Hebu tudadavue ukubwa wa tatizo la ajira nchini: Ni wangapi wanaingia kwenye soko la kutafuta ajira kwa mwaka? Uwezo wa kuajiri (serikali & private)?

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Je ni waalimu wangapi kwa mwaka wanaingia kwenye soko la ajira kutafuta ajira wakiwa na certificate, diploma na degree? Je ni kwenye sekta ya afya kwa kada mbalimbali ni wangapi wanaingia sokoni kwa mwaka kusaka ajira wakiwa na certificate, diploma, degree nk. Hali kadhalika kwa wanasheria, wahandisi, wahasibu, maafisa utumishi, na kadhalika na kadhalika!!

Kwa kukadiria kwangu kwa kada mbali mbali wakiwa kwenye ngazi mbali mbali, kuna wafanyakazi watarajiwa takriban 200,000 kwa mwaka wanaingia kwenye kinyang'anyiro cha kusaka ajira!! Kwa kuwa ajira kwenye utumishi wa umma zilisimama kabisa kuanzia mwaka 2015, kuna mlundikano wa wasaka kazi zaidi ya milioni moja na nusu wa miaka hiyo wakati kila mwaka wanazidi kuongezeka!! Kwa hiyo hizo nafasi za ajira takriban 13,000 katika sekta ya elimu na afya ni kidogo mno japo tarakimu inaonekana kuwa kubwa!!

Ndiyo maana ili kuwatendea haki sekretarieti ya ajira huita watu wengi sana kwenye usaili hata kwa nafasi moja tu, ili walau wajisikie kuwa wameitwa kwenye usaili kuliko kutoitwa kabisa! Ndiyo maana anayepata ajira lazima amshukuru sana Mungu na afanye kazi kwa bidii!!

Je, suluhisho la kudumu ni lipi?
 
Ajira sio haki ya waliosoma tuu hata ambao hawakusoma wanahaki ya kuajiriwa.
Serikali lazima iboreshe mifumo ya Watu kujiajiri hasa kwenye ishu za Kodi ili kutoa fursa Kwa Vijana wanaotaka kujiajiri.

Nilisikia kuwa Serikali Ilitangaza kuwa Kijana anayeanza kujiajiri atapewa Grace period ya Mwaka mmoja asilipe Kodi, ikiwa ni kweli basi itakuwa NI UAMUZI mzuri Sana.
Na Vijana wanachopaswa ni kuanzisha biashara na kuzisajili ili Kupata fursa hiyo.

Hata hivyo mchakato wa kusajili biashara au Kampuni inapaswa iwe rahisi ili kutowakatisha tamaa Vijana chipukizi
 
1. Tubadili kabisa fikra zetu na utamaduni wetu. Fikra ni #1.

2. Tubadili mwelekeo wa elimu yetu. Maana elimu ya sasa (kwa miaka mingi tu) haiendani na MAHITAJI ya soko.
Mimi nimekuwa kwenye biashara na soko la ajira muda mrefu sasa. Watoto wamefundishwa kufaulu mitahani! Wamekaririshwa tu vitu ambavyo zaidi ya 70% havina uhusiano na maisha yao, kazi wala havimjengei skills na maarifa wala ubunifu wakutatua matatizo yao/jamii, achilia mbali kazi.
Kwa ufupi graduates wetu wana uwezo mdogo sana kwa kila hali. Ni long story. Inasikitisha sana. Niishie hapo.

3. Mfumo wa elimu na mitaala husika vibadilishwe completely. Mfano iwe; kuanzia darasa la tano watoto wetu wafundishwe ujasiriamali na wengine ufundi kweli kweli (practicals). Sekondari waendelezwe hivyo mpaka vyuo na VTCs. Tufute A Level kwa muundo wa sasa, tuweke High/Specialized Level 2-3yrs after Lower/Ordinary Level. Mtoto yeyote atayehitimu kwenye hizo level 2 ataweza kujiajiri na anaajirika ndani na nje ya nchi kwa level yake.
Nayo ni mada ndefu pia.

