Heche kumtunishia misuli msajili wa vyama – analazimisha CHADEMA kufutwa?

Heche kumtunishia misuli msajili wa vyama – analazimisha CHADEMA kufutwa?

Hivi pilipili, chumvi au maji ya limao kimoja wapo kikiingia kwenye kidonda kibichi kipi kina leta maumivu zaidi? Anyway nahisi Kuna wanasiasa wanamlengo wa kiarakati, na kukubalika kwao kwa kupokelewa vzr na wananchi ndio inatumika kama fulsa kudhorotesha juhudi za chama kwa kutumia ajenda ficho ambayo imeshindwa kutafsiliwa na wananchi wenye Nia thabiti na chama Chao! Ni swala la muda watakuja kupata majibu mchezo unaochezwa maana wenye wenye akiri ndio wabeba maono ya chama Chao ila mwananchi anafata upepo kulingana na ukali wa maisha yake!
 
Huyo msajili ni Mungu wa kuogopwa na kutenda miujiza? Au chawa tu wa sisiemu?
 
Katiba ya nani vile? Aliyewaita nyumbu aendelee kupewa maua yake. Kinachofuatwa ni sheria ya vyama vya siasa we bwege
Sijakutukana wala kukukoti. Tuheshimiane na ushike heshima vizur kabla ya athari.
 
Mlimnyima Lissu hela za Matibabu vipi alikufa? Magufuli alizuia ruzuku kwa miaka 5 vipi Chadema ilikufa?

Si mmemwambia Msajili akifute Chadema? Akifute sasa lengo lenu litimie. Chadema haiwezi kupiga magoti kwenu nyie wezi wa kodi za Wananchi na Madhalimu.
Hawa Jamaa ni Wapumbavu mnooooo
 
mkuu chadema ni kama mkia wa kenge unavyoukata ndo unazidi kurefuka na anakuwa na nguvu zaidi, ukiuacha unarefuka unafika kikomo na kenge anakuwa mzito hawezi tena kukimbia, ukiifuta cdm ndo inakuwa na nguvu kwani hautajua kiongozi ni nani na hautaweza kuisimamia, ni kama genge linalopiga mwizi ukomo wake ni mwizi afe kwani halina kiongozi
Chadema ndio matumaini ya watanzania siku ikifutwa lazima tutagawana mbao za ikulu na ofisi zote za Uma. Maana tusio kuwa na vyama tutakuwa wengi na wote tutajitetea kwa njia zote.
 

Attachments

  • Screenshot_2025-05-28-12-10-03-68_1c337646f29875672b5a61192b9010f9.jpg
    Screenshot_2025-05-28-12-10-03-68_1c337646f29875672b5a61192b9010f9.jpg
    446.8 KB · Views: 14
Imesomeka.......tukumbuke haki huinua Taifa!!!!!
Haki gani ya kuwadhalilisha waliokuwa viongozi wenu na kuwapa majina mabaya!? Mnatweza na kuwaona ni dhalili sio?? Hapo ndio mnaona mnajenga chama chenu sio??
 
Jamani hatuna hata mia ya kuitisha mkutano mkuu, labda Mbowe aingilie kati
 
Vyama vya siasa nchini vinaendeshwa kwa mujibu wa sheria, na Msajili wa Vyama vya Siasa ana jukumu la kuhakikisha kuwa sheria hizo zinatekelezwa ipasavyo. Hakuna chama kilicho juu ya sheria. Lakini ni wazi kwamba baadhi ya viongozi wa juu ndani ya CHADEMA, akiwemo John Heche, wameamua kwa makusudi kuvuruga misingi ya kisheria. Kwa hatua zake, Heche anaonekana ama kwa kujua au kutokujua, kukiongoza chama kwenye anguko la aibu

1. Ruzuku Kusitishwa kwa Makusudi
Ruzuku ya serikali ni haki ya msingi kwa chama kilichosajiliwa kisheria. Hata hivyo, CHADEMA imejiondoa kwenye haki hiyo baada ya kukaidi maagizo halali ya Msajili kuhusu uthibitisho wa viongozi walioteuliwa na Baraza Kuu la Januari 2025. Badala ya kuitisha vikao halali na kuwasiliana na msajili kama chama kinavyotakiwa, Heche na uongozi wake wamejifanya kuwa jeuri. Matokeo yake ni hasara kubwa kwa chama, sidhani kama "Tone Tone" itawezesha shughuli zote. Hii ni hujuma ya wazi kabisa.

