Heche kumtunishia misuli msajili wa vyama – analazimisha CHADEMA kufutwa?

Vyama vya siasa nchini vinaendeshwa kwa mujibu wa sheria, na Msajili wa Vyama vya Siasa ana jukumu la kuhakikisha kuwa sheria hizo zinatekelezwa ipasavyo. Hakuna chama kilicho juu ya sheria. Lakini ni wazi kwamba baadhi ya viongozi wa juu ndani ya CHADEMA, akiwemo John Heche, wameamua kwa makusudi kuvuruga misingi ya kisheria. Kwa hatua zake, Heche anaonekana ama kwa kujua au kutokujua, kukiongoza chama kwenye anguko la aibu

1. Ruzuku Kusitishwa kwa Makusudi
Ruzuku ya serikali ni haki ya msingi kwa chama kilichosajiliwa kisheria. Hata hivyo, CHADEMA imejiondoa kwenye haki hiyo baada ya kukaidi maagizo halali ya Msajili kuhusu uthibitisho wa viongozi walioteuliwa na Baraza Kuu la Januari 2025. Badala ya kuitisha vikao halali na kuwasiliana na msajili kama chama kinavyotakiwa, Heche na uongozi wake wamejifanya kuwa jeuri. Matokeo yake ni hasara kubwa kwa chama, sidhani kama "Tone Tone" itawezesha shughuli zote. Hii ni hujuma ya wazi kabisa.

2. Kugomea Kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi
Kwa miaka yote, CHADEMA imekuwa sehemu ya mchakato wa kisiasa kwa kusaini kanuni za maadili ya uchaguzi. Lakini Heche na Lissu waliamua kukaidi hatua hii muhimu, hawakwenda kusaini wala kutuma mwakilishi. Kitendo hiki kinakiuka taratibu na kimelenga kukinyima uhalali wa kisheria Chama katika uchaguzi ujao. Huu ni usaliti uliovishwa joho la upinzani.

3. Kushindwa Kudhibiti Migogoro ya Ndani
Baada ya uchaguzi wa ndani, migogoro mingi imeota mizizi, kuondoka kwa viongozi waandamizi kumeendelea kukidhoofisha chama. Uongozi wa Heche na Lissu haujachukua hatua yoyote kupoza makovu ya kisiasa. Badala yake, wamekuwa watazamaji wa mgawanyiko huo huku wakijifanya hawaoni shida yoyote. Migogoro hii sasa imefanya mikoa mingi kukosa viongozi. Hali ni mbaya zaidi maeneo kama Kigoma, Kanda ya Kati na Kaskazini.

4. Kueneza Chuki Dhidi ya Wengine Na kujiona Shujaa
Katika hali ya kushangaza, Heche amekuwa mstari wa mbele katika mijadala ya wazi kuwapaka matope viongozi wenzake, akiwemo Mwenyekiti mstaafu Freeman Mbowe. Hili limezua mvutano mkubwa ndani ya chama, hasa kwa vijana na makada wa muda mrefu. Mtu anayeeneza chuki dhidi ya viongozi wastaafu au viongozi wengine wa chama chake si kiongozi bali ni msaliti, eti yeye anajiona shujaa!

Vitendo vya John Heche si tu vinaathiri CHADEMA kisiasa, bali vitampa Msajili wa vyama vya siasa sababu ya kuhoji uhalali wa chadema. Kama wanachama na wapenzi wa demokrasia, hatuwezi kukaa kimya tukishuhudia chama kinachodai kuwa mbadala kikichukuliwa mateka na watu wenye ajenda binafsi. Heche anapaswa kuwajibishwa kabla CHADEMA haijafutwa kisheria.
Je, mtasema hamkuambiwa? Kazi kwenu.
1. Mwanamke kutoka Kizimkazi,unaijua sheria hata moja ya msajili wa vyama vya siasa kada wa CCM Jaji Mtungi ya kupokea,kusikiliza,kuhukumu na kufuta uongozi wa CHADEMA ?
2. Mwanamke kutoka Kizimkazi,Msingi wa kufuta uongozi na kuzuia ruzuku kwa pamoja kwa sheria ya vyama kif.18(6) je, Baraza la wadhamini ambao ni wenye chama nao wamefutwa ?
NO REFORMS NO ELECTION 2025 !
 
Hatuna hata mia ya kuitisha mikutano ya kikhanithi. Hao akina Mchome mliokuwa mnatumia kuharibu chama mmewaagiza wahamie chauma.
Maria Sarungi amechelewesha malipo ya mwezi huu, wazungu hawajaachia hela?
 
