Changamoto katika maisha ni nyingi sana, si ajabu huyo uliye achana naye ni mungu amekuepusha na matatizo ambayo ungeweza kuja kukutana nayo mbeleni, usiteseke kwa sababu umeachana na mwanaume bali fikiria ni maisha ya aina gani yanyoweza kukupa furaha hapa duniani. Kumbuka kupendani ni hisia za ndani za mtu, unaweza ukampenda asiye kupenda au unaweza kupendwa na usiye mpenda. Ni vizuri kujipa likizo ya ku-analyze ulikosea wapi, inawezekana ulimpenda asiye kupenda au vinginevyo. Lakini usijipe kifungu mwenyewe cha miaka mitano ukidhani baada ya hapo utampata umpendae, usipo fakiniwa baada ya 5yrs nadhani utaweza kuwa na wakati mgumu sana. Mimi nakushauri kama una mpango wa kupenda tena basi uliza moyo wako unataka nini then ukimpata uliyeridhika nae tumia taratibu zilizopo kuingia kwenye ndoa halali bila kujali kipengele cha miaka ya likizo.
Note: Usitumie ngono kama silaha ya kumfanya mwaume akuoe au kuimaarisha mahusiano, mwanume atakuoa kama moyo wake umekuridhia. Fanya ngono kama unataka kuburudisha mwili vinginevyo achana nayo.