2. Kugomea Kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi
Kwa miaka yote, CHADEMA imekuwa sehemu ya mchakato wa kisiasa kwa kusaini kanuni za maadili ya uchaguzi. Lakini Heche na Lissu waliamua kukaidi hatua hii muhimu, hawakwenda kusaini wala kutuma mwakilishi. Kitendo hiki kinakiuka taratibu na kimelenga kukinyima uhalali wa kisheria Chama katika uchaguzi ujao. Huu ni usaliti uliovishwa joho la upinzani.

3. Kushindwa Kudhibiti Migogoro ya Ndani
Baada ya uchaguzi wa ndani, migogoro mingi imeota mizizi, kuondoka kwa viongozi waandamizi kumeendelea kukidhoofisha chama. Uongozi wa Heche na Lissu haujachukua hatua yoyote kupoza makovu ya kisiasa. Badala yake, wamekuwa watazamaji wa mgawanyiko huo huku wakijifanya hawaoni shida yoyote. Migogoro hii sasa imefanya mikoa mingi kukosa viongozi. Hali ni mbaya zaidi maeneo kama Kigoma, Kanda ya Kati na Kaskazini.

4. Kueneza Chuki Dhidi ya Wengine Na kujiona Shujaa
Katika hali ya kushangaza, Heche amekuwa mstari wa mbele katika mijadala ya wazi kuwapaka matope viongozi wenzake, akiwemo Mwenyekiti mstaafu Freeman Mbowe. Hili limezua mvutano mkubwa ndani ya chama, hasa kwa vijana na makada wa muda mrefu. Mtu anayeeneza chuki dhidi ya viongozi wastaafu au viongozi wengine wa chama chake si kiongozi bali ni msaliti, eti yeye anajiona shujaa!

Vitendo vya John Heche si tu vinaathiri CHADEMA kisiasa, bali vitampa Msajili wa vyama vya siasa sababu ya kuhoji uhalali wa chadema. Kama wanachama na wapenzi wa demokrasia, hatuwezi kukaa kimya tukishuhudia chama kinachodai kuwa mbadala kikichukuliwa mateka na watu wenye ajenda binafsi. Heche anapaswa kuwajibishwa kabla CHADEMA haijafutwa kisheria.
Je, mtasema hamkuambiwa? Kazi kwenu.
Ujeuri na kiburi Cha kina Heche
 
Mbona siku za hivi karibuni ID za member zimekua nyingi...yani watu wamejiunga sana mwaka huu...na wana hoja fulani hivi za mrengo wa kijani wengi
Id za ccm kuelekea uchaguzi mkuu, unakumbuka zile sa kina Bia yetu kuelekea uchaguzi mkuu 2020.
 
Jamani hatuna hata mia ya kuitisha mkutano mkuu, labda Mbowe aingilie kati
Hatuna hata mia ya kuitisha mikutano ya kikhanithi. Hao akina Mchome mliokuwa mnatumia kuharibu chama mmewaagiza wahamie chauma.
 
Mbona siku za hivi karibuni ID za member zimekua nyingi...yani watu wamejiunga sana mwaka huu...na wana hoja fulani hivi za mrengo wa kijani wengi

Hao huwa ni member ambao hawajulikani, mkuu.
 
Mbona siku za hivi karibuni ID za member zimekua nyingi...yani watu wamejiunga sana mwaka huu...na wana hoja fulani hivi za mrengo wa kijani wengi
Ni jukwaa huru, unaweza tupa trend ya watu kujiunga jf kwa miaka mitano iliyopita?
 
Back
Top Bottom