Vyama vya siasa nchini vinaendeshwa kwa mujibu wa sheria, na Msajili wa Vyama vya Siasa ana jukumu la kuhakikisha kuwa sheria hizo zinatekelezwa ipasavyo. Hakuna chama kilicho juu ya sheria. Lakini ni wazi kwamba baadhi ya viongozi wa juu ndani ya CHADEMA,

28 May 2025
Dodoma, Tanzania

Mbatia amgaragaza Msajili wa Vyama vya Siasa, na pia aibwaga NCCR Mageuzi mahakamani​

Soma zaidi jinsi Msajili anavyotumika :
 
Vyama vya siasa nchini vinaendeshwa kwa mujibu wa sheria, na Msajili wa Vyama vya Siasa ana jukumu la kuhakikisha kuwa sheria hizo zinatekelezwa ipasavyo. Hakuna chama kilicho juu ya sheria. Lakini ni wazi kwamba baadhi ya viongozi wa juu ndani ya CHADEMA, akiwemo John Heche, wameamua kwa makusudi kuvuruga misingi ya kisheria. Kwa hatua zake, Heche anaonekana ama kwa kujua au kutokujua, kukiongoza chama kwenye anguko la aibu

1. Ruzuku Kusitishwa kwa Makusudi
Ruzuku ya serikali ni haki ya msingi kwa chama kilichosajiliwa kisheria. Hata hivyo, CHADEMA imejiondoa kwenye haki hiyo baada ya kukaidi maagizo halali ya Msajili kuhusu uthibitisho wa viongozi walioteuliwa na Baraza Kuu la Januari 2025. Badala ya kuitisha vikao halali na kuwasiliana na msajili kama chama kinavyotakiwa, Heche na uongozi wake wamejifanya kuwa jeuri. Matokeo yake ni hasara kubwa kwa chama, sidhani kama "Tone Tone" itawezesha shughuli zote. Hii ni hujuma ya wazi kabisa.

2. Kugomea Kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi
Kwa miaka yote, CHADEMA imekuwa sehemu ya mchakato wa kisiasa kwa kusaini kanuni za maadili ya uchaguzi. Lakini Heche na Lissu waliamua kukaidi hatua hii muhimu, hawakwenda kusaini wala kutuma mwakilishi. Kitendo hiki kinakiuka taratibu na kimelenga kukinyima uhalali wa kisheria Chama katika uchaguzi ujao. Huu ni usaliti uliovishwa joho la upinzani.

3. Kushindwa Kudhibiti Migogoro ya Ndani
Baada ya uchaguzi wa ndani, migogoro mingi imeota mizizi, kuondoka kwa viongozi waandamizi kumeendelea kukidhoofisha chama. Uongozi wa Heche na Lissu haujachukua hatua yoyote kupoza makovu ya kisiasa. Badala yake, wamekuwa watazamaji wa mgawanyiko huo huku wakijifanya hawaoni shida yoyote. Migogoro hii sasa imefanya mikoa mingi kukosa viongozi. Hali ni mbaya zaidi maeneo kama Kigoma, Kanda ya Kati na Kaskazini.

4. Kueneza Chuki Dhidi ya Wengine Na kujiona Shujaa
Katika hali ya kushangaza, Heche amekuwa mstari wa mbele katika mijadala ya wazi kuwapaka matope viongozi wenzake, akiwemo Mwenyekiti mstaafu Freeman Mbowe. Hili limezua mvutano mkubwa ndani ya chama, hasa kwa vijana na makada wa muda mrefu. Mtu anayeeneza chuki dhidi ya viongozi wastaafu au viongozi wengine wa chama chake si kiongozi bali ni msaliti, eti yeye anajiona shujaa!

Vitendo vya John Heche si tu vinaathiri CHADEMA kisiasa, bali vitampa Msajili wa vyama vya siasa sababu ya kuhoji uhalali wa chadema. Kama wanachama na wapenzi wa demokrasia, hatuwezi kukaa kimya tukishuhudia chama kinachodai kuwa mbadala kikichukuliwa mateka na watu wenye ajenda binafsi. Heche anapaswa kuwajibishwa kabla CHADEMA haijafutwa kisheria.
Je, mtasema hamkuambiwa? Kazi kwenu.
Heche anaweza kuwa ni "Project" ya Deep State.
 
Back
Top Bottom