Kwa kufuatilia press za Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Heche sijapata kusikia hii taarifa ya Heche kukiri kuwa kuna baadhi ya viongozi wa CHADEMA wanhusika kuchochea kufanya vurugu bali wakati wote CHADEMA na viongozi wake wamekuwa wahanga kwa kukanamizwa na Serikali ya Samia
Kama ni kweli basi itakuwa ni kutaka kuchafua na kuharibu imani ya CHADEMA kwa wananchi, hao viongozi kama mnawatambua wafukuzeni
Kama ni kweli basi itakuwa ni kutaka kuchafua na kuharibu imani ya CHADEMA kwa wananchi, hao viongozi kama mnawatambua wafukuzeni
- Tunachokijua
- Madai
Kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook kumekuwapo na grafiki yenye utambulisho wa Jambo TV huku ikiambatana na ujumbe unaodaiwa kuwa ni wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara, John Heche amesema.
"Tunatambua kuna baadhi ya viongozi wenzetu (CHADEMA) wanatumika katika kuchochea hizi vurugu"
Uhalisia wa taarifa hiyo
JamiiCheck kupitia ufuatiliaji wa kina imejiridhisha na kubaini kuwa taarifa hiyo ama nukuu hiyo haijatolewa na John Heche.
Grafiki yenye ujumbe potoshi inarejea hotuba ya Heche aliyoitoa Novemba 19, 2025 ambapo pamoja na mambo mengine hakuzungumza maneno hayo kuwa;
"Tunatambua kuna baadhi ya viongozi wenzetu (CHADEMA) wanatumika katika kuchochea hizi vurugu"
Katika hotuba yake Heche alipinga tume iliyoundwa na Rais Samia ikiwa na lengo la kuchunguza kilichosababisha vurugu za Oktoba 29, 2025 wakati wa uchaguzi mkuu 2025.
Ufuatiliaji zaidi umebaini kuwa grafiki hiyo haijachapishwa na chombo cha habari cha Jambo TV kupitia kurasa zake rasmi na badal yake ni za kughushi na zimetumia fonts tofauti.