HECHE anangojea hukumu kwa kukosea, anaingilia hukumu.

Wafanya vurugu walipewa targets kubwa sana za kuzifikia, hata sijui walipewa njia mkakati na nyenzo gani za kutumia ili kufikia malengo. Nadhani aliyewapa hizo targets alikuwa mjinga sana asiyejali maisha ya wengine na kichaa kidogo.

Hata hivyo nadhani alifanya SWOT analysis akagundua yafuatayo:

S - Strenghs: Alidhani vijana wote nchini wanamuunga mkono na wanakerwa na mfumo. Pia kuna nguvu nyingine ya wanaotaka Tanganyika, wafanyabiashara, watu wa dini, taasisi za nje, diaspora, fedha za kutosha kutoka nje ya nchi na ndani ya nchi.

W - Weakness: Hawana silaha, hivyo lazima wapore vituo wazipate za moto wachanganye na viberiti vyao.

O- Opportunities: Mpasuko ndani ya CCM, askari wengi kuwa bize na uchaguzi nchi nzima, vyombo vya habari vya kimataifa, diaspora, taasisi za kimataifa kama EU, kuwaunga mkono, internet na uwepo wa ICC.

T- Threats: CCM kuwa karibu na majeshi, SADC, EA, migogoro mikubwa na muhimu kwenye mataifa mengine kama Ukraine, Gaza, Iran, DRC, Sudan, Ethiopia, Yemen, Lebanon inayovuta attention ya dunia.

Hapa walijua kabisa wataumizwa na kuuliwa wengi. Lakini nadhani walipata assurance kutoka baadhi ya wanajeshi kuwa watakuwa nyuma yao.

Hata hivyo Taifa ni kubwa kuliko wao. Hesabu zikaenda kombo.
 
Heche hawezi kukaa kimya kusubiri hukumu ya mahakama za maagizo.
 
Kichwa maji mtu akisikiliza hizi hekaya zako anaweza akadhani unaongea kitu cha maana. Yaani ni kama vile unaona hatuujui ukweli, ila tunausubiri kuujua ukweli toka kwako na majizi ya uchaguzi. Ungetuambia ni wapi kura 31m Samia kazipata, wakati vituo havikuwa na hao wapiga kura, tungeona unaongea kitu cha maana.
 

 

Attachments

  • Screenshot_20261005_192436_Instagram.jpg
    99.8 KB · Views: 5
Kavutata,Una ugomvi binafsi na Heche ama Chadema kwani haueleweki!
 
Mimi kazi yangu ni kukusogezea facts ambazo zipo tu lakini wewe hujui kama zipo, ni juu yako kuchukua au kuacha.

Ni mtu mjinga tu ataamini kama uchaguzi ule ulivurugika eti kwa vurugu za sehemu chache kama zile zilizoanza saa 10 jioni. Ni mjinga tu ambae alikuwa hafuatilii nyomi za kampeni za CCM.

Tofauti ya CCM na chadema ni kwamba CCM wanahakikisha kuwa kila mwanaCCM anapiga kura, wajumbe wa nyumba kumi wana kazi ya kuwatafutia kura wagombea wao wote asubuhi na mapema kabisa. Chadema ina wavutabangi wengi ambao siku ya uchaguzi hawaendi kupiga kura.

Wapigakura wengi nchi hii ni wakinamama ambao hawaipendi chadema. Bahati nzuri uchaguzi wa 2025 mgombea Urais alikuwa mwanamke mwenzao.

Wewe unatumia hisia kusema badala ya facts
 

Papropaganda uchurwara.
 
Narudia tena ww ni kichwa maji, usidhani siku ya kupiga kura tulikuwa nje ya nchi. Tulikuwa hapa hapa, tumeona kwa macho yetu vituo havikuwa na wapiga kura. Tuna ndugu na jamaa waliokuwa wasimamizi kwenye vituo vya kura wanakiri hakukuwa na wapiga kura. Mimi binafsi nilizunguka zaidi ya vituo vitano vya kupigia kura kuanzia saa 3 hadi saa 5 na nusu asubuhi, hakukuwa na wapiga kura zaidi ya mawakala. Kama zamani mlizoea kuhadaa watu, safari hii cdm kususia uchaguzi wa kishenzi kumewaumbua.

Nyomi ya ccm ilikuwa ni ya kutengenzezwa sehemu muuaji Samia alipokuwa, na fedha za umma ndio zilizokuwa zinatumika kumbemba mgombea wa ccm. Huu ni ukweli mchungu kwa kila mwanaccm. Vua nguo, piga kelele, jilize huwezi kubadili ukweli huu.
 
