Hekaheka Uzeeni

Hekaheka Uzeeni

Balaa
UPDATE

Simulizi hii ina misimu mitatu (three seasons) na zote zitakuwepo kwenye uzi huu huu.

1st season ina episodes 4 tu japo ndefu ndefu kiasi.

2nd season ipo post #90 na episodes zake ni fupi fupi...

UTANGULIZI

Maisha baada ya kustaafu huwa yana ‘stress’ nyingi. Kujaribu kupunguza stress hizo nilifungua ‘account’ hii JF ili kujiburudisha na kuburudishwa. Account zangu nyingine JF zina ‘personality’ tofauti kabisa.

Michengesho (decoys) zipo kama kawaida ili kulinda nukta kuunganishwa.

HEKAHEKA UZEENI

Sehemu ya kwanza – KUSTAAFU UTUMISHI WA UMMA SI JAMBO LA GHAFLA.


Katika kazi za utumishi wa umma, wapo wanao staafu wakiwa na miaka arobaini na mitano na kuendelea, mimi nilibahatika kufanya kazi hadi miaka sitini na kustaafu kwa mujibu wa sheria. Kujifunza ‘hakwishi’, kuna karaha zake baada ya kustaafu hususani wakati wa kufuatilia stahiki zako. Angalau siku hizi utaratibu ni mzuri sana usumbufu umepunguwa kwa kiasi kikubwa.

Kwakuwa kustaafu ‘hakukuji’ ghafla, yampasa mtumishi yeyote aliyeajiriwa kuajiandaa na maisha baada ya kustaafu. Tumeshuhudia wengi baada ya kustaafu kuendelea Kwenda eneo la kazi na kukaa kupiga soga nk, hii hutokana na ama kufuatilia mambo yake ama kukosa sehemu muafaka ya Kwenda kwakuwa labda hakujiandaa na mahali ya Kwenda baada ya kustaafu.

Miaka 45 ni mtu mwenye nguvu bado, hivyo anaweza kufanya Maisha yaendelee kwa mtindo mwingine bila kuathirika na kazi alizozioea kazini, vivyo hivyo kwa miaka 50 ama 55 ama 60 na hata 65 bado mtu anaweza kujishughulisha na mambo ambayo yatamfanya asiwe ‘bored’

Mara nyingi kwa watumishi wengi maisha yao baada ya kustaafu huwa ni ya upweke, ‘kupigwa mizinga’ kutoka kwa ndugu na jamaa na usipokuwa makini utajikuta unapata magonjwa ya kisukari na moyo pasipo kutarajia kutokana na mtindo wa maisha utakao kuwa nao.

“…hela ya mafao ya kustaau siyo ya kujengea kaka…!” aliwahi kuniambia mzee mwenzangu mmoja aliyetangulia kustaafu.

“…hiyo hela ni ya kukutunza wewe, ni ya kufurahia maisha yako ya uzeeni hadi siku Mwenyezi Mungu atakapo kuchukuwa…”

“…ndugu na jamaa wengi watakuletea shida zao, sisemi usiwasaidie, lakini saidia kwa kiasi tu ili usiharibu fungu lako wala uhusiano wako na ndugu na jamaa, ikiwezekana tangaza hali mbaya ya uchumi kabisa ili wasiweke dhana kwamba una hela, singizia chochote kuepusha usumbufu, mwenzako yamenikuta sana…” Ni maneno yamzee mwenzangu mwingine ambaye yeye alitangulia kustaafu pia.

Sentesi ya ‘hela ya kustaafu ni ya kufurahia maisha..’ ndiyo iliyonifanya nianze kuandika simulizi hii.

Kama nilivyoserma awali, kwakuwa kustaafu ‘hakukuji’ ghafla yapaswa kujiandaa kwa kuwa na miradi midogo midogo wakati ukiwa bado katika utumishi. Hii ni kwa wote, watumishi wa umma na wa sekta binafsi. Anzisha mradi wowote wenye kukuingizia kipato hata kama ni kidogo ili mradi kiweze kukidhi mshahara wa anayesimamia, kutunza mtaji, kukuza mtaji na kujipatia faida kidogo. Hapa nazungumzia wale ambao kima chao cha mshahara ni cha chini. Kwa wale wenye vima vya juu nawashauri wafikirie kufanya miradi mikubwa yenye kuleta ajira kwa vijana na kutopeleka hela nje ya nchi, wekezeni humu humu nchini hiyo miradi yenu mikubwa kwa maana mzunguko wa fedha hizo zitabaki ndani. Sisemi msiwekeze nje ya nchi lakini nasema msisahau kuwekeza ndani kuwasaidia hawa vijana wetu wanaomaliza masomo yao kila mwaka.

Hebu niache haya mambo ya ushauri-nasihi usio rasmi maana kila mtu anajipangia mambo yake mwenyewe, lakini usisahau pia kuishi na mkeo / mmeo vizuri maana ukitangulia kustaafu kabla ya mwenza wako na haukuwa unaishi naye katika mahaba tarajia ‘stress’ za vijimambo vidogovidogo tu ambapo sasa vitakusanyika na kuwa kero.

nijikite sasa kwenye hii sentesi …”..hela baada ya kustaafu ni za kufurahia Maisha…”

Wakati na mbwela-mbwela kusubiria ‘fuba’ la mkupuo si nikapata mkataba fulani hivi kusaidia mambo fulani nchini DRC!. Ulikuwa ni mchongo wa miezi mitatu. Namshukuru sana yule jamaa aliyeniunganisha maana alikuwa anajuwa uwezo wangu katika fani ile kuhusiana na mchongo huo.

‘Paapu’, nikaambiwa niripoti Goma – Kivu ya kaskazini DRC tarehe fulani. Nikajiangalia mfukoni nikaona kuchukuwa flight hakunifai.

“…bora nipande basi kwa kuwahi wiki moja kabla ya tarehe husika…” nilijisemea moyoni.

Wakati huo Stendi ya Mbezi, “Magufuli Bus Terminal” ilikuwa bado haijaanza kutumika, hivyo nikatinga Ubungo bus terminal kuangalia usafiri maridhawa. Nilikuta kuna basi mbili za kampuni moja ambayo niliambiwa ni wazuri kwenye huduma ambazo zote zilikuwa zinaenda Kigali. Nikakata tiketi ya basi kubwa kama walivyokuwa wakiita wenyewe.

Kwakuwa huwa napenda kuona mbele ya basi kwenye lami, nilichaguwa siti ya nyuma ya dereva siyo upande wa dirishani lakini ingawaje palikuwa bado hapajachukuliwa. Sababu nyingine iliyonifanya kuchukuwa nafasi hiyo nili ile nafasi kati ya dereva na siti nyuma yake ni kubwa pa kuweza kunyoosha miguu na pia kuna kama meza fulani hivi mbele (fridge) hivyo kufanya paonekane ni sehemu muafaka kwangu kwa safari ndefu kama ile.

Siku ya safari nikafika mapema sana Ubungo bus terminal, moja kwa moja kwenye eneo ambalo basi husika lilikuwa linapakilia abiria, nilikuta baadhi ya abiria wakiwa tayari ndani ya basi ingawaje nilifika takribani nusu saa hivi kabla ya safari. Sikuwa na mizigo bali backpack Fulani hivi kubwa kiasi ambayo iliweza kubeba laptop yangu pamoja na nguo zangu chache ambazo nilidhani kwa kazi ya siku 90 ningeweza ‘kupiganisha’ bila kuhisi sina nguo za kubadilisha.

Kampuni ya basi ilikuwa inaitwa ‘utatu mtakatifu’, kwa kweli basi nililopanda walijitahidi sana kufanya liwe na hadhi yake mle ndani, viti vyenye vitambaa vya ngozi (synthentic leather), nafasi kubwa kati ya siti na siti, ila kwenye lugha za kuhudumia wateja walikuwa wanafeli sana, sijui ni kwa sababu ya kutojuwa Kiswahili vizuri ama nini. Hakika kwenye hili walikuwa wanafeli, siku hiyo kulikuwa na madereva wawili, mmoja Mtanzania na wa pili ni Mnyarwanda, na mhudumu tuliye safiri naye mmoja mwanume na mwingine ambaye alishukia njiani alikuwa ni wakala wao, akisindikiza gari.

