Pre GE2025 Heche: Posho siku moja tu Bungeni tulikuwa tunalipwa laki nne, halafu Mwalimu kwa mwezi unamlipa laki 4!

Pre GE2025 Heche: Posho siku moja tu Bungeni tulikuwa tunalipwa laki nne, halafu Mwalimu kwa mwezi unamlipa laki 4!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kaongea ukweli
giphy.gif
 
Ukisikia hazina za taifa ,, ndiyo watu kama hawa ,, mimi sina cha kuongezea zaidi ya kumuombea kwa mungu amzidishie rehema na baraka tele katika kizazi chake chote kwa kuwa muwazi,,, kwakuwa mtu asiyepindisha pindisha mambo
 
Mliambiwa hawa ni wanaharakasti hamuelewi..

Kwenye office , Head of Sales analipwa Mil 18, na dereva analipwa laki 3 , hapo kuna unyonyaji mmoja ampunguzie mwingine?

Nilifikiri kwa mtu mwenye hadhi yake angeongelea Muundo wa Bunge na namna gani wanaweza punguza vikao na safari zisizo na tija yeye analinganisha mishahara?

Duniani kote watu wanalipwa kutokana na Value na Impact anayoweza sababisha kwenye jamii..

Kalangabhao
 
Mnafiki tu huyu.Angelalamika kwamba posho ni kubwa ipunguzwe akiwa mjengoni angekuwa na credibility. Kuwa nje ya mjengo halafu ulalamike ni unafiki tu na hadaa.
Alilalamikia sana hiyo tofauti ya mapato hata akiwa bungeni. Ila chama pendwa kiliweka pamba masikioni.

Amandla...
 
Mliambiwa hawa ni wanaharakasti hamuelewi..

Kwenye office , Head of Sales analipwa Mil 18, na dereva analipwa laki 3 , hapo kuna unyonyaji mmoja ampunguzie mwingine?

Nilifikiri kwa mtu mwenye hadhi yake angeongelea Muundo wa Bunge na namna gani wanaweza punguza vikao na safari zisizo na tija yeye analinganisha mishahara?

Duniani kote watu wanalipwa kutokana na Value na Impact anayoweza sababisha kwenye jamii..

Kalangabhao
Tuambie value ya wabunge hawa wagonga meza na kusinzia? wana utalaam gani kumzidi mwalimu aliyesoma na sifa ya mbunge ni kujua kusoma na kuandika basi lakini dereva anayemwendesha lazima awe na cheti cha F4?
 
Sijaelewa unafiki wake uko wapi, kuwasemea walimu au kuvujisha posho za bunge?
Ni unafiki kutomjua mnafiki. Jibu swali tokea lini Heche alikataa posho akiwa mbunge.Ni rahisi kusema kwamba kiatu hakibani kikiwa kwenye mguu wa mwingine.
Heche angesema hili alilosema akiwa mbunge na kuwa mfano wa kukataa posho.
Pamoja na kwamba posho hizo ni kubwa na zinatakiwa kufanyiwa review lakini Heche hana moral authority ya kuzungumzia swala hili kwani yeye amepata faida kubwa kwenye huu mfumo akiwa mbunge.
 
Back
Top Bottom