4. Hizo hela za HESLB, TASAF, UFISADI nk zitumike kuwapa mitaji, kujenga mazingira, masoko, nk

5. Kuweko na open industrial forums/platforms za kuwasaidia na kuwanoa vijana ktk tasnia husika.
Hayo ni kwa ufupi.

:::To be honest ukinipa mimi VETA zote nchini na bajeti ya miaka 3-4; ndani ya miaka 5 tutakuwa tumepunguza tatizo la ajira kwa zaidi ya asilimia 50%. Na baada ya miaka 10 Tanzania itakuwa mfano wa kuiga Africa. Nazungmzia practical facts/realities na sio nadharia au siasa hapo.
 
Hizo ni siasa ambazo hutumiwa na wanasiasa wetu kujipatia umaarafu kwenye majukwaa ya siasa kama kweli wanania ya kuwapatia 'grace period' wanaojiajiri wangepeleka bungeni muswada wa kubadili sheria mbalimbali za kodi kuliko kuhubiri majukwaani halafu tukija mtaani hali tofauti na kinachohubiriwa hawana nia ya kweli maana wao na familia zao hayawagusi haya washajitengenezea njia za kutafuna keki ya taifa bila jasho chida inabaki kwa Watoto wa matabaka ya chini na kati kuhangaika na ajira ikiwa pamoja na kupambana kwenye kujiajiri.
 
Huwezi tengeneza ajira kama hakuna mabadiliko ya tekinolojia. Wingi wa Ajira na Kujiajiri zote hutegemea mabadiliko hayo ya tekinolojia. Nchi lazima iwe katika mabadiliko ya kitehama ndipo elimu au ufundi utabadilika kuwa ajira. Wasomi hawafiki milioni 5, katika nchi ya watu milioni 60, lakini hao milioni 5 hawazioni fursa katika raia milioni 60. Tatizo ni nchi bado ipo katika nyakati za ujima, wakati dunia ipo katika tehama.
 
Nafikiri tatizo kubwa linaanzia kwenye mfumo wetu wa Elimu iko na shida maana kama vijana wengi wanamaliza vyuo lakini mawazo yao hasa yako kwenye kuajiriwa kibaya zaidi hata uwaambie baadhi yao unao uwezo wa kuwapatia mitaji watakwambia uwaonyeshe na biashara ya kufanya.
 
Lazima Serikali iweke mazingira mazuri ya vijana kujiajiri, its not option hii ni LAZIMA. Kujiajiri si kitu cha mchezo na hili ndilo kosa kubwa sana wanalofanya viongozi wetu sijui kwa makusudi ama kwa kutojua.

Kwa mfano, Je leo hii Serikali imeweka mazingira gani rafiki ya huyu Kijana Graduate kuweza kujiajiri kwenye ujasiliamali mdogo mdogo kama Kilimo, Ufugaji, Ufundi n.k Mazingira ni pamoja na mfumo wa Elimu yetu je unaendana na hali ya ajira nchini na Duniani kote.

Huwezi toka chuo ambapo umesoma kwa mkopo, wazazi wako wapo hoi kwa maskini kijijini huko with high expectation about you, yet kiongozi wa miaka 68 mtunga sera amekaa kwenye kiyoyozi na kiti cha kuzunguka anakuambia eti ukajiajiri, this is not fair.
 
Ni jinsi gani tunaweza kuongeza ajira!?
Tubadili sheria mbalimbali zenye kuweka ushawishi wa ustawi wa sekta binafsi maana yake wengi watashawishika kujiajiri kwa kufungua biashara/makampuni, biashara ndogo/kubwa na ajira zitaongezeka mara dufu. Lakini kingine ni kubadili mitaala ya Elimu yetu iendane na mabadiliko mbalimbali mfano kwa namna ilivyo ni ngumu kwa mtu aliyemaliza elimu yake kupata fursa ya kujiajiri maana haimuandai kuwa hivyo zaidi ya kusubira kuajiriwa.
 
