Pre GE2025 Heche: Huyu mama hawezi kushinda uchaguzi Lissu akiwa mgombea na sisi tukiongoza chama sababu ni mwanamke, Mzanzibar na hana hoja

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Heche ni kilaza. Uwezo wake wa kujenga hoja ni mdogo mno. Hapo kamshambulia personally Mama Samia kitu ambacho sio sawa. Dhambi ya ubaguzi itawatafuna sana CHADEMA. Nawapongeza waliovujisha hii clip kwa sababu shetani Heche naye karopoka kuwa watu wavujishe maongezi ya mwenyekiti wake.
 
Usiwe mjinga kiasi hicho. Ni watanganyika wangapi wameiongoza Zanzibar kwa kuwa ni marais wa jamhuri ya muungano? Acha kuwaza kama nyumbu😀😀
Unajichekesha kama shoga ambae amekalia mashine huku ukiwa hujui kwamba Rais wa Muungano hana mamalaka yoyote yale Zanzibar, Zanzibar ina rais wake kwa mambo yake ambayo sio ya muungano.
 
Akupe solutions?Unamlipa?
 
Watanzania wana haki kikatiba ya kutoa maoni yao juu ya yeyote na chochote kuhusu nchi yetu na nchi nyingine duniani. Wewe ni nani hata uthubutu kuwanyooshea kidole watanzania wanaotumia haki yao kikatiba?
So you think hence katumia busara?
 
Hawana haki ya kutoa maoni ya kibaguzi na yanayo hatarisha umoja wa kitaifa kama wapi Rais anatoka, mwanamke n.k.
Wewe unaona ni sawa nchi moja kuwa na marais wawili ? Uliona wapi ujinga kama huu duniani kote au hata tangu enzi za tawala za kifalme uliona wapi eneo moja kuwa na wafalme wawili ?
Na wote wanatoka nchi moja ? Ni udhaifu mkubwa sana wa kikatiba.

Na hata waliotinga katiba wangejua kuwa hata wakubwa wanakufa wasingeweka kifungu cha katiba cha makamu wa Rais kushika madaraka moja kwa moja endapo Rais atafariki . Hii ndiyo inayowezekana ikatumika kuleta hujuma kwa yule anayekua madarakani .Inaweza ikatumika kumalizana kama makamu atakua na Tamaa . Ni wazi kama haitabadilika itaendelea kuwa hivyo maana kwa sasa ni wazi kuwa urais ni kama umungu kwa katiba iliyopo . Rais wa nchi za kiafrika kwa miaka miwili tu madarakani anaweza kuwa bilionea kama mfanyabiashara wa karne moja . Sasa hali hii inaleta kila mtu kuwa na tamaa ya ama kubwa Rais au Rafiki yake kuwa Rais ili kunufaika binafsi.

Katiba ilipaswa kuwa makamu anakaimu tu kwa muda wa miezi 6 na kisha unaitishwa uchaguzi na sio kushika fulu pawa wakati hakuchaguliwa kwa kura na hajawahi kuweka maono yake juu ya nchi zaidi ya kuteuliwa kama mgombea mwenza .

Mfano Yule Makamu wa leo sidhani kama aliwahi hata kujihusisha na siasa kabla ya kuteuliwa tu na kuwa Mbunge na kisha waziri .Sasa ni makamu . Kesho unasikia amekua Rais bila kupigiwa kura wala kushindanishwa na satu wenye ndoto hizo tangu utotoni kama akina Januari , Nape , Mwigulu, Jafo, Makonda , Bashe , Mwakyembe Wasira , Sumaye , Majaliwa , Makongoro n.k

Hawa wa kupewa tu wanaweza wakafanya chochote kufilisi na kuhujumu nchi kwa manufaa ya wachache. Na pia wetu kama hawa wanakua na hofu na chuki kubwa sana ndio maana wanatengeneza makundi ya kidini na kikabila kupata sapoti kubwa ili kujihami . Na makundi ya kidini na kikabila ni makundi yanayotumika mara nyingi kuua watu maana ni ya watu wenye vinasaba na itikadi za kuona wanaomtetea ndugu yao .
Kiongozi anayeingia madarakani kwa kura na maono anakua ni kiongozi wa kitaifa ndio. Hata teuzi zake zinakuwa za kitaifa na zenye sera sio itikadi za kidini kikabila .

Tunao mfano wa watu waliotia nia kwa muda na kujipanga kwa sera na maono kama Kikwete na Mkapa . Hawa hawakua na mambo ya kijinga kijinga wa Udini na ukabila. Wakizingatia Utaifa kwanza na hawakua na hofu na vyombo vyao vya dola .

Kwa sasa tangu alipoibuka JPM kwa kuteuliwa kati ya mgogoro nchi imekua ikiongozwa hofu kama serikali iliyopatikana kwa mapinduzi . Hawana imani na hata vyombo vyao vya kiusalama . Huu ni udhaifu . Inakua kama Museveni anaweka mwanawe kuwa CDF lakini ni kwa sababu ya mazingira ya Uganda na namna alivyoingia madarakani .
 
KUMBE HUYU HECHE NI BOGUS KIASI HIKI, HAFAI KABISA, NI PUNGUANI, UWEZO WAKE NA UFAHAMU WAKE NI MDOGO SANA.
 
Huyu mkurya aliye na wajomba na baba wadogo Kenya, aliyesoma SAUT kwa kulipiwa na Barrick North Mara na mkopo wa bodi ya elimu anajiona msafi kuliko watanzania wengine.

Unaweza ukawa na Hoja ila ulipoanza tu kusema ..... Huyu Mkurya ..... hapo ndipo Umeharibu kwani unaonekana una Chuki kubwa na Wakurya halafu Wewe ni Mbinafsi na Mkabila hivyo hufai hata Kusikilizwa.
 
Watanzania wana haki kikatiba ya kutoa maoni yao juu ya yeyote na chochote kuhusu nchi yetu na nchi nyingine duniani. Wewe ni nani hata uthubutu kuwanyooshea kidole watanzania wanaotumia haki yao kikatiba?
Kwani kaongea uongo siyo mzanzibar? watulie
 
Watu wana haki kutoa maoni yao kama yanavunja sheria basi wafikishwe mahakamani.
Mengine hayahitaji kupoteza muda adhimu wa mahakama

Lakini Kwa kusema hivyo siungi mkono kabisa utekaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…