Nilitulia kwenye kiti vizuri huku basi likiwa limekaribia kujaa kabisa abiria lakini kwenye kiti changu bado hapakuwa na abiria aliyekuja. Shingo nikiwa nimeinua juu kidogo kuangalia kwaya walizoweka kwenye runinga ya basi pale mbele mara nikasikia sauti ikiniambia…

“Excuse me, let me pass that is my seat..” alikuwa ni binti mrembo na kwa sura ile moja kwa moja nikajuwa huyu ni Mnyarwanda.

Nikampisha bila kusema neno, na alipokuwa ameketi sasa ikanibidi siti nibonyeze sehemu ili kuongeza nafasi ili tuenee vizuri maana si kwa ma ‘hips’ yale.

“Hujambo?” nilimsalimia na akaitikia kwa kichwa huku akiendelea na mambo yake mara kashika hiki mara kashika kile ili mradi alikuwa hatulii kama ana wasiwasi fulani hivi kama vile kuna jambo halijakamilika.

Macho nikarudisha kwenye runinga kuendelea kuburudika na kwaya za kisabato, ‘what a beautiful melody!’

Punde si punde mlango wa basi ukafungwa na tukawa kwenye foleni ya kutoka nje ya bus terminal. Ajabu ni kwamba vurugu za mabasi kugombania kutoka nje ya geti zilikuwepo licha ya utaratibu mzuri ambao uliwekwa na uongozi wa kituo na kusimamiwa na askari.

Baada ya chekecha chekecha ya hapa na pale hatimaye tukawa kwenye mstari ulionyooka sasa wa kutoka nje. Nikageuza shingo kuangalia nyuma, hakika basi lilikuwa limejaa na hakukuwa na mtu aliyesimama zaidi ya mhudumu mmoja na Yule msindikizaji ambao wote walisimama pale mlangoni, wakati huo tayari yule wakala msindikizaji alikuwa amesha maliza mambo ya ushuru wa getini nk.

===

Safari iliendelea hadi maeneo ya Mbezi Luis ambapo yule msindikizaji alikuwa ameshakamiliza zoezi lake la kukabidhi kila abiria tiketi ya mashine ingawaje tulikuwa na zile tiketi za karatasi. Tiketi hizi za mashine (POS) hazikuwa hizi zilizounganishwa na mifumo ya LATRA na TRA bali zilikuwa kwa ajili ya udhibiti wa kiofisi yao tu.

Niliangalia begi langu kwa mara nyingine, nikajiridhisha lipo salama haliwezi kumuangukia abiria wa jirani maana nililiweka kwenye kibebeo (carrier) cha upande wa kushoto wakati mimi nipo siti za upande wa kulia ili niweze kuliona muda wowote ninapotaka ingawaje watu wengine hupenda kuweka upande huo huo alipo kaa yeye tena juu sehemu aliyokaa.

Safari iliendelea, wakati huo video ilikuwa imezimwa na kufunguliwa radio (RFA) tukiendelea kupata habari. Kwenye hili la kelele za miziki, video za ndani ya basi walikuwa wamefanikiwa, maana hawakuwa wakifungulia kwa sauti za juu, ilikuwa sauti ya kadri tu ambapo hata ukiongea na simu kwa sauti ya chini bado mtasikilizana.

Basi lilitembea mwendo wa Serikali, ‘tatu bila, tano bila nane bila’ hadi tulivyofika Chalinze na misafara ya mabasi kuongozana na kukimbizana ikapungua na mabasi kuanza kumwaga moto. Kutoka Mbezi hadi Chalinze nadhani siku hiyo kulikuwa na fatiki kabambe ya ‘traffic police’ kwa maagizo ya kamanda wa wakati huo, maana kabla ya safari kulisikika tangazo pale Ubungo bus terminal kuwa madereva wote wakusanyike sehemu husika kwa ajili ya kuongea na Kamanda (alitajwa). Nadhani semina fupi ile iliwaingia hadi Chalinze tu, sijui madereva wa mabasi wana matatizo gani, kha!

Basi lilikuwa ni YUTONG, sijui namba ngapi ngapi lakini wenyewe wanasema ndio kubwa katika mfululizo wa wakati huo. Huko mbele ya safari ndio nikajuwa maana niliona ilivyokuwa inafunguka. Licha ya kuchezewa vts lakini pia nahisi ‘limiter’ ya spidi pia ilichezewa, si kwa mwendo ule baada ya kuvuka Rusumo border.

Chalinze hadi Moro basi lilitembea lakini ile kibongo bongo, minara ilikuwa inafanya kazi maana yule mhudumu muda wote alikuwa na simu sikioni na mkono mmoja ameweka juu ya dashboard, mara anapiga dashboard mara anainua kama vile anaita yani alikuwa anapata taarifa nje ya basi na yeye alifikisha ujumbe kwa dereva kwa kupiga dashboard, kuinua kiganja na kuita kwa kiganja.

Mwendo haukuwa hatarishi kiasi cha kuripoti kwa askari waliokuwa akiuliza sehemu za ukaguzi na dereva wala hakuwa mchafuzi wa overtake za ‘kubeti’ ila kwenye mwendokasi sehemu za hamsini hadi tulivyofika mbele kidogo ya Singida. Huko ilikuwa muda mwingi ni over 90kph.

Kabla ya kufika Morogoro, jirani yangu ambaye katika simulizi hii nitampa jina la Janeth, alikuwa ametulia, maana muda wote tangia Dar alikuwa kwenye simu akiongea mara akiandika jumbe za simu. Nikaanza kumsemesha sasa kwa Kiswahili ili kujuwa uwezo wake katika lugha hii adhimu, alikuwa anajibu kwa tabu sana ingawaje alifinyanga finyanga tukawa tunaelewana.

Kwa haraka haraka kutokana na maongezi ndani ya basi, nikajuwa mle ndani kuna Wabongo, Wanyarwanda, Warundi, Wakongo, wa Uganda na Wakenya. Pia kulikuwa kuna watu weupe wawili mmoja akiwa mwanamme, sijui ni Wazungu au Wamarekani lakini hawakuwa Waasia.

Janeth hakuwa mweupe wa rangi, bali maji ya kunde na aling’aa vyema kama ngozi yake ilivyokuwa ikionesha, alivaa ‘tracksuit’ na raba kama vile alikuwa ametoka kufanya mazoezi, nywele alisokota rasta bila kuunganisha nywele za bandia. Hakunizidi urefu, mana pale Chalinze tulipokuwa tunakunywa chai tuliteremka pamoja na kutembea pamoja kabla hatujaachana njia mimi nikielekea maliwatoni upande wa wanaume.

Kwakuwa mimi ni mpenda chai ya maziwa yenye kahawa, basi nilienda upade ule kwenye huduma hiyo na yeye Janeth wa sikumuona tena alipoelekea.

Kwenye jambo hili la kuwapa muda wa kutosha abiria wakati wa chakula, hawa jamaa nao walifaulu vizuri, maana mhudumu alipotangaza alisema tutatumia nusu saa kuchimba dawa pamoja na kupata chochote, tuzingatie namba ya basi maana yalikuwa mawili, baadaye sana ndio nikajuwa kuwa moja litaelekea Uganda na lile tulilopanda ndio litaelekea Kigali.

Kwakuwa siti yangu ilikuwa jirani na sikuwa nakaa dirishani, niliingia wa mwisho mwisho kwenye basi na kumkuta Janeth akiendelea kula nyama za kuchoma alizofungiwa kwenye bahasha fulani hivi ya khaki.

“Welcome nyama choma…” alinikaribisha huku akimaanisha nichukuwe msongo mmoja niendelee nao…

“Aaah, ahsante sana, unaitwa nani?” nilijibu huku moyoni nikikataa kuchukuwa nyama kwa ishara ya kuonesha nimetosheka (nimeshiba)

“Yaleyale ya kupewa chakula na usiyemjuwa wala kuona chakula kilipotoka mwisho wa siku unajikuta umeshaibiwa…” niliwaza.

