mungu wa mwampo kanisaidia, hawasemi Yesu kaniponya, utukufu na sifa zote hawa manabii wanazichukua waonekane ni wao ndio watenda miujiza
 
Hapa Tanzania wapo manabii na mitume wanataka wao ndio wasifiwe zaidi ndio wanaponyesha magonjwa. waumini wanasema mungu wa geo kaniponya, mungu wa mwampo kanisaidia, hawasemi Yesu kaniponya, utukufu na sifa zote hawa manabii wanazichukua waonekane ni wao ndio watenda miujiza
 
Wakuu, heshima zenu. Mna habari kwamba unabii huu nao tayari umetimia?
Mathayo 24:24 – "Kwa maana watatokea Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, ikiwezekana, hata walio wateule.”
Marko 13:6 – "Wengi watakuja kwa Jina langu wakidai, ‘Mimi ndiye[Yesu Kristo],’ nao watawadanganya wengi."

Tumezoea kusikia Manabii wa uongo kuliko Makristo wa Uongo. Makristo wa Uongo kwa Kiingereza ni “false Christs.” Hao ni watu wanaodai kuwa wao ni Kristo lakini wanawadanganya watu kwa mafundisho ya uongo na miujiza feki

Hizi ni baadhi ya Sifa/Tabia za Makristo wa Uongo:
  • Wanadai wao ndio Yesu aliyerudi.
  • Wanapotosha mafundisho ya Biblia
  • Wanatenda ishara za uongo kwa kutumia ujanja, miujiza feki au hata kwa kutumia nguvu za giza(mapepo) ili kuwashawishi watu wawaamini
  • Wanajiinua juu ya Kristo badala ya kuwaelekeza watu kwa Yesu. Wanatafuta kuwa na mali, umaarufu, kuheshimiwa na kuwa na “power”
Hawa ni Baadhi ya Makristo wa Uongo Waliopo katika nchi mbalimbali:
Apollo Quiboloy wa Philippines

Anadai kuwa yeye ni "Mwana wa Mungu.” Mwaka 2021, Quiboloy alishtakiwa kwa kosa la kuwalazimisha wasichana na wavulana wajihusishe na ngono na kuwatishia kwamba wasipofanya hivyo wataangamia milele!

Alan John Miller wa Australia
Anadai kuwa yeye ni Yesu aliyerudi katika mwili mwingine. Mke wake Mary Suzanne naye anadai ndiye Mariamu Magdalene(Mary Magdalene).

Inri Cristo wa Brazil
Anadai yeye ni Yesu aliyerudi mara ya pili; na ana wafuasi.

Jung Myung-seok wa Korea Kusini
Anadai yeye ni Yesu aliyerejea mara ya pili, na kwamba yupo ili kukamilisha kazi iliyokuwa haijamalizika. Jung aliwahi kupatikana na hatia ya kubaka na kutumikia kifungo cha miaka 10.

Oscar Ramiro Ortega-Hernandez wa Marekani
Ortega-Hernandez alijitaja mwenyewe kuwa ni Yesu Kristo aliyetumwa kuja kumuangamiza aliyekuwa Rais wa 44 wa Marekani kwa madai kwamba ni Mpinga Kristo. Mwaka 2011 Ortega alikamatwa kwa kosa la kupiga risasi jengo la Ikulu ya Marekani.

Yesu wa Tongaren, Kenya
Hivi majuzi, huko Kenya alijitokeza mtu anayedai kuwa yeye ni Yesu. Wakati fulani wa Pasaka, vijana wa Kenya(Gen Z) walimtaka akubali kusulibiwa msalabani kama kweli yeye ni Yesu!

Ndugu zangu, Biblia ni kitabu cha kweli. Yaliyoandikwa miaka mingi iliyopita, tunaona yakitimia waziwazi katikati yetu. Unabii huo wa kuja kwa Makristo wa Uongo nao umetimizwa. Hiyo ni dalili kuwa Yesu amekaribia kurudi. Yesu atakaporudi, atawanyakua na kuwapeleka mbinguni wale tu waliofanya mambo haya:
  • Waliotambua kuwa ni wenye dhambi (Warumi 3:23).
  • Wanaokiri na Kuamini kuwa Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zao (Warumi 5:8).
  • Waliotubu dhambi zao na kuziacha (Matendo 3:19).
  • Waliompokea Yesu mioyoni mwao kwa imani atawale maisha yao (Warumi 10:10-13).
  • Wanaoishi maisha mapya ya utakatifu katika Kristo (2 Wakorintho 5:17).
Mimi ni miongoni mwao. Wewe je?
Act swiftly before time eludes you. Do not be beguiled by the fleeting pleasures of this world, for they are merely a passing illusion. In heaven awaits an eternal and incomparable bliss.

Mbona hao wa hapo kwenu wamejaa halafu huwasemi. Kazi kuwasema wengine tu
 
Back
Top Bottom