Pre GE2025 Heche: Posho siku moja tu Bungeni tulikuwa tunalipwa laki nne, halafu Mwalimu kwa mwezi unamlipa laki 4!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Heche hii ni hoja ya kitoto sababu,hukuwahi kupinga hizo laki 4 kwa siku na ulipokea.
Sasa simamia vitu vingin,ni hoja dhaifu sana kwa mwenyekiti.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Ni unafiki kutomjua mnafiki. Jibu swali tokea lini Heche alikataa posho akiwa mbunge.Ni rahisi kusema kwamba kiatu hakibani kikiwa kwenye mguu wa mwingine.
Heche angesema hili alilosema akiwa mbunge na kuwa mfano wa kukataa posho.
Pamoja na kwamba posho hizo ni kubwa na zinatakiwa kufanyiwa review lakini Heche hana moral authority ya kuzungumzia swala hili kwani yeye amepata faida kubwa kwenye huu mfumo akiwa mbunge.
So issue ni time ya kusema? Walioko bungeni kwa sasa kuna ambae amesema?
 
Mliambiwa hawa ni wanaharakasti hamuelewi..

Kwenye office , Head of Sales analipwa Mil 18, na dereva analipwa laki 3 , hapo kuna unyonyaji mmoja ampunguzie mwingine?

Nilifikiri kwa mtu mwenye hadhi yake angeongelea Muundo wa Bunge na namna gani wanaweza punguza vikao na safari zisizo na tija yeye analinganisha mishahara?

Duniani kote watu wanalipwa kutokana na Value na Impact anayoweza sababisha kwenye jamii..

Kalangabhao
Kwa hiyo ndiyo mjilipe pesa zote hizo,afu walimu ambao ndiyo wenye impact kubwa katika jamii kuliko hawo wabunge mnawanyonga hivyo.
 
Alilalamikia sana hiyo tofauti ya mapato hata akiwa bungeni. Ila chama pendwa kiliweka pamba masikioni.

Amandla...
With due respect angeenda a step further na kukataa kupokea kama solidarity na wengine wenye kipato cha chini.Hii huwa inafanyika kwa wanaoamini wanachokipigania sio maneno matupu.
 
Mliambiwa hawa ni wanaharakasti hamuelewi..

Kwenye office , Head of Sales analipwa Mil 18, na dereva analipwa laki 3 , hapo kuna unyonyaji mmoja ampunguzie mwingine?

Nilifikiri kwa mtu mwenye hadhi yake angeongelea Muundo wa Bunge na namna gani wanaweza punguza vikao na safari zisizo na tija yeye analinganisha mishahara?

Duniani kote watu wanalipwa kutokana na Value na Impact anayoweza sababisha kwenye jamii..

Kalangabhao
Hilo sio tatizo kama lakini 3 inamtosha kukimu maisha yake. Ila kama hazitoshi ujue atafanya kila njia kujiongezea kipato hata kama ni kuiba matairi na petroli. Kama zinamtosha kulipia makazi yake, kumlisha yeye na familia yake, kusomesha watoto, kulipia gharama za hospitali inapobidi n.k. hatakuwa na tatizo akiona Bosi wake analipwa milioni 18. Na huyo Bosi atakuwa anatakiwa kila mara kumthibitishia muajiri wake kuwa anastahili mshahara huo. Hiyo ni tofauti na wabunge ambao wengi hawachangii lolote katika kuisimamia serikali na kulinda maslahi ya waliomchagua.

Amandla...
 
Sasa hivi ndio nimeelewa kwanini Walimu wanaishi kwenye Poverty.
 
So issue ni time ya kusema? Walioko bungeni kwa sasa kuna ambae amesema?
Hawana pia moral authority ya kusema kwa sababu ndio mfumo unaowafaidisha.Sio kusema tu bali ni kuonyesha solidarity kwa kutopokea hiyo posho sio maneno matupu.
 
Hayo ndiyo malipo ya mbunge, je mbunge akiteuliwa kuwa waziri au naibu waziri malipo yake si yatakuwa zaidi? Na bado rushwa na ufisadi wanaofanya

keki ya taifa ipo kwaajiri ya wateule wachache wa CCM
 
With due respect angeenda a step further na kukataa kupokea kama solidarity na wengine wenye kipato cha chini.Hii huwa inafanyika kwa wanaoamini wanachokipigania sio maneno matupu.
Mtumishi wa umma hawezi kukataa mshahara na posho zake anazostahili. Atalipwa tu stahili yako hata aseme nini. Njia pekee ya kuzuia kulipwa ni kuacha kazi. Anachoweza kufanya ni kuupokea na kuutumia kuwahudumia wananchi wenzake na kuendelea kupiga kelele.

Amandla...
 
Mnafiki tu huyu.Angelalamika kwamba posho ni kubwa ipunguzwe akiwa mjengoni angekuwa na credibility. Kuwa nje ya mjengo halafu ulalamike ni unafiki tu na hadaa.
Wewe ndio mnafiki na Hujitambui!

Heche amekuwa akisema hayo tangu akiwa bungeni
 
Hilo sio tatizo kama lakini 3 inamtosha kukimu maisha yake. Ila kama hazitoshi ujue atafanya kila njia kujiongezea kipato hata kama ni kuiba matairi na petroli. Kama zinamtosha kulipia makazi yake, kumlisha yeye na familia yake, kusomesha watoto, kulipia gharama za hospitali inapobidi n.k. hatakuwa na tatizo akiona Bosi wake analipwa milioni 18. Na huyo Bosi atakuwa anatakiwa kila mara kumthibitishia muajiri wake kuwa anastahili mshahara huo. Hiyo ni tofauti na wabunge ambao wengi hawachangii lolote katika kuisimamia serikali na kulinda maslahi ya waliomchagua.

Amandla...
Upo sahihi kiasi

Ila mshahara haumtoshi mtu hata siku moja mkuu...

Hao wabunge wenyewe wana madeni ya kuwatosha na bado wanakopa na wakitoka huko hali mbaya
 
Mnafiki tu huyu.Angelalamika kwamba posho ni kubwa ipunguzwe akiwa mjengoni angekuwa na credibility. Kuwa nje ya mjengo halafu ulalamike ni unafiki tu na hadaa.
Kosa moja halihalalishi jingine.
Labda kwa walumbavu ndipo justification ya namna hiyo inaweza kuwa sawa.
 
Kwa hiyo ndiyo mjilipe pesa zote hizo,afu walimu ambao ndiyo wenye impact kubwa katika jamii kuliko hawo wabunge mnawanyonga hivyo.
Mkuu laiti ungejua kuwa walimu kwa ujumla wao ni rahisi sana ku replace, na hapo ndipo panapotofautisha Value, Impact na Uwezo wa mwajiri kupata mwingine mwenye aina yako.
 
Back
Top Bottom