Nikatoa ‘chewing gum’ za ‘mint’ na kuanza kutafuna ili kuweka kinywa changu katika hali ya kuanzisha maongezi ya kisafari safari.

“Karibu bublish…” nilinyoosha mkono na kumpatia kadhaa na akapokea kimya kimya na kuzihifadhi kwenye kimfuko kidogo kilichopo kwenye lile friji mbele ya siti zetu huku akiendelea kutafuna minofu ya mishikaki ya ng’ombe.

Safari ikaanza tena tukiitafuta mizani ya Mikese, mwendo mzuri, nane bila na uchafuzi wa speed kiasi maana dashboard nilikuwa naiona lakini ilikuwa haizidi 89kph. Pila nilikuwa na Garmin Drive 52 iliyoipata katika harakati za kutafuta ugali ambapo katika safari hii nilitarajia itanisaidia kule niendako ambako sikuwa na uhakika wa coverage ya internet.

Kelele za king’amuzi (vts) kilikuwa almost muda wote alipokuwa zaidi ya 85kph kinasikika kwa mbali sana, sijui waliweka kitu gani wale jamaa, maana kama sio mjuzi wala huwezi kuelewa ni kitu gani kinaendelea, dereva huyu Mtanzania alikuwa na nidhamu ya michoro ya makatazo ya kuovateki ila alikuwa ana ‘maintain maximum’ ya Latra muda mwingi, hii ilifanya tusiwe nje ya muda wa ratiba ya gari.

Janeth mkononi alikuwa amevaa kitu mama shanga hivi maarufu kama “culture” lakini ilikuwa na bendera ya Kenya.

“Wewe ni mkenya?” nilimuuliza huku nikiutolea macho mkono wake wa kushoto ambao ndio alikuwa amevaa hiyo shanga.

“No, Mnyrwanda” alijibu huku akitabasamu.

Nikachukuwa smartphone yangu, nikafungua playstore ili nidownload dictionary ya English – Kinyarwanda lakini haikunisaidia sana maana wakati huo bado haikuwa na maneno mengi.

“Do you speak English” nilimuuliza tena ili kama vipi tuhamier kwenye Kiingereza maana Kiswahili chake kilikuwa hakieleweki.

“Kidogo…” alijibu kisha akaendelea … “French and Kinyarwanda okay...”

Katika harakati za maisha sikubahatika kujifunza Kifaransa, bali niliyajuwa maneno machache sana maana rafiki yangu wa zamani sana, mototo wa Kihindi aitwaye Raani alinipatia kamusi ya Kifaransa kwa kiingereza lakini wala sikuwa na mzuka. Raani binti yule wa Kihindi urafiki wetu haukudumu kwa sababu ya Sue mototo wa Kispaniola ambaye naye pia wala hatukufika mbali, maana baada ya chuo tu miezi ishirini hivi baadaye mawasiliano yalikatika.

Alivyojibu kuwa kwenye Kifaransa na Kinyarwanda ndio yuko vizuri, basi sikuwa na chaguo lingine zaidi ya kuvumilia Kiswahili chake na kiingereza chake ingawaje kwenye kiingereza alikuwa yuko vizuri zaidi kuliko Kiswahili.

Hili ni jambo lingine la kushangaza, yani ukitoka Bongo kwenda Rwanda, hapo Rwanda wenyeji wanazungumza kilugha chao tu na Kifaransa, siyo wengi wazungumzao kiigereza. Ila ukivuka Rwanda kwenda Congo DR huko utakutana na Kiswahili cha aina yake, lakini angalau watu wanaelewana.

Kigali haikuwa mara yangu ya kwanza kwenda, lakini huko Goma ndiyo ilikuwa ‘fisrt time’. Niliuchangamkia huo mchongo ingawaje Hamida alinikataza nisiende kwa kuhofia hatari iliyopo ya vita baina ya majeshi ya Serikali na watu wanaojiita waasi.

“The first time when I saw you, I knew for sure you are Mnyarwanda…” nilisema.

“Why?” aliniuliza.

Hapo ndipo nikafunguka kuhusu jinsi sisi Wabongo tunavyowaona Wanyarwada. Nilimwambia kuhusu maumbile yao ya urefu, sura nyembamba, urembo wa asili, nyama za kutosha sehemu ambazo huwafanya wanaume wageuke nyuma kuangalia ili kuburudisha macho, nikaeleza weee mwishoe naye akaniambia kuwa hiyo dhani si asilimia mia sahihi, siyo Wanyarwanda wote warembo kama nilivyowapamba…

Eeee ni kweli nilimpamba sana ‘mixer’ ukweli na chumvi ili kuwasifia kama ilivyo kawaida ya wanaume.

Kwakuwa Rwanda haikuwa mara yangu ya kwanza kwenda, nilikuwa najuwa hawa warembo tunaowaona kwenye mitandao ni wachache tu, wanawake wa Kinyarwanda wapo kwa maumbile mbalimbali na sura tofauti wengi ni wa kawaida sana na tofauti kabisa na tunao waona hawa wa kwenye mitandao. Hata hivyo haiondoi ukweli kwamba wapo wanawake warembo wa sura na maumbile huko Rwanda. Tabia zao tu ndio zina ukakasi kiasi fulani juu ya kujiona wapo matawi ya juu sana, kuwa na ukatili uliojificha labda kutokana na historia yao nk.
“…Lakini sasa mbona umevaa bendera ya Kenya?” nilidadisi.

Hapa akafunguka kuwa yeye ni mfanyabiashara, ana duka la nguo za wanawake kwao Kigali na kabla hajajuwa machimbo ya Tanzania alikuwa akifungia mizigo yake Uganda na Kenya, na hiyo ‘bracelet’ aliyovaa aliipatia Kenya…

Mazungumzo ya kawaida yaliendelea kama ilivyo kawaida kwa abiria na abiria. Safari nayo ilisonga salama kabisa hadi tukafika Dodoma pale jirani na panapoitwa ‘four ways’, tukawa na ‘short break’ ya dakika kumi ya ajili ya kuchimba dawa kisha safari iliendelea hadi Singida baada ya mizani mbelembele kidogo gari ikaingia sehemu fulani kuna hoteli ambapo napo tulipata dakika ishirini za kuchimba dawa na kupata chochote kisha safari ikaendelea. Tulipokaribika Igunga giza fulani hivi lilianza kuingia, hadi tunapita mzunguko wa Nzega pale tayari dereva yuleyule tuliyetokanaye Dar akiwa anaendesha hadi muda huo aliwasha taa hafifu zilizowaka kwenye sakafu ya basi pembeni pembeni na kufanya mandhari kuwa nzuri sana ndani ya basi.

Awali nilidhani basi litanyoosha moja kwa moja hadi border ya Rusumo lakini kumbe hayapitilizi bali wanalala Kahama kisha asubuhi na mapema safari huendelea hadi boda.

“Have you made your reservation to pass your night at Kahama…” Janeth aliniuliza wakati gari ikiwa inakunja Tinde kuelekea Isaka.

Nilimjibu kuwa sijafanya chochote, si nitalala ndani ya basi!

“Please don’t sleep in the bus, you will get tired, and you won’t enjoy your looong journet from there to Kigali, its tiresome…” alisema Janeth na alikuwa anamaanisha. Nilijua hivyo siku ya pili baada ya kufika Rusumo.

“I don’t have enough cash with me…” nilitaka kujitetea akanikatisha…

“Don’t worry, I will pay for you and you will refund me when we reach border or Kigali…”

Sikumwambia kuwa mie pale mpita njia tu naelekea DRC. Nadhani alidhani namie ni mmoja wa wanaoelekea kwenye “sabasaba yao” (trade fair) maana tarehe hizo kulikuwa na maonesho ya kibiashara hapo Kigali iliyoanza kama siku mbili zilizopita na inayotarajiwa kuwepo kwa siku kadhaa zijazo.

