Salaam!
Hayo yamesemwa Leo na kamanda John Heche makamo mkt wa CHADEMA taifa akiwa kahama.
Yaani ikiwa hujaelewa ni hivi, mtanzania yeyote awe boda boda, machinga, muuza mchicha, mkulima ,mfanyabiasha ,mlemavu nk nk, ukifikisha miaka 60,utalipwa pensheni ya uzeeni sababu ulishiriki kuijenga nchi yako kwa miaka yote kabla ya kuzeeka.
Ikumbukwe CHADEMA ya John Heche pia iliahidi kupiga marufuku michezo ya kubahatisha,kamari Ili kuondoa ujinga wa kudhani MAISHA ni bahati ilhal SI kweli.
Sasa Ili ahadi hiyo itimie, Kila mtanzania na aunge mkono hoja ya NRNE Ili kuzuia uchaguzi batili usifanyike kwa maandamano Hadi pale reforms zitapofanyika kupata Tume huru ya uchaguzi.
Usiache kufuatilia mikutano hii ya ukombozi wa nchi yetu.
Mungu Mbariki John Heche,
Mungu ibariki CHADEMA,
MUNGU ibariki nchi YANGU nzuri niipendayo Tanzania 🇹🇿
Karibuni 🙏