Heka Hela za machimboni: Hizi ndizo sifa za Hoteli (migahawa) ya masankuloni ukiwa machimboni

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
6,944
Reaction score
14,351
Enyi wadau ukienda machimboni halafu upite kula masankuloni basi kuwa makini.

Kwanza hoteli hizo Huwa chini ya mti mkubwa kama mwembe ama utakuta wamefunga hema na jioni litaondolea nk.

Wa mama lishe mara nyingi chakula hupikia kwao majumbani na kubeba Kila Asubuhi Hadi sehemu husika.

Mara nyingi chakula ni makande, mchanyato.wali ugali na mboga hupikiwa hapo hapo kwani majiko ya mkaa hubeba pia.

Mteja ukienda kula huko chakula Cha 500 ama 1000 ni chakula Cha kushiba.

Mfano unaweza agiza wali wa 1000 na maharage ukashiba Hadi kubakiza wali nyama 1500-2000 utakula na kushiba.

Ikitokea umebakiza hicho chakula basi jua wazi kuwa hicho kilichobaki hakitupwi!!

Hapo Sasa iwe chai utakunywa ibakie utatunzwa chapati ibakie itatunzwa.

Huo wali uliobaki iwe ulikula na samaki ama nyama na ukabakiza utatunzwa.

Basi huchanganywa na kuitwa mchanyato mixer!! Huo mchanyato mixer ukienda na jero utakula Hadi ubakize pia na utatunzwa Tena vilevile.

Hata kama una Hela ya chai tu yaani200 chapati utapata Bure kakipande ama vipande vitatu.Hapa hutegemea na ukubwa wa kipande kilichobakizwa.

Kuna muda ukienda huna Hela kabisa utakula na utashiba Bure kabisa na utahudumiwa kama mteja wa VIP.

Kule chakula chote hicho kilicho mixsiwa hutupwa saa3-4 usiku wateja wakiwa wameisha.

Katika kufanya research yangu ndogo niligundua Hawa wamama lengo lao sio baya kabisaa!

Ukiwa chimboni huko kupigwa doro ni jambo la kawaida unaweza maliza hata siku2 au hata wiki hujaingiza Hela yoyote ama unapata Hela kidogo mno.

Katika Hali kama hii Kimbilio lako ni huko masankuloni.utakula na kama Kuna kivuli kikubwa utalala chini ya mti na kuamka Tena!

Kama wewe utaenda kiboss utahudumiwa kiboss vilevile huo mchanyato hutauona Wala hutajua kinachoendelea Hadi walengwa maalumu. Wapo kabisa wanajulikana bayana.

Sasa ukijichanganya wewe usiye zoea huu mchanyato mixer utaharisha Hadi ukasimulie.

Huo mchanganyiko hauna harufu maalumu ukisikia mchanyato mixer ndo huo harufu ya samaki imo,nyama imo,maharage na mboga za majani zimo. Wamama wapo smart sana hutokuta mfupa Wala mwiba wa samaki mle!!

Guest house,loudge za machimboni.

Hapa Sasa Kuna gest Hadi za 1500! Kwa usiku mzima fasta buku nk.

Hizi gest bana za 1500 hazina mashuka na magoro nimeusi tii na yananuka. Mara nyingi wateja ni walevi,wachimbaji ambao akili imeruka kiaina nk.

Magoro haya mara nyingi Huwa yanatoka chimbo Hadi chimbo Kwa kuhama hama Kila panapo Hila(panapo vuma Kuna dhahabu)

Zipo zingine za buku3000 Kwa usiku!. Hizi Zina uafadhar mtu wa aina yoyote anaweza lala japo Kwa shida kiasi.

Hapa utakuta magoro hayajatumika sana japo pia utakuta hakuna mashuka ni godoro kama godoro tu.

Hizi unaweza pigwa hata 5000 wewe kama ni mgeni.

Basi ilikitokea siku Moja nikalala kwenye gest za buku3000 kipindi hicho .kwanza hizi gest mle ndani ukuta na ukuta Huwa zinatofautishwa na hema (turubai)

Na kunakuwa na milingoti iliyochanwa kati ikawa miepesi sana.

Jirani yangu akaingiza demu kwake

Usiku ule ulikuwa mrefu sana kwangu. Jamaa aliipiga Hadi wakadondoshana kwenye chumba changu asee.

Baada ya kuangusha kwangu nikawauliza oyaah vipi Tena mbona Fujo mkuu?.

Jamaa akanijibu kausha man nikajua labda watafunga hili turubai lao kwakweli walipanda kitandan na kuanza Tena kupelekeana moto.

Nikawa nawasha tochi ya simu nikidhani labda wataacha ama kupunguza lakini haikusaidia.

Ule usiku kwakweli haukuwa mzuri kwangu nilipitisha usingizi saa10 japo nilitakiwa niamke tena saa12 kuendelea na kazi yangu.

Kufupisha hizi gest hutofautiana ubora na ulinzi pia kwani zipo za madoni hulala na hakuna kelele pia Kuna ulinzi!

Kunachimbo fln chumba Cha madoni unalipia 30k per day.

Kwa ujumla hizo gest zote hujengwa Kwa mabati juu Hadi chini mabati tupu. Wakati wa mchana huwezi lala mle maana panachemka balaa.

Ukienda lazima utakuwa kama unapigwa nyungu(sauna) Kwa jasho lake!

Gest za buku ten nk mle ndani chumba na chumba kimetenganishwa na bati vilevile.