“Why spend a lot of money! We can share the room…” nilichombeza huku nikiwa simaanishi.

“…Really!?” alihoji

“Why not!” nikajikuta tu neno limenitoka.

Mazungumzo yaliendelea na akaniambia yeye hufikia Gaprena Hotel. Nikatafuta review ya hotel hiyo harakaharaka kwenye simu nikaona ni zile wanazoita hotel kumbe ni lodge tu iliyochangamka. Anyway, ni Hotel. Sifa kuu aliniambia kuwa pako salama na ni karibu na stendi kuu pia gharama ni ndogo kulinganisha na hadhi ya hoteli yenyewe. Mimi wakati huo nimeshasoma review kadhaa na kupata picha halisi ya sehemu anayotarajia kufikia.

Tukaingia mizani Kahama na baada ya kutoka hapo mhudumu alitutangazia ratiba ya gari na kutupatia elimu maelekezo na tahadhari. Moja ya maelekezo aliyotoa ni kwamba basi halitoendelea na safri hadi kesho saa kumi na mbili asubuhi, hivyo anashauri abiria watafute lodge za kupumzika kwa watakaopenda kufanya hizo, na wale watakao amua kulala ndani ya basi wawe makini na mizigo yao ya ndani ya basi maana ulinzi wa mali iliyo ndani ya basi ni wa abiria husika.

“Muwe makini na mutu mugeni yanakuja ndani ya basi, hakuna abiria naingia usiku huu…” alimalizia yule mhudumu na Kiswahili chake kibovu.

Gari ikakunja kulia moja kwa moja hadi stendi kuu. Stendi ilikuwa imechangamka sana na ilikuwa ni majira ya saa tatu hivi usiku. Watu wengi, wauza vyakula mama lishe wengi huku wakikaribisha wateja, wapiga debe wa lodge pia wengi wakijitahidi kutafuta wateja, hakika Kahama palikuwa pamechangamka sana.

Wahudumu wa basi tulikuwa nao safarini wote waliondoka akaja wakala mkazi wa hapo ambaye alikuwa akisimamia ‘shoo’ bila shaka na walinzi wao pia walikuwepo ingawaje sikuwaona mara moja.

Abiria walikuwa wanajivuta sana kushuka mimi na Janeth tukiwemo. Nusu saa baadaye tuliamua kutembea kuelekea hoteli ambayo abiria mwenzangu alikuwa ameweka nafasi. Bajaj, tax na bodaboda zilikuwepo, lakini tuliamua kunyoosha miguu baada ya safari ndefu.

Tulivyofika pale mapokezi tulikaribishwa kwa bashasha lakini ‘walinikata maini’ nilipoulizia kama kuna chumba…

“Ishi, kwani hampo pamoja!...” aling’aka yule mhudumu

“Vyumba vyote vimejaa, basi ngoja nikupeleke hoteli ya jirani na hapa, pale unaweza kupata ila bei ipo juu kidogo…” aliongea yule mhudumu kwa lafudhi ya kisukuma.

Janeth akaingilia kati…

“Lets share as you said, no problem… are you going to swallow me!?”

Yani hapa angalau kwenye uandishi inabidi nikinyooshe kidogo hivi vilugha vya watu maana jinsi alivyokuwa akiongea Janeth unaweza ukawa unacheka tu kila mara.

“Well, its okay, lets share the room and I promise will not swallow you…” tukawa tunacheka huku tukielekea chumba husika maana mwenzangu pale inaonekana ni mwenyeji.

======

INAENDELEA…

View attachment 2540333View attachment 2540338View attachment 2540341
 
Hii kanda ya wenye nayo Eroni afu sijui huwa kuna siri gani huku!! Sijui ni vyakula labda!!
Nilianza hekaheka nikiwa form 6 ila miaka yote hio umwagiliaji nilikuja kuukuta huku baada ya kuajiriwa yule Mwamba siwezi msahau[emoji41]!!
Weeeee
 
[emoji1787][emoji23][emoji38]
Hakika umenifanya na mimi nikatalii hadi Goma kabla ya kumaliza mwaka huu.

Nadhani mke Hamida ni Mmanga vile. Maana hakuna mwanamke anayeweza kukubali ukaoe mwingine. Kwa vile wao wamekulia katika mitala, hivyo haoni ni jambo la ajabu.

Pili hukupata shida kwa Janeth kwa vile alishavuka miaka ya kupenda (18-25) hiyo miaka binti anakuwa machachali, hasikii la mtu. Ila akifika 26 anaanza kufikiria ndoa na kujenga familia. Hivyo kwa wote wawili ulikuwa sex partner tu. Ndiyo maana ilikuwa ni rahisi kumface Hamida na pia wakakubali kutafuta wengine. Wewe kwao ulikuwa ni daraja la kufanyia biashara. Mwanamke akipenda ni hatari, nakumbuka kuna mwanamke mmoja alikuwa ananipenda yeye akiwa sekondari na mimi primary (kumbuka miaka hiyo unamuogopa mtu aliye sekondari, sikumla) hadi leo pamoja na kuwa na wajukuu bado ananipenda sana imagine.
 
Msimu wa tatu.

Season III

(a) Kukirimiwa ukwasi cha njia ya ajabu


Blaze (Blaise) ni kijana aliyekulia katika mazingira ya migodini huko nchini DRC, ni Kijana wa Kinyarwanda ambaye wazazi wake walikimbilia nchini Congo kufuatila machafuko ya kikabila. Wazazi wake wakajikuta wapo katika kazi ngumu ya kwenye machimbo ya migodi huko msituni Congo katika ile hali ya kutaka kujinasua na hali ngumu ya uchumi. Walikuwa wakitumikishwa kwa ujira mdogo kwa siku lakini hawakuwa na chaguo lingine bali kutumika.

Katika mazingira hayo wazazi hao baba yake na Blaze akajikuta ameanzisha uhusiano wa kipapenzi na mama yake Blaze na wakapata mtoto wa kiume waliye muita Blaise (Blaze). Baada ya mtoto wao huyo kuchipukia (kukuwa) naye akawa miongoni mwa wafanyakazi katika mgodi huo ambao ulikuwa na idadi kubwa ya watoto chini ya umri wa miaka kumi na minane na wachahe waliozidi umri huo kwa maana umri ukienda sana ni ngumu kwa mtu kuhimili mikiki mikiki ya kazi za migodini hapo.

Akiwa na miaka kumi na minne, Blaze alipatwa na msiba mzito wa kufiwa na wazazi wake. Siku hiyo wafanyakazi wengi mgodini hapo walifariki kwa kufukiwa na udongo uliotokana na mlipuko huko chini ambao inasemekana ulikuwa wa bahati mbaya maana ni kawaida yao kulipua kukiwa hakuna watu walio katika msafara wa kupandisha mchanga (udongo / mawe) wenye madini na kuupelea sehemu husika ambapo pia ni mbali na njia ni ya hatari ki miundombinu na kiusalama kutokana na wanyama na wadudu wakali msituni humo.

Ulikuwa na msiba mkubwa sana mgodini hapo, na Blaze mwenyewe anaelezea…

Ndio vile, tukaikala kwa muda, baada ya kutosha maiti zote zikafukiwa kwenye shimo moja kubwa kisha mgodi ukafunguliwa na kazi ikaanza tena.

Ilibidi kutumika tu juu hakukuwa na namna ya kupata kukula wala pa kukimbilia, nyumbani kwenye wazazi wangu walitoka sikujuage wala sijawahi kutoka nje ya njia za kazi za migodi.

Tulikuwa tunatosha michanga na mawe yenye ina madini ndani, sijui hata ilikuwa madini gani, tunabeba mu mukichwa ama kumugongo kupandisha nayo juu kisha kufuata njia kupeleka fasi ambapo barabara ya magari imeishia. Ni mbali Papaa, ukitoka leo utatembea mchana wote na usiku, ukichoka unalala tu popote ukiamka ndo unaenda hadi ufike fasi wameweka kambi unapata damashi (chakula) kidogo ndo uendelee tena hadi ufika fasi hiyo kuna magari.

