Hebu tukumbushane machungu ya timu zetu siku tulipojutia kwenda uwanjani au Vibanda Umiza

Hebu tukumbushane machungu ya timu zetu siku tulipojutia kwenda uwanjani au Vibanda Umiza

Mechi ya kwanza nafikiri ndio Rooney aliumia ya marudiano akalazimika kuchomwa sindano ili acheze na kwa mchango wake tuliongoza 3 bila hadi apo anaanza kuchechemea ikabidi atolewe bayern wakaamka sasa
Mechi ya kwanza ndiyo alichomwa sindano
 
Man u alihitaji city apigwe au atoke sare, sasa hadi dakika ya 90 city kapigwa mbili moja, dakika za nyongeza city kasawazisha na kapiga latatu mtu mzima Kun kafanya yake na ndio game ya mwisho epl
Nilijisikia uchungu sana ile siku. Mario Balotelli hatakaa asahaulike kamwe nyau yule
 
Mimi mechi ya simba na stella abdijan mwaka 1993, iliniumiza sana ,kilichoniumiza nilikuwa mdogo,nilimuona mama analia sana,simba alipigwa 2 au 3 kama sijakosea.kuna magoli alifunga jamaa aliiitwa boli zozo.

Nyingine ni mechi ya senegal na uturuki robo fainali kombe la dunia 2002.goli la hakan sukur liliniumiza sana ,
Simba tulikula 2-0 siku ile. Ni mwaka 1993
 
Liverpool 4 Barca 0
Hii mechi mashabiki wa Barca hawataki kuisikia kabisa. Meza ilipinduliwa kibabe mnoooo. Mikeka ilochanika vibaya sana, kwa wale wanaopenda ku bet. Spurs akapindiua meza ya Ajax 😀 😀 😀 😀
 
Kuna siku Yanga hadi mapumziko alikua anaongoza goli 3 dhidi ya simba nkajua zile 5 leo zinarudi mechi inaisha 3 tatu, ilinuima sana hii mechi.
Watu walizimia sana taifa ile siku. Naikumbuka sana
 
Man u vs barca ( uefa final).Xavi, Iniesta, Messi dah ilikuwa mateso kwa Man u kwa dakika 80 maana Man u walicheza dakika 10 tu.
hii mechi iliniumiza sana,mesi na iniesta ni washenzi hawana huruma kabisa,David villa naye alipiga goli Kali sana.......yan mpaka Alex fergie alikuwa anatetemeka vle nkaona hapa catalunya wametuweza aiseee
 
Hakuna siku niliumia kama siku JT wa Chelsea kutukosesha UCL kwa kukosa penati ya mwisho dhidi ya Man U ilikuwa 2008 mjini Moscow.

Saivi tungekuwa tunahesabu 2 UCL CUPS

Hebu tiririka mechi gani ilikuuma sana.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Hakuna siku niliumia kama siku JT wa Chelsea kutukosesha UCL kwa kukosa penati ya mwisho dhidi ya Man U ilikuwa 2008 mjini Moscow.

Saivi tungekuwa tunahesabu 2 UCL CUPS

Hebu tiririka mechi gani ilikuuma sana.
basi kama kuna siku niliichukia real madrid ni pale real ramos anamvuja mkono salah...karius anatuchoma bale anatutungua benzema anatutungua[emoji23][emoji23] aise ile game sitasahau
 
Kuna mwaka nimeusahau mtanikumbusha. Yanga alikuwa anaongoza ligi kwa point 2 zaidi ya simba, mtibwa (kama sijakosea) alikuwa nafasi ya pili kamzidi simba point 1, simba akiwa anashika nafasi ya tatu na kila mtu amebakiwa na mechi moja zote zinachezwa siku moja. Ubingwa ulikuwa kati ya yanga au mtibwa simba hakuwa kwenye hesabu za ubingwa. Siku hiyo RTD hawakutangaza mechi yoyote kwa hiyo kila mtu alikuwa anasubiri saa mbili kasorobo asikie yanga au mtibwa atangazwe bingwa. Mbili kasoro mtangazaji anaanza kwa kusema SIMBA BINGWAAA.
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
basi kama kuna siku niliichukia real madrid ni pale real ramos anamvuja mkono salah...karius anatuchoma bale anatutungua benzema anatutungua[emoji23][emoji23] aise ile game sitasahau
Sisi teamZizzou hii siku tulifurahi sana.
Hala Madrid✋🖐
 
Back
Top Bottom