mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Je ni waalimu wangapi kwa mwaka wanaingia kwenye soko la ajira kutafuta ajira wakiwa na certificate, diploma na degree? Je ni kwenye sekta ya afya kwa kada mbalimbali ni wangapi wanaingia sokoni kwa mwaka kusaka ajira wakiwa na certificate, diploma, degree nk. Hali kadhalika kwa wanasheria, wahandisi, wahasibu, maafisa utumishi, na kadhalika na kadhalika!!
Kwa kukadiria kwangu kwa kada mbali mbali wakiwa kwenye ngazi mbali mbali, kuna wafanyakazi watarajiwa takriban 200,000 kwa mwaka wanaingia kwenye kinyang'anyiro cha kusaka ajira!! Kwa kuwa ajira kwenye utumishi wa umma zilisimama kabisa kuanzia mwaka 2015, kuna mlundikano wa wasaka kazi zaidi ya milioni moja na nusu wa miaka hiyo wakati kila mwaka wanazidi kuongezeka!! Kwa hiyo hizo nafasi za ajira takriban 13,000 katika sekta ya elimu na afya ni kidogo mno japo tarakimu inaonekana kuwa kubwa!!
Ndiyo maana ili kuwatendea haki sekretarieti ya ajira huita watu wengi sana kwenye usaili hata kwa nafasi moja tu, ili walau wajisikie kuwa wameitwa kwenye usaili kuliko kutoitwa kabisa! Ndiyo maana anayepata ajira lazima amshukuru sana Mungu na afanye kazi kwa bidii!!
Je, suluhisho la kudumu ni lipi?