Sahihi kabisa mazingira lazıma yaandaliwe yawe rafiki kiasi kwamba iwe rahisi zaidi kujiajiri maana mazingira yanaruhusu
 
Tubadili sheria mbalimbali zenye kuweka ushawishi wa ustawi wa sekta binafsi maana yake wengi watashawishika kujiajiri kwa kufungua biashara/makampuni, biashara ndogo/kubwa na ajira zitaongezeka mara dufu. Lakini kingine ni kubadili mitaala ya Elimu yetu iendane na mabadiliko mbalimbali mfano kwa namna ilivyo ni ngumu kwa mtu aliyemaliza elimu yake kupata fursa ya kujiajiri maana haimuandai kuwa hivyo zaidi ya kusubira kuajiriwa.

Makini hii kijereshi
Thanks

Bureaucracy bado ipo juu mno
Serikali ianze kuangalia kuwekeza kwenye utaalamu wa watu wake ili wafungue makampuni na waajiri watu wengi zaidi
Regulators ambao ni serikali huduma zao mbovu kama kusajili kampuni tuu inaweza chukua miezi -brela
TRA- system iko down muda wote
Halmashauri ndio usiseme
TIC wamekomaa na wawekezaji wa nje huku wakiwakatisha tamaa wazawa
Halafu customer care ya watendaji mbovu mnooo huwezi amini ndio hao wanaoomba salary increments may mosi🙄
 
Asante sana kuondoa huo urasimu sasa ni vita kubwa umeongea kila kitu cha ukweli Brela, tra, TIC angalau halmashauri sahivi kupitia mfumo mpya tausi leseni zinatoka haraka na mianya ya rushwa na upotevu wa mapato inazibwa
 
1. Tubadili kabisa fikra zetu na utamaduni wetu. Fikra ni #1.

2. Tubadili mwelekeo wa elimu yetu. Maana elimu ya sasa (kwa miaka mingi tu) haiendani na MAHITAJI ya soko.
Mimi nimekuwa kwenye biashara na soko la ajira muda mrefu sasa. Watoto wamefundishwa kufaulu mitahani! Wamekaririshwa tu vitu ambavyo zaidi ya 70% havina uhusiano na maisha yao, kazi wala havimjengei skills na maarifa wala ubunifu wakutatua matatizo yao/jamii, achilia mbali kazi.
Kwa ufupi graduates wetu wana uwezo mdogo sana kwa kila hali. Ni long story. Inasikitisha sana. Niishie hapo.

3. Mfumo wa elimu na mitaala husika vibadilishwe completely. Mfano iwe; kuanzia darasa la tano watoto wetu wafundishwe ujasiriamali na wengine ufundi kweli kweli (practicals). Sekondari waendelezwe hivyo mpaka vyuo na VTCs. Tufute A Level kwa muundo wa sasa, tuweke High/Specialized Level 2-3yrs after Lower/Ordinary Level. Mtoto yeyote atayehitimu kwenye hizo level 2 ataweza kujiajiri na anaajirika ndani na nje ya nchi kwa level yake.
Nayo ni mada ndefu pia.

4. Hizo hela za HESLB, TASAF, UFISADI nk zitumike kuwapa mitaji, kujenga mazingira, masoko, nk

5. Kuweko na open industrial forums/platforms za kuwasaidia na kuwanoa vijana ktk tasnia husika.
Hayo ni kwa ufupi.

:::To be honest ukinipa mimi VETA zote nchini na bajeti ya miaka 3-4; ndani ya miaka 5 tutakuwa tumepunguza tatizo la ajira kwa zaidi ya asilimia 50%. Na baada ya miaka 10 Tanzania itakuwa mfano wa kuiga Africa. Nazungmzia practical facts/realities na sio nadharia au siasa hapo.
Safi sana, indeed you're a great thinker. Mimi nilishangaa tunaimba Tanzania ya viwanda au kilimo kwanza wakati mtoto mpaka anamalizia form 6 hana technical skill yoyote.
 
iyo milion kumi ya magoli ya umeme katika ni mkopo wa vijana kujiajiri zaid ya 10 kama kikundi
 
Safi sana, indeed you're a great thinker. Mimi nilishangaa tunaimba Tanzania ya viwanda au kilimo kwanza wakati mtoto mpaka anamalizia form 6 hana technical skill yoyote.
Asante mkuu, pamoja sana.

Niko tayari kuchangia, kushiriki na kusaidia nchi yangu kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.
 
Back
Top Bottom