Hebu tukumbushane uongo ambao Watanzania tuliwahi kudanganywa

Hebu tukumbushane uongo ambao Watanzania tuliwahi kudanganywa

Serikali ya Magufuli ilitutaka tuwachangie wahanga wa tetemeko Bukoba ambao nyumba zao zimebomoka, hawana chakula Wala nguo. Tukachanga, mwisho wa siku michango yetu ikachukuliwa eti ikaboreshe Miundombinu.
Ule ulikuwa Ni zaidi ya utapeli na dhuluma
Tangu tutapeliwe michango yetu ya wahanga wa tetemeko la ardhi huko Kagera,nimeacha kuchangia kitu chochote kinachosimamiwa na mwana CCM.
 
Katika uongo mkubwa kupita mauongo yote nadhani huu ni mkubwa kupita kiasi, eti gasi ya Mtwara ingeinua uchumi wa bongo "drastically"!!!!🤣🤣.

leo cha ajabu hata Wapinzani wote wapo kimya kama kwamba fikra zao ni "blind folded" juu ya suala la gesi ya Mtwara.

sio Wapinzani wala Chama tawala wote hawazungumzii kabisa juu ya gesi ya Mtwara.

kama Wtz tumelogwa, tumepigwa bumbuwazi,!!!!🤣🤣
Sisi tuna flow na vibe mkuu yani ni sawa tuko kwenye dance tunaenda na flow la DJ sasa hivi tunaambiwa stiglers gorge itamaliza mahitaji ya umeme, same as tulivyoambiwa kwenye gas.
 
Balali Kafariki na kuzikwa Marikani, kweli bila hata picha wala muwakilishi kutoka Tanzania, hii inasababisha Mungu kukata mishipa ya viwanda vya uongo ghafla.
 
Kuna watanzania wanaambiwa Magu kalipa madeni yote hatudaiwi hata senti
Mkuu nasikia ndani ya miaka hii mitano deni limeongezeka mara dufu. Hii 40 Tr sijui kweli?!
CAG wakutuambia hayupo day!!
 
Ndege ya aina hii ni special sana na katika Africa hakuna nchi iliyowahi kuinunua.
 
Kuna uongo mwingi tuliwahi kuongopewa na watanzania weangi wakauamini hadi watu wakubwa na tuliodhani wanajua mambonao wakaukumbatia. Mimi ninaanza na huu.

1. Kipindi cha Jakaya Mrisho Kikwete akiwa rais, nakumbuka magazeti kadhaa na redio kadhaa ziliwahi ripoti kuwa kuna mapacha wawili ni watanzania ila wamesoma Marekani mmoja ni daktari bingwa na mwingine ni mfanyakazi wa NASA.

Eti kwamba walikuwa amerudi Tanzania, kwa likizo fupi ambapo huyo daktari bingwa alikuwa kafanya operesheni wagonjwa takribani 8 na wote wanaendela vizuri hapa Tanzania, wakati huyo mwanaanga wa NASA ni kati ya wanaanga wa kwanza kutembelea sayari ya Mars. Habari hiyo nakumbuka ilishikiliwa bango PJ na Gerald Hando wakati wote wako Clouds. Wakadai hawataki hojiwa na vyombo vya habari mpaka wakutane na rais.

Mimi nilianza kuwa na shaka na hao mapacha baada ya kusikia tu kuwa eti mmoja wao kashafika Mars, wkati mpaka muda huo na mpaka leo hakuna binadamu ambaye kakanyaga sayari ya Mars zaidi ya vyombo kama Rovers. Na nadhani Kikwete alikuwa mjanja hakuwahi kuwaalika ikulu.

2. Project Kubwa ya kujenga Kigamboni. Nakumbuka kuanzia mwaka 2009 mpaka 2014 nadhani, kulikuwa na video zinazoonyesha jinsi Kigamboni itakavyojengwa na wamarekani, viwanja kigamboni vikawa havishikiki kigamboni ikawa lulu. Zile video zilikuwa zinavutia sana. Jamaa yangu aliuziwa maeneo kule kwa pesa ndefu sana lakini sijajua hii story iliishia wapi, na viwanja vikaanguka thamani hadi alipotaka kuuza hakuweza kuuza hata robo ya pesa aliyotoa.

Nitarudi kuongeza
TANZANIA YA VIWANDA.
 
1.Milioni 50 kila kijiji
2.Tanzania itakua Dona kantri
3.Acacia wakitulipa kila mtanzania atamiliki Noah
4.Magufuli ni Yesu.
Hiyo ya nne imenichekesha sana [emoji23],[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Watu waongo ni balaa, eti mbowe alipigwa na machangudoa bar hadi wakamvunja mguu akasingizia kavamiwa na majambazi
 
Back
Top Bottom