Nilifanya kazi hii kwa sankanii (5 yrs) ndo Mungu akanitosha pale kwa ajabu kabisa. Siku yenye nimefika ile fasi ya kukuta magari yenye yanachukuwa michanga na kuondoka nayo, papaa mmoja akawaambia wenzake kuwa mimi naweza kufanya kazi ile wanaenda kutumikisha huko. Nilikuwa nipo byee niko na nguvu japo nilikuwa nimekonda kutokana na kazi ngumu na daamash (chakula) ndogo lakini nilikuwa byee.

Baadaye ndio nikajuwa kuwa kuna mtu alikuwa anatumika katika fasi hiyo ambayo sasa nitaenda kuishika juu yeye aligonjeka akaafriki. Tulipanda mu lori, na ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kupata gari, tukasafiri usiku na mchana hadi kufika fasi ingine ambako ndo kama kuna kiwanda. Papaa, ni porini huwezi kuona nyumba, ni kambi tu za wafanyakazi wachache na eapo (airport) ndogo yenye petite avion (ndge ndogo) zinakuja, zinakamata maudongo yenye tumeyaandaa na kuruka. Sijue kwenye wanapeleka.

Sasa nikapewa tente (tent) yenye huyo jamaa niliye chukuwa fasi yake niwe nakaa humo. Nikamshukuru Mungu kwa kunitoa kule porini ingawaje hapo palikuwa bado ni porini lakini kazi ngumu ya kupandisha maudongo hadi kufika usawa wa ardhi na kazi ya kutembea siku njiani hadi kufika pale fasi gari zinaishia ilikuwa nguma sana. Nikatumika hapo kwa makumi matatu (mwezi mmoja) nikagonjeka paludizme (malaria) nikashindwa kwenda mu kazi. Bakanipatia medicine (dawa) na kikawa nimepumzika mu tente.

Sasa vile nimelala mu tente nikaona sac ya nailon ndogo ndo nikasema nifungue nione. Kufungua nikaona ramani yenye imeonesha fasi watu banachimba madini na njia ya kupita hadi kufika ile fasi ya gari zinafika na barabara ya gari hadi kiwandani tulipo na njia tatu za kutoka kufika fasi nyingine. Nikairudisha nikaificha vizuri. Juu kwa vile nilikuwa sijui kusoma, papaa mie sikukwenda masomo tangia nizaliwe nipo tu migodini.

Nikiwa natumika hapo kiwandani, kwenye tulikuwa tunachuja na kutosha michanga na mawe kisha kugawa fasi tatu lakini kila fasi banaweka kwenye sac yake, na avio ikija inaondoka nayo, nikapata du amis (marafiki wawili) ambao wao walikuwa wakubwa kuliko mimi lakini mmoja ndiye alikuwa mkubwa zaidi kuliko sisi wawili. Tulikuwa tunatumika kwenye fasi ya kuchekecha udongo kwenye mashine ndo tukawa tunajuwana. Nikamweleza yule mwenzangu ambaye kidogo tunalingana umri kuhusu ramani, akawa na hamu ya kuiona.

Jioni ile tulienda kwenye tente yangu na tukawa tuniangalia, yule jamaa akasema hizi ni njia zenye zitatupeleka vijijini na moya itatupeleka hadi Fungurume ambako kuna mji. Tukawa tumefurahi na kuanza mipango ya kutoroka ili tuende huko mjini Fungurume. Yule jamaa yangu, Ferii, akaniambia tumshirikishe yule kaka mkubwa ambaye alikuwa shufel wa malori ya mgodi wa Mutanda ili tuone atatushauri vipi.

Baada ya kumshirikisha naye Jeremii akasema amechoka kutumika mu kazi za vumbi ndo alikuwa anakusanya faranga ili arudi Lubumbashi. Sasa timu ikawa imetimia na tukaanza mipango ya kutoroka eneo lile maana lilikuwa lina ulinzi mkali.

Baada ya siku kadhaa ya kupanga namna ya kuondoka pale, tukiongozwa na Papaa Jeremii tulifanikiwa kutoka usiku ule muda wa watu kulala ili kunapokucha tuwe tumefika mbali. Mimi nilikuwa na faranga kidogo juu kule huwezi kuweka akiba ya hela, unatumika na inaisha yote ili ubaki kutumia tena, lakini wenzangu waliokuwa hapo kiwandani Ferii na Jeremii wao walikuwa wana hela kiasi hivyo kuifanya safari yetu ya kutoroka iwe nyepesi.

Tulitembea usiku kucha hadi asubuhi tukafika stesheni ya reli. Hapo papa Jeremii akatuambia tumsubiri ili yeye akasome mazingira. Tulibaki pale kwa muda mrefu hadi njaa ikaanza kuuma sana na jua lilikuwa limesonga. Tukapitiwa na usingizi tukiwa tumekata tamaa ya kumuona tena Jeremii.

Bahati nzuri ilipofika mida ya jioni, papaa Jeremii alikuja, tulifurahi sana, juu alikuja na paa (mikate) na juis ndo tukapooza njaa pale kisha akatuambia tumfuate kwa kuacha hatua kadhaa yeye akiwa mbele. Tukasonga hadi fasi moja ndio tukakuta kamio (lori) ya kwenda Likasi. Kumbe alikuwa ameshafanya mipango yote, shufel akatuambie tuikale nyuma kwenye bodi na safari ikaanza kuelekea tusikokujua japo Jeremii alikuwa anasema kamio inaelekea mjini Likasi.

Njia haikuwa nzuri lakini tulifika Likasi neuf heures usiku (9pm) ndio tukashuka, yule shufel wala hakuitisha faranga labda Jeremii alimalizana naye. Jeremii akatuambia yeye ni mwenyeji hapo akatupeleka kwenye minzodot moya ya byee ( lodge) na tukaoga muzuri na kulala.

Asubuhi tukakamta kamio nyingine na kuelekea Lubumbshi ambapo ndio nyumbani kwa papa Jeremii. Nikaanza kutumika kuosha makamio ndo Napata faranga za byee na Ferii alitumika na papa Jeremii gari yenye Jeremii aliomba tumike nayo. Mimi nikaanza masomo ya jioni ili nipate kujua kusoma. Nikajisajili kwenye college yenye banafundisha mu anglee (English speaking school). Kila siku jioni nikawa masomo na baada ya simwaa (miezi sita) nikaweza kusoma kwa anglee.

Lengo langu la kujuwa kusoma likatimia vizuri baada ya mwaka mmoja ndio nikafungua ile ramani tena niliyotoka nayo kule mgodini kiwandani na kusoma upya, sasa nikaelewa vizuri. Inaonekana ile ramani yule kijana aliyekufa aliipata kutoka kwa mzungu aliye sahau mfuko ule pale jirani na sehemu yake ya kazi na yeye akauchukuwa, labda akidhani ndani kuna pesa au madini. Kuna karatasi nyingine ambayo iliambatanisha na ramani ambayo sikumwonesha Jeremii wa Ferii nikaitoa nayo na kuisoma na ndio ikawa chanzo cha mimi kupata mali hii unayo iona leo.

Ni kwamba kulikuwa na mawe yamefichwa jirani na ziwa Upemba. Kilomita chache kutoka ziwa hilo kuna machismo yam awe, lakini mawe hayo inaonekana kama yalichepushwa na kuhifadhia hapo kandokando ya ziwa.

Katika ila ramani kulikuwa na sehemu mbili ambzo zote kulifichwa madini, ikabidi niichore ile ramani upya ili kuonesha sehemu moja tu na kuficha baadhi ya taarifa za ziada. Ni kilomita zaidi ya 800 kutokea Lubumbashi na barabara si rafiki lakini pia ilionekana hakuna njia ya gari, wala baiskeli ama pikipiki kufika hapo ziwani moja kwa moja bali ni lazima kwanza upite kijiji cha Misa kisha ufuate mto unaoingiza maji ziwani Upemba na kwa kufuata ramani sehemu hizo mbili zenye madini fichwa zilikuwa zimetofautiana umbali wa kilomita moja hivi.

Nikaona hili zoezi siliwezi kulifanya mimi peke yangu, ikabidi nimshirikisha papa Jeremii na ferii ambao walikuwa wakitumika kwenye magari. Baada ya majadiliano ya muda mrefu tulipanga tufanye safari wakati wa kiangazi ambapo njia angalau inakuwa ipo vizuri. Miezi ya sita na wa saba ndio mvua huwa hakuna, tukapanga tukusanye hela kwa ajili ya safari hiyo isiyo na uhakika.

Nilikuwa nakaribia kutimiza miaka vantia (21yrs) ndipo tukawa na faranga za kutosha kufanya safri hivyo baada ya maandalizi ya miezi makumi sis (6 months). Ilituchukuwa juma moja hadi kufika mji mdogo unaoitwa Luena. Hapo tukapiga kambi na kujifanya tunauzisha biashara ya ice cream na keki mu majumba ya watu. Tulikuwa tunanunua kwenye bakery moja iliyopo hapo Luena na kuzungusha kuuza, lakini faida ilikuwa ndogo sana na wala malengo yetu hayakuwa kupata faida bali kuzoe kijiji na kupata usaidizi wa jinsi ya kufika kijiji kingine kiitwacho Misa.

Tukapata rafiki mwendesha boda boda maarufu hapo kijijini na kuomba atusaidie kutufikisha Misa. Baada ya ushawishi wa faranga kadhaa akakubali na maandalizi yakaanza, tulimwambia kuwa tunataka kwenda kujumuika na wavuvi wa samaki huko Misa. Baada ya maandalizi ya mikate na maji, tukaanza safari alfajiri ya siku iliyofuata ikiwa ni wiki moja tangia tufike hapo Luena. Tukamlipa ujira wake na kumwambia kila wiki awe anakuja hapo misa ili tumpatie samaka arudi nao Luena kuuzisha na hela atutunzie yeye huko huko Luena. Hii ilikuwa mbinu ya kujihakikishia usafiri mara baada ya kupata mali tuliyoikusudia. Lilikuwa wazo la papa Jeremii. Wazo la kuuza keki na Luena lilikuwa la Ferii mimi akili yangu yote ilikuwa inawaza mawe.

Ni mwendo wa siku nzima, mwendo wa tabu kwa pikipiki lakini kulikuwepo na njia ndefu ya kuzunguka njia ambayo tungetumia siku 5 kwa pikipiki kama alivyo tuleleza dereva wa motoo. Baada ya wiki moja kweli yule dereva wa motoo alikuja, bado hatukuwa tumeanza kuvua samaki lakini tayari tulishapata wenyeji wavuvi, tukampatia faranga za esensoo (mafuta ya pikipiki) ya kuja na kurudi na faranga kidogo ya ziada ili aje tena wiki ijayo. Tulichanganyika vyema pale kijijini Misa na tukaanza kazi ya kuvua samaki ziwani, wale wenyeji fungu lao walikuwa wanauzisha hapo hapo kijijini, sisi tulikuwa tunakausha na kusubiri shufel wa motoo aje tumpatie akauzisha kule Luena.

Ile ramani baada ya marekebisho nilimpatia papa Jeremii na mimi nikabaki na ramani halisi ambayo ilikuwa inaonesha njia zote kwa ufasaha hadi mawe hayo yalipofichwa. Tulipanga kwenye chumba kimoja cha mmoja ya wale wavuvi wenyeji na kuwekeana zamu ya mmoja kubaki nyumbani wakati wengine wameenda kuvua ili wakirudi wakute chakula tayari kimeandaliwa. Mpango huu ulikuwa ni wangu ili kutengeneza nafasi ya kuanza ufuatiliaji ya zile njia kisiri. Wiki ilikatika na yule shufel wa motoo alikuja na tukampatia samaki tulio kusanya akaondoka nao. Zamu yangu ilipofika hiyo wiki ya tatu nikafanya ziara ya kwenda kule kwenye mawe yaliyofichwa.

Nilifanikiwa kuziona pointi zote zenye hayo madini, lakini siku hiyo sikufanya chochote na kurudi nyumbani kuandaa chakula kwa ajili ya wenzangu. Nikarudia kuisoma ile ramani yenye maelezo ya ziada na nikagungua kumbe yale madini yaligawanywa sawa kwa sawa na kuhifadhiwa sehemu hizo tofauti labda kwa sababu ya usalama au sababu nyingine. Sehemu zote mbili kulikuwa kuna mti uliopandwa lakini ukionesha kabisa haukuwa wa asili ya eneo husika. Nikaanza kuwaza je endapo wahusika walirudi kuja kufuata mali zao! Sikujali wala sikuwa na la kufanya kwa wakati huo bali kuyaoga maji ambayo tayari nimeyavulia nguo.

Wiki ikaisha tena na yule shufel wa motoo akafika tukampatia samaki wengine wengi na akaondoka nao. Zamu yangu ya kubaki nyubani ikafika tena sasa tayari nilikuwa nimeshaandaa zana za kuchimbia chini kitu kama panga hivi na nondo iliyo chongoka. Walivyotoka tu kwenda ziwani na mimi nikatoka moja kwa moja hadi kule ambako kwenye ramani ambayo papa Jeremii hana na kuchimbua ule mti. Baadaya kuutoa, nilikuta chini kuna jiwe kubwa ambalo lilifunika mfuko wa ngozi mdogo. Nilipoufungua nikakuta ndani kuna mawe ya kijani na mekundu kadhaa ambayo hayajachongwa. Nilifurahi sana, nikatoboa sehemu ya suruali niliyovaa kwenye pindo na kuanza kuyasokomeza hayo madini kwenye mzunguko wa mkanda kisha nikavaa mkanda kwa juu na kufanya nionekane nipo kawaida tu. Ndani ya ule mfuko wa ngozi kulikuwa na karatasi ndogo nyingine yenye majina ya kizungu na namba za simu. Nikaichukuwa na kuihifadhi vizuri.

Jioni tulivyokuwa pamoja nikamwabia papaa Jeremii kuwa nilitembea hadi sehemu yenye mawe na kuwa nimepaona. Ajabu na yeye akaniambia ameshapaona lakini Ferii yeye hakuwa ameenda kuangalia. Siku ya zamu ya papa Jeremii kubaki naye akaenda kule na jioni yake akarudi na mfuko wa ngozi kama ule ambao mimi niliutupa mtoni, lakini mawe aliyokuja nayo hayakuwa mengi kama yale niliyokuta mimi. Nikajuwa tu huyu amejisevia mengine pasipo julikana. Hata hivyo vipande vilikuwa vingi na pale pale tukaamua kugawana sawa kwa sawa ili kila mmoja awe ameshika mali yake. Tulifurahi sana kuwa safari yetu imezaa matunda. Samaki tuliokusanya wiki hiyo wote tukawauza hapo hapo kijijini na motoo ilipokuja tulipanda mishikaki kama kawaida kurudi mjini (kijijini) Luena.

Tukafanya hesabu ya mauzo ya samaki na mauzo ya wiki moja tukamwachia yote yule shufel wa moto na kumuomba atusindikize hadi Lukasi ili tukanunue vifaa vya uvuvi wa kisasa (tulimdanganya). Tukafika Lukasi baada ya safari ndefu na kuagana na shufel wa motoo na kumbuambia tutarudi wenyewe kwa kuwa ni mbali asipate shida kutufuata. Pale Lukasi Papa Jeremii alikuwa ni mwenyeji hivyo akashauri tuchange jiwe moja moja ili tuuzishe pale kwa wanunuzi wanao langua madini. Dooo tulipata dola nyingi na kufurahi licha ya mnunuaji kudai sijui zimepigwa na radi sijui hazina ubora. Tulilala pazuri siku hiyo na kununua nguo nzuri na kula vizuri tukiwa na furaha na kupanga siku ya pili kukamata kamio kurudi Lubumbashi. Tulivyofika Lubumbashi tulikubaliana kila mtu auze mali yake kivyake vyake, na wote watatu tukanunua telephone ntelijio (smartphone) na kubadilishana namba za simu.

