Hebu tukumbushane machungu ya timu zetu siku tulipojutia kwenda uwanjani au Vibanda Umiza

Kuna mwaka nimeusahau mtanikumbusha. Yanga alikuwa anaongoza ligi kwa point 2 zaidi ya simba, mtibwa (kama sijakosea) alikuwa nafasi ya pili kamzidi simba point 1, simba akiwa anashika nafasi ya tatu na kila mtu amebakiwa na mechi moja zote zinachezwa siku moja. Ubingwa ulikuwa kati ya yanga au mtibwa simba hakuwa kwenye hesabu za ubingwa. Siku hiyo RTD hawakutangaza mechi yoyote kwa hiyo kila mtu alikuwa anasubiri saa mbili kasorobo asikie yanga au mtibwa atangazwe bingwa. Mbili kasoro mtangazaji anaanza kwa kusema SIMBA BINGWAAA.
 
🤣🤣🤣 alooo
 
Mi ni shabiki wa Manchester united, nakumbuka mechi na bayern Munchen 2010, Roho iliniuma sanaaaa, robben alitufanya kitu kibaya Sana, ile red card haikuwa ya Halali kabisa..
Screenshot_20210101-195127_1.jpg
 
Mimi mechi ya simba na stella abdijan mwaka 1993, iliniumiza sana ,kilichoniumiza nilikuwa mdogo,nilimuona mama analia sana,simba alipigwa 2 au 3 kama sijakosea.kuna magoli alifunga jamaa aliiitwa boli zozo.

Nyingine ni mechi ya senegal na uturuki robo fainali kombe la dunia 2002.goli la hakan sukur liliniumiza sana ,
 
Back
Top Bottom