Ikitokea jirani Yako kaleta demu mle utapata tabu sana kwani Kila mguno utausikia na mapigo ya pumb*Ile pwa pwaa ama paa paaa nk utayasikia.

Hakuna kiyoyozi kwenye gest za chimbo.

Starehe machimboni.wakuu hapa Sasa ndo mahala pake chimbo LIKIWA limetema kabisa Kwa siku kuingiza 50k nikawaida hata uwe mama ntilie tu!!

Sikia Kuna Wakati huchanganya watu Wana banana kama mnavyopishana hapo kariakoo
Kwa walio bahatika kufika nyangarata kipindi limetema watakubaliana na Mimi watu walikuwa wengi mno.

Ile bapa la katani(mkonge) lilikuwa linauzaa buku. Kuchimbia mashimo labda Kuna mtu anatengeneza kibada ilikuwa Kila shimo3000-5000/=

Hapa Bata lake lilikuwa sio la mchezo. Bar Huwa ni nyingi kama utitiri na Huwa wanauza mnoo.

Bia husombwa kuanzia asubhi Hadi jioni watu wanapshana tu kupeleka kwa bajaji ama tractor.

Hawa makahaba wenu wa mjini hurudi huku maana Huwa kumenoga sana.

Kwa kifupi tu hata iwe wapi Bata la machimboni Huwa la aina yake mno na Huwezi kulifananisha na sehemu yoyote Ile.

Ng'ombe wanaochinjwa ni wengi mno mbuzi pamoja na kuku.Huduma zote za muhimu uzijuazo wewe hurudi huko machimboni.

Usalama. Kwa upande wa usalama hutegemea lakini si pakuamini sana ukiuza usilale porini(chimbo) nenda mjini kahifdhi Hela zako.

Ubabe huko ni sifa ya Kila mchimbaji hakuna mnyonge kule.

Tena duara yenu ikihira(kuwa na dhahabu) Kuna jamaa wanaoitwa manyani.

Manyani Hawa Huwa hawana duara yao.kazi Yao ni kuzamia tu kwenye duara zilizo fika na Zina mzigo.

Akizamia huingia na bob Marley mgongoni hako pekee ndo atachambua mawe yenye Mali
Na kuondoka nayo.

Kipindi anazamia anakuwa yupo tiyari Kwa lolote kufa ama kupona kupigana ama kupigwa!!

Hapa Sasa ndo Huwa wanakutana na upinzani mkali lakini mara nyingi wenye duara huishia kukimbia! Au kuwapisha Kwa amani kabisa.

Maana wao wanakuwa wamejitoa kufa ni sawa na jambazi avamie kwako kule huitwa manyani na wanakuwa wanafahamika kabisa

Kwahiyo jambo la usalama hasa Kwa miaka ya nyuma lilikuwa dogo sana kwani mchimbaji alichukuliwa kama mtu aliye shindikana ama aliye acha familia yake na kuendelea na maisha hayo yeye anakuwa ni mtu wa kuhama tu Leo yupo hapa kesho kule.

Karibu machimboni.

Screenshot_20241026-160716_1.jpg
 
Na kunakuwa na milingoti iliyochanwa kati ikawa miepesi sana

Ubabe huko ni sifa ya Kila mchimbaji hakuna mnyonge kule
Tena duara yenu ikihira(kuwa na dhahabu) Kuna jamaa wanaoitwa manyani.

Manyani Hawa Huwa hawana duara yao.kazi Yao ni kuzamia tu kwenye duara zilizo fika na Zina mzigo.

Akizamia huingia na bob Marley mgongoni hako pekee ndo atachambua mawe yenye Mali
Na kuondoka nayo.

Kipindi anazamia anakuwa yupo tiyari Kwa lolote kufa ama kupona kupigana ama kupigwa!!

Hapa Sasa ndo Huwa wanakutana na upinzani mkali lakini mara nyingi wenye duara huishia kukimbia! Au kuwapisha Kwa amani kabisa.

Maana wao wanakuwa wamejitoa kufa ni sawa na jambazi avamie kwako kule huitwa manyani na wanakuwa wanafahamika kabisa

Kwahiyo jambo la usalama hasa Kwa miaka ya nyuma lilikuwa dogo sana kwani mchimbaji alichukuliwa kama mtu aliye shindikana ama aliye acha familia yake na kuendelea na maisha hayo yeye anakuwa ni mtu wa kuhama tu Leo yupo hapa kesho kule.

Karibu machimboni.View attachment 3135959
Aiseee,Asante boss.
Bado uko machimboni?
Hamna connection?
 
Umenikumbusha kitunda SIKONGE TABORA
Kitunda nilikua nakuja asubuhi , usiku naenda kulala mission, itumbi, nyangarata, nyanzaga, kiwanja, saza , ukweli kama mpambanaji haukuwahi kupita machimboni bado unakua kama underground , haujui timba ni nini, fonga/fonka, vikole, Azam mifuko, karasha, Mercury , mwalo baadhi ya terms , mchimbaji anatembea hakuna mchezo akisikia Dar pori , mbinga mbinguni nae yupo, akisikia mpanda kama kawaida kafika, mnakua wengi wengi hupata na wengi hukosa , mwisho wa siku mfanyabiashara ndio anapata hela , wengine zinaishia kwenye starehe , hadi Makota wanaendekeza starehe wanaishiwa
 
Back
Top Bottom