Kwakuwa tayari nilikuwa naweza kusoma anglee (English) na kuspikee french byee nilitafuta habari kuhusu wanunuzi wa madini haya ya kijani na mekundu ambayo sasa niliyajuwa kuwa na rubi na emorod. (Ruby & Emerald). Kwanza nikaita zile numeroo za kwenye zile karatasi hazikuitika. Lakini nikaja kujuwa baadaye kuwa nchini Zambia kuna mji wanaitwa Kabwe kuna wazungu wenye wanalangua madini. Nikaamua kufunga safari kuelekea Zambia. Pale boda nikapata makaratasi ya kuvukia. Nilidandia makamio hadi nikafika Kapiri ndo nikakamata basi kwenda Kabwe.

Nikauzisha mawe matatu kama majaribio nikapata dola nyingi sana lakini nikiangalia kwenye telephon bei naona bado wamenipunja. Nikaendalea kukaa hapo kabwe hotelini juu nilikuwa na dola za kutosha na kufanya utafiti wapi nitauzisha mzigo wangu kwa bei nzuri. Nikaja kujuwa kwenye boda ya Tanzania na Congo kuna wenye wanalangua, Dar es Salaam na Tunduru Tanzania. Ndio nikakamata basi hadi Nakonde. Pale nikavuka kwa msaada wa motoo usiku wa manane juu sikuwa na paspo ya byee.

Nikataka kwanza niende Rwanda nione nchi yenye wazazi wangu walitokeaga, nawasukuru sana Watanzania wa pale Tunduma kwa kunipa muongozo wa kufika Rwanda kwa urahisi kwamba kwanza nifike Dar es Salame ubalozi wa Congo ndo pale nitapata mambo yote juu vile nitafanya. Kwakuwa nilikuwa na dola nyingi sana sikuwa na wasiwasi na bado nilikuwa na yale mawe ya kiunoni ambayo bado nilikuwa sijayagusa.
==

Nilitosha dola nyingi nikapata paspo ya Congo yenye imeonesha nimekuja Tanzania kutokea Kinshasa kwa kupitia eapo ya Dar na visa yam waka mmoja. Hata sijui waliwezaje wale watu wa pale Upanga lakini muhimu sasa nilikuwa na paspoo ya byee. Ndio nikasafiri nayo kwa ndege kwenda Kigali na kuanza kuulizia kwenye ukoo wetu wanatokaga, wakasema ukoo huo ni Banyamulenge nikaona isiwe tabu bora niachane na kutafuta wandugu bali niendelee na mpango wa kuuzisha mawe yangu ili nifanye biashara ya byee yenye itaniingizia hela za kila siku.

Dar es salame nikazunguka fasi zote zenye wamesema wanalanguaga gems, Mikocheni, Kinondoni Moroco, Masaki na Kariakoo lakini kote nimekuta wenye wanapiga watu lakini angalau waThailand walikuwa wana bei muzuri lakini kabla sijataka kuwauzia ndio nikaona nisafir kwenda Tunduru. Nikafika hadi machimboni na kuona wapi wanapeleka kuuza na nikajuwa bei zao pale angalau ilikuwa bei nzuri. Nikawauliza wapi wao huuza madini yao lakini hawakuniambia, nikawambia kuwa kuna jamaa zangu wako Congo wana madini hayo mengi wanataka kuuza, nikawatolea na sampo jiwe moja…

Yule jamaa (alikuwa mswahili) akaliangaliaaa, akalimulika na tochi, mara akalipima kwenye mashine kisha akaniuliza kwamba hao jamaa zangu wanayo mengi kiasi gani, nimakjibu kuwa sijui lakini ndio wamenipa sampo hii. Akanipatia namba niende Dar nikifika nimtafute huyo mwenye namba hiyo. Nikahitimisha safari yangu na kurudi Dar na kukutana na mwenye namba hiyo ambaye alikuwa ni mhindi. Mara ya kwanza alinialika hotelini sea cliff na kuangalia sampo, huyu nikampa mawe mawili la kijani na jekundu. Alivyoyaona akawa kama amevurugikiwa hivi na kuniuliza yapo mengi kiasi gani. Nikamjibu kuwa sijui lakini wanataka uhakika wa bei nzuri. Akasema kuwa atanipa bei nzuri sana maana hayo madini ni safi sana hayajachomwa wala hayajachongwa, akayapima mara tatu tatu pale kisha akaniomba namba ya akaunti ili afanye muamala palepale. Nilipomuuliza kwa bei gani ndipo nilishangaa na kuona ni kiasi kukubwa cha pesa ambayo sikuwahi kushika maishani na wala nikichanga madini yote niliyoyauza kule Lukasi, Lubumbashi na Kabwe haifikii kwa mawe haya mawili niliyouza.

Roho yangu sasa ikaridhika na bei hii sikutaka makubwa zaidi. Nikampa namba ya account ya Exim bank niliyofungua Kabwe Zambia. Akafanya muamala na pale pale nikapata notification kwenye simu yangu. Tukapeana mikono na akanipa namba nyingine mzigo ukifika Tanzania nimpigie kwa namba hiyo. Nilifurahi sana siku hiyo na kuona Mungu kweli hamtupi mja wake.

Katka matembezi yangu Dar es Salaam kwenye kumbi kadhaa za starehe ndio nikakutana na madame mmoja tukawa tunaishi byee hotelini lakini akashauri tununue nyumba Sinza, tukawa tunaishi wote lakini kumbe alikuwa ni mwizi. Akaniletea majambazi wakanidhulumu nyumba ya sinza wakachukuwa na dola mia nane zilikuwaga ndani.

Nikapata madame mwingine yeye akanishauri nijenge nyumba mbezi, nikamwambia siwezi kusubiri bora kununua, ndio nikanunua mansion ya byee Mbezi beach na nika chanjee jina ya hati mu jina yangu lakini tulikuwa hatukai kwenye nyumba hiyo, tuliipangisha na sisi tulipanga apartment Masaki. Kipindi cha covid yule madame aligonjeka akaondoka kwenda kwao Moshi, hakurudi na numero yake haiiti tena. Sasa niko peke, nimehamia kwenye nyumba yangu ya Mbezi baada ya mkataba na mpangaji kwisha nikamwambia nataka kuishi mwenyewe, ndo vile naishi Mbezi beach sasa.

Nimefungua biashara yangu ya kununua magari na kuuza. Nina yadi ndogo Mikocheni, nikitosha magari bandarini yanafika Mikocheni kisha yanaenda Rwanda, Burundi na Congo ambako wateja wangu wengi wapo huko. Niko sasa na miaka vant nef (34yrs), nimetumika Tanzania sasa miaka duzoo (12yrs) na sikuwa na uhusiano na wanawake mpaka nilivyofikisha miaka 26 wakati nimeshauzisha madini yangu yote, faranga ziko kwa beki tatu tofauti, moja Zambia moja hapa Dar es Salaame na moja Kigali.

Tunawasiliana na Ferii, yeye alikamata makamio ndio anatumika nayo, ni tajiri yupo Lubumbashi na Papa Jeremii siku ziliposonga numeroo yake haikupatikana lakini naye aliuzisha mawe yake akanunua makamio ya mingi yakawa yantumika huko kwenye kubeba makopa (shaba).

Nilifanya uchunguzi nikagundua kumbe kule Misa kuna mgodi mkubwa wa Rubi na vito vingine na huenda yale mawe yaliibwa na kufichwa ili baadaye waje wayachukuwe wauzishe, lakini ile ramani ikaangukia mikonono mwangu kupitia kwa marehemu. Zile namba za kwenye ile karatasi sijui ndio zilikuwa za mnunuaji au zilikuwa za mhusika mwenye madini, hata wa leo sijuage.
===

Hayo yalikuwa maelezo ya Papa Blaze ambaye alimuona Bosio kwenye moja ya hoteli alizokuwa akienda kujiburudisha akija Dar es Salaam na kumtokea ili aanzishe uhusiano. Bosio alivyolifikisha suala lake kwetu (mimi na Hamida) ndio tukafanya kikao naye ili tupate kumjuwa vizuri ndio akafunguka kama nilivyoeleza hapo juu kwa kifupi, maana alisimulia kwa kirefu sana. Sote tuliridhika kwa maelezo yake, tukafanya uchunguzi kiasi kutaka kujuwa ukweli wa aliyosema kuanzia mpaka wa Tunduma, Ubalozi wa DRC Dar es Salaam na na ubalozi wa Rwanda hapa Dar na tukaridhika kuwa amesema kweli.

Hamida akaongea na Bosio na kumweleza kuwa aliyo ongea Papa Blaze ni ya kweli na kwamba amepata mchumba aliyepitia hali ngumu hivyo wanaweza kujenga uhusiano ulio imara....

ITAENDELEA...
 

Attachments

  • RDCCM1.mp4
    18.5 MB
  • RR2.jpg
    RR2.jpg
    13.3 KB · Views: 64
  • GE1.jpg
    GE1.jpg
    59.1 KB · Views: 49
  • RR1.jpg
    RR1.jpg
    32.6 KB · Views: 47
  • CE2.jpg
    CE2.jpg
    25.8 KB · Views: 49
(b) Zari la mentali

Hayo yalikuwa maelezo ya Papa Blaze ambaye alimuona Bosio kwenye moja ya hoteli alizokuwa akienda kujiburudisha akija Dar es Salaam na kumtokea ili aanzishe uhusiano. Bosio alivyolifikisha suala lake kwetu (mimi na Hamida) ndio tukafanya kikao naye ili tupate kumjuwa vizuri ndio akafunguka kama nilivyoeleza hapo juu kwa kifupi, maana alisimulia kwa kirefu sana. Sote tuliridhika kwa maelezo yake, tukafanya uchunguzi kiasi kutaka kujuwa ukweli wa aliyosema kuanzia mpaka wa Tunduma, Ubalozi wa DRC Dar es Salaam na na ubalozi wa Rwanda hapa Dar na tukaridhika kuwa amesema kweli.

Hamida akaongea na Bosio na kumweleza kuwa aliyo ongea Papa Blaze ni ya kweli na kwamba amepata mchumba aliyepitia hali ngumu hivyo wanaweza kujenga uhusiano ulio imara.

Taratibu za kufikisha barua ya posa Kishasa zikaendelea.

Aidha kwa upande wa Janeth alipitia kashkash kadhaa lakini wote baada ya uchunguzi ilionekana hawakidhi vigezo…

Kuna aliyejaribu kuligonga gari lake (gari yangu niliyompa atumie akiwa Dar) ili tu apate nafasi ya kubadilishana namba kisha kuwa karibu wakati wa matengenezo ya gari na hatimaye kutaka kuanzisha uhusiano…

Huyu kijana alikuwa ni mtoto wa mwanasiasa mkubwa nchini lakini baada ya uchunguzi ilionekana anajihusisha na magenge ya kihalifu, akapigwa chini.

Kuna Mchungaji ambaye alifiwa na mke miezi kadhaa iliyopita (wakati huo), akitokea kanisa lingine la dhehebu hilohilo, bila shaka alipata taarifa za uwepo wa Janeth kutoka kanisa analosali, lakini baada ya uchunguzi ilionekana amezalisha waumini wasiopungua wawili wa kanisa lake na afya yake pia ilikuwa ina mashaka, akapigwa chini.

Kuna waumini kadhaa wa kanisa alilokuwa akisali walijitokeza lakini wote hawakuionesha subira ama nia ya dhati ya kutaka kuoa bali kushiriki tendo tu, wengine eti Janeth ashike ujauzito kwanza kisha taratibu zingine zifuate, walipigwa chini.

Bahati ikaangukia kwa kijana Dikolu ambaye walikutana kule gereji ambako Alphard ilipelekwa kwa ajili ya kunyooshwa ilipogongwa na baladhuli yule, huyu kijana alikuwa na fundi makanika wa ile gereji (kapuni), ingawaje hakuhusika katika kulirudisha lile gari katika hali yake ya kawaida, lakini alionekana hapo akiendelea na kazi zake za kila siku. Dikolu alikuwa ni mrefu na aliyejazia misuli na kifua kama wafanya mazoezi ya viungo, nadhani ni kutokana na kazi za ufundi lakini bila shaka alikuwa ni mfanya mazoezi.

Dikolu alikuwa ni kijana mwenye umri usiozidi thelathini na miwili, ni mchaga aliyetokea eneo la Kishimundu na kuja Dar miaka kumi na tano iliypoita akitokea Moshi. Alikuja mara tu baada ya kufeli kidato cha pili na kufukuzwa nyumbani kwao, akaamua kuja Dar kujibanza kwa kaka yake ambaye alikuwa dereva wa daladala. Kwa vile alikuwa anapenda mambo ya ufundi magari, kaka yake aliona asipoteze hela kumsomesha sekondari bali alimpeleka gereji anapofanyia sevisi daladala lake ili aanzie hapo kujifunza mambo ya ufundi.

Baada ya mwaka mmoja kukaa gereji kaka yake aliamua ampeleke Chang’ombe veta ili apate mafunzo rasmi ya darasani. Alifaulu vizuri trade test grade III na kurudi pale gereji kuendeleza ufundi kwa vitendo ambapo akapata umaarufu sana kutokana na bidii ya kazi pamoja na kazi nzuri azifanyazo za kutengeneza magari. Baada ya mwaka mmoja mwingine wa kufanya kazi, yeye mwenyewe aliamua kurudi veta ili kusoma na kufanya trade test grade II ili aweze kuwa na ujuzi wenye uhakika na kutambulika zaidi. Kweli baada ya kurudi mtaani aliendelea na kazi lakini kaka yake akaona sasa mdogo wake amevuka daraja la kufanyia kazi ‘uchochoroni’ hivyo akamtafutia nafasi katika gereji kubwa maarufu ambako ndipo alipoonekana na Janeth.

Nilishangaa sana siku naangalia service card ya gari ya Janeth nikakuta ni ya gereji nyingine na siyo ile niliyozoea, kumbe ilipofika muda wa kufanyia sevisi gari alirudi pale gereji lilipo nyooshwa gari kwa ajili ya kazi ya sevisi ya kawaida ya gari.
===

Kufupisha stori ni kwamba, siku nyingine Janeth alimuomba fundi huyo aliendeshe gari na kuisikiliza maana ilikuwa inatoa mvumo sio wa kawaida. Ni kweli gari ilikuwa inahitajia kubadilishwa ‘wheel bearing’ za mbele, lakini pia Janeth alitumia nafasi hiyo kumtega Dikolu na Jamaa uvumilivu ukamshida wakajikuta wamebusiana.

Siku nyingine wakajitafutia nafasi wakazungumza wee ndipo sisi tukaletewa taarifa kuwa kuna kijana Dikolu ambaye anataka kuleta posa.

Baada ya uchunguzi tuligundua kuwa ni kweli Dikolu ni mzaliwa wa Kishimundu, lakini tayari walikuwa wameshayaweka sawa masuala ya kufukuzana nyumbani na wazazi kusema walikuwa wanampa akili kwa njia ya vitendo, kaka yake alikiri juu ya utulivu wa mdogo wake katika kazi na masuala mazima ya maisha, na Dikolu mwenyewe alisema hakujihusisha na masuala ya mapenzi lakini alikuwa mteja wa ‘ambiance’ siku mojamoja akizidiwa maana kwa mujibu wake alikuwa hapati ‘kichwa kuuma’ wala kuwa mtumwa wa kutoa pesa mara kwa mara kama angeanzisha uhusiano na alikuwa anajilinda vizuri na magonjwa yaambukizayo kwa njia ya kujamiiana.

Vipimo vikafanyika kwa wote inaonekana wapo salama, wakