kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
- Thread starter
- #21
Wafanya vurugu walipewa targets kubwa sana za kuzifikia, hata sijui walipewa njia mkakati na nyenzo gani za kutumia ili kufikia malengo. Nadhani aliyewapa hizo targets alikuwa mjinga sana asiyejali maisha ya wengine na kichaa kidogo.Usiseme kwa kutumia nguvu kubwa. Sema kwa kuwashoot na kuwaua .... hatukuona mahali police wakizuia vurugu kwa njia za kawaida na kuonekana wamezidiwa nguvu na raia. Hatukuona mahali police ikikamata hao waandamanaji .... au ndiyo walikuwa wanazuia nyunyunyu na nywi nywi nywi kwa kutumia vitu venye ncha kali .... kwa shoot watu mgongoni wakati wanakimbia kama yule mama wa Arusha.... Acheni kutetea na kuhalalisha UUAJI uliofanyika kwa kusukumia lawama kwa akina LISSU na Heche. Video zipo watu wanaandamana na kuimba mbele ya magari ya jeshi bila vurugu zozote.
Hata hivyo nadhani alifanya SWOT analysis akagundua yafuatayo:
S - Strenghs: Alidhani vijana wote nchini wanamuunga mkono na wanakerwa na mfumo. Pia kuna nguvu nyingine ya wanaotaka Tanganyika, wafanyabiashara, watu wa dini, taasisi za nje, diaspora, fedha za kutosha kutoka nje ya nchi na ndani ya nchi.
W - Weakness: Hawana silaha, hivyo lazima wapore vituo wazipate za moto wachanganye na viberiti vyao.
O- Opportunities: Mpasuko ndani ya CCM, askari wengi kuwa bize na uchaguzi nchi nzima, vyombo vya habari vya kimataifa, diaspora, taasisi za kimataifa kama EU, kuwaunga mkono, internet na uwepo wa ICC.
T- Threats: CCM kuwa karibu na majeshi, SADC, EA, migogoro mikubwa na muhimu kwenye mataifa mengine kama Ukraine, Gaza, Iran, DRC, Sudan, Ethiopia, Yemen, Lebanon inayovuta attention ya dunia.
Hapa walijua kabisa wataumizwa na kuuliwa wengi. Lakini nadhani walipata assurance kutoka baadhi ya wanajeshi kuwa watakuwa nyuma yao.
Hata hivyo Taifa ni kubwa kuliko wao. Hesabu zikaenda kombo.