Hebu sikieni ninavyowaza!!

Hebu sikieni ninavyowaza!!

Kwa mtaji huo nakushauri umalizie kifungo chako maana katikati hapa si salama kabisa kwako. Tafuta jambo la kukuweka bize na wala si kutafuta ushauri wa kuahirisha kifungo

Asante RF, na asante zaidi kwa sababu umenielewa nachotaka/tafuta

Basi tu niliona sina sababu ya kumwamini mwanaume,
Najifikiria kwa nini nisipende bwanaaaaaaaaaaaaaaa!!!!
Kwa hiyo kutokana na mahekima niliyoyapata hapa, nimefungua mlango, na likizo imeishia hapo kwenye miaka miwili.
Lakini mapenzi ya Mungu yatimie zaidi!!!!!!!
:clap2::cheer2::welcome::violin:
 
Say something nataka kuongeza.......ooppss lakini LD atakuwa ameishaacha kuwaza na amepata solution ngoja nimsubirie nione

Ha ha ha TF unasubiria nini mtu angu!! Nimeshapata PM za kutosha na nyingine zinaendelea kuingia. Nadhani kuanzia Ijumaa na shortlist, wiki ijayo Intaviu itaanza, kila anayetuma atajibiwa lakini sio wote watapewa nafasi ya kuendelea. Na uzuri vigezo ninavyo mimi mwenyewe wala hakuna anayejua natumia vigezo gani kwa hiyo tuma PM usije ukalalamika mzee!! Hakuna upwa katika hili.
 
Life is too short make the most of it!

Usijitese weka mawasiliano na watu utapata tu.

kwa ushauri zaidi ni PM
 
Ha ha ha TF unasubiria nini mtu angu!! Nimeshapata PM za kutosha na nyingine zinaendelea kuingia. Nadhani kuanzia Ijumaa na shortlist, wiki ijayo Intaviu itaanza, kila anayetuma atajibiwa lakini sio wote watapewa nafasi ya kuendelea. Na uzuri vigezo ninavyo mimi mwenyewe wala hakuna anayejua natumia vigezo gani kwa hiyo tuma PM usije ukalalamika mzee!! Hakuna upwa katika hili.
PM yangu nitakutumia VIA MOBILE ili iwe tofauti na wengine hapo natumaini kwenye PM za VIA MOBILE nitakuwa peke yangu tu kwahiyo hakuna haja ya wewe kunifanyia assessment yaani wewe ni ku-approve moja kwa moja
 
Mwenzenu nilivunjwa moyo miaka miwili iliyopita, Tangu moyo ulivyovunjika nimekuwa nikimuomba Mungu aniponye na nina Imani ameniponya kabisa, manake najiona sina kinyongo, wala uchungu na huyo heart breaker, na ninachomshukuru Mungu zaidi nina furaha na Amani, na maisha yanaendelea vizuri.

Pamoja na hivo ninamshukuru Mungu kwa sababu amenisamehe dhambi niliyokuwa nimeitenda, kwa sababu nilijidai ninampenda sana huyo mtu kuliko hata Mungu, nikampa vyote, nafsi, roho na mwili. Wakati mwingine hata muda wa kwenda kuabudu ulipungua kwa kumpa huyo heart breaker muda mwingi zaidi.

Baada ya tukio hilo,niliamua kujipa likizo ya kumpenda mwanaume, yani nikaziba madirisha yote ya kumkaribisha mwanaume moyoni mwangu.
Siwachukii lakini nimejipa likizo kwa muda wa miaka mitano hivi, na sasa huu ni mwaka wa pili, ina maana bado miaka mitatu.

Je uamuzi wangu wa kujipa likizo ni sahihi?
Najiona ninaweza kuendelea na likizo hadi miaka mitatu iliyobakia iishe, je ni kweli au
naidanganya nafsi yangu.

Angalizo Marufuku kunitania Broken Heart!! Umesikia GY, Asprin, TF, Askofu na Teamo T, bila kumsahau Bigirita. Mjukuu mtiifu umesikia!! na wewe St. RR.
Umepote ukweli wanaume ndivyo tulivyoumbwa hatuzidiani kifikira!!hata baada ya miaka mitano utakaye kutana naye atakuwa kama uliyekuwa naye miaka mitano iliyopita!!!

mi naona unajidanganya sababu kwa jinsi nnavyojua lov inakuja yenyewe labda ujiweke mbali na watu, ninacho kiona hujaonana na mtu atakayeteka moyo wako, ukimuona unasisimka, ukiongea nae unapata raha, hapo ndipo utakapo amini miaka 3 ni kifungo cha maisha.
Huyu alidhani kazaliwa naye na akitongozwa barabarani au ofisini nakwingineko alikuwa anawajibu nina boyfriend Kwa mbwembwe na majigambo mengi kumbe mlikuwa wawili bila kujijua ambaye akuwana namajigambo ndo kabaki naye pole!Ila leo kayaleta majuto hapa JF!!
 
Umepote ukweli wanaume ndivyo tulivyoumbwa hatuzidiani kifikira!!hata baada ya miaka mitano utakaye kutana naye atakuwa kama uliyekuwa naye miaka mitano iliyopita!!!

Huyu alidhani kazaliwa naye na akitongozwa barabarani au ofisini nakwingineko alikuwa anawajibu nina boyfriend Kwa mbwembwe na majigambo mengi kumbe mlikuwa wawili bila kujijua ambaye akuwana namajigambo ndo kabaki naye pole!Ila leo kayaleta majuto hapa JF!!

Umesema kweli kabisa, na hivyo ndivyo nilivyokuwa. Lakini namshukuru Mungu kwa hii shule manake nimebadika sana sasa hivi.
 
hata mimi ilishawahi ntokea nikajipa likizo ya mwaka kutotaka kumsikiliza mwanaume.Hiyo yako ni ndefu mno maisha mafupi ya nini ujikoseshe raha?
nadhani hiyo miwili imetosha sasa anza kusikiliza kidogokidogo.

ANGALIZO:usimkaribie mtu asiye na hofu ya mungu, kuna wakaka kibao wanakwaya/wainjilisti makanisani kama vipi anza kujifua kuima nadhani hili halitamchukiza MUNGU manake unamtaka kondoo wake kwa nia safi.

kwani wanakwaya ni watakatifu sana??
usimdanganye mwenzio:decision:
 
Kila kitu ni uamuzi LD, kama umeamua utaweza, miaka mitano siyo mingi ukiwa unaishi na amani....................
fuata nafsi yako. kupumzika hasa baada ya kuvunjika moyo ni kuzuri sana ingawa wadada wengi hawataki kufanya hivyo, na matokeo yake unajikuta unahama kwa mkaka mmoja baada ya mwingine maana kila mwanaume unakuwa humwamini.
My advice to u LD, take as much break as you can, hata ikifika miaka 10, so long as you are happy.

We! acha kumdanganya mwenzio...
 
Shauri yako!!! Upo tayari kukaguliwa kwanza?? Kuna mkaguzi wa wajukuu wa kiume hapa?? Naomba ajitokezo mara moja.
Hii si kwa ajili yangu. Hizo nukuu zisikuumize kichwa pia. Ni kwa ajili ya wanajamvi wote
 
hapana likizo inatosha,wapo wanaojuwa thamani ya mwanamke,omba mungu atakufunulia huyo ubavu wako,hyo likizo sio suluhisho maana stil itakapoisha unaweza ukadondokea kwa kimeo kingine,ukajilaumu maisha naona hapo utaamua kuwa sista kabisa kama ni mkristo.anyway poleeeee:mullet:
 
Labda ukaishi kwenye kisiwa ambapo wakoa hawakuoni vinginevyo ulivyofikiri is wrong to yuou heart!!!!
 
Mabibi na mabwana nawashukueu nyoteee kwa michamgo yenu, na mafundisho yenu na ushauri wenu.
Kwa kweli Mungu awabariki, na muwe na moyo huo huo, wakutoa maoni na maushauri kwa jamii.
Ninayo Imani mimi sio wakwanza wala wapili kupitia jaribu kama hili. Ninachomshukuru Mungu, anajua ni kwa nini,
anatupisha katika njia ambayo, wakati mwingine hatukuitaka.
Ni ili pia tumtafute yeye zaidi.

Mbarikiwe mpaka mshangae!!!!
 
Okey LD usijali sasa ingia mtaani kutana na watu tofautitofauti pia usimsahau mungu. ujumbe soma zaburi 118 ndio kama hapo chini
 
Jamanie, nilidhani kwenda Kariakoo ni lazima upitie ubungo then Moro road kumbe sio. Ni ushamba wangu tu! Kumbe hata dirisha ni mlango ikibidi? Kumbe pia mwenye nyumba aweza kuwa mpangaji? Dereva kuwa abiria? Without no further clarification, through this topic I would like to salute all women for being so clever, yet so prone to some circumstances
 
Discuss
 
Back
Top Bottom