Kavutata,Una ugomvi binafsi na Heche ama Chadema kwani haueleweki!
HEche ni rafiki yangu, sina ugomvi nae. Anajitafutia riziki kupitia siasa za harakati huku akijua kwamba ni ngumu sana kuitisa serikali. Ugomvi wangu nae ni kushiriki mpango ambao utasababisha vifo kwa watanzania wenzake na kuharibu miundombinu katika nchi masikini kabisa inayotegemea misaada na mikopo.
Kusema Lissu na Heche hawana uhusiano na vurugu za Oct29 ni dharau kwa watanzania waliopoteza wapendwa wao na mali zao.

Heche tumshauri awe na kiasi, asipuuze ushauri wazazi wake, ndugu na jamaa kama kuna kitu wamemshauri au kumuonya. Samia ni mwanamke ndiyo, lakini ni Rais wetu, mkuu wetu wa nchi na Amirijeshi Mkuu wa majeshi yote ya Tanzania. Hata kama hataki lakini lazima amheshimu.
 
Nchi haiendeshwi kwa hisia. Hamna takwimu za kuwafanya UN, EU, ICC na dunia wasikitike na kutoa machozi. Ndio maana wabunge wa mabunge ya dunia wanafanyia mkutano wao hapa Arusha, Tanzania. Kuonyesha kuwa nyie ni wahuni na waseramavi wanaoihadaa dunia. Wazungu wana akili na ma satellites kibao huko angani wanajua kila kitu mlichokifanya kabla, wakati na baada ya oct29.
 
Nchi haiendeshwi kwa hisia. Hamna takwimu za kuwafanya UN, EU, ICC na dunia wasikitike na kutoa machozi. Ndio maana wabunge wa mabunge ya dunia wanafanyia mkutano wao hapa Arusha, Tanzania. Kuonyesha kuwa nyie ni wahuni na waseramavi.
Ukweli wetu hauhitaji endorsment ya UN, EU, ICC nk, tuna ukweli tunaoweza kuutumia popote maana ni ushahidi wa kweli . Ushahidi wetu sio wa kuridhisha taasisi yoyote maana ni ukweli usiohitaji proof ya yoyote.

Huo mkutano unafanyika hapa nchini maana ni mkutano usio na tija kwa sasa. Acha huo, hata ule wa UN kwa sasa hauna tija yoyote. Cdm wanajiamini sana kwakuwa wanasimamia ukweli, bila kujali nani anauona. Akitoka mtu anayetaka ukweli, basi ukweli upo wazi. Hapo ndio cdm wanapotambia, na ukweli huo umewaweka huru. Mtatengeneza matume ya kupindisha ukweli, lakini waliosimama kwenye ukweli wataendelea kutamba.
 
Safi, ficheni migongo yenu lakini kabla ya kuianza safari ya gologota.
 
We jamaa mbona uchaguzi haukufanyika kwa miji mikubwaaa au upo ulayaa..kula walihesabu vp??
Kwa mfano nilipo na nilishuhudia kwa macho ni kama watu wanne hv au watano wa MWANZO ndio walipiga kula wengine woote kilichafukaaa mabomu watu walikimbia nk..Sasa natokea yanakuja kinyume chake






Hakukuwa na uchaguzi mwaka Jana wtz ni waoga weng hawalwenda
 
Mahakama iko huru kuamua kwa haki, hailazimishwi lakini haitishwi wala kutishiwa kutoka upande wowote.
Kwahiyo wewe unajiona mjanja na mwerevu sana kuliko Rostam Aziz?

Ama upo kibaruani mkono uende kinywani?

Don’t insult our intelligence.
 
Mimi nilipiga kura comfortably kabisa, kwenye eneo hakukuwa na foleni ndefu ingawa watu walikuwa wengi sana. Hii iliwezekana kwakuwa kuliwekwa maturubai mengi sana katika kituo kimoja hivyo ndani ya saa moja tu watu wengi sana waliweza kupiga kura. Sijui walijuaje kama jioni fujo zitazuka. Mtu akisema watu hawakupiga kura naona propaganda tu za kitoto maana mimi na familia yangu ya watu 4 pamoja na majirani zangu wote tulipiga kura na kurudi nyumbani salama kama.

Hata hivyo, kama ni kweli watu hawakupiga kura, wale waliokatwa vidole vyenye wino waliwapata wapi?
Acheni propaganda za hisia. Ndio maana ICC walitupilia mbali upuuzi wenu. Mnadhani wazungu ni maboya kama nyiye?
 
mlisusa au mliweka mpira kwapani?
UKisusa wenzio wala, na wamekula kweli. Tunaomba msuse tena next time.
 
Aziz ndiyo nani? Mtu asiyependa kufuata taratibu hapendi mamlaka za udhibiti kama polisi, mahakama, TRA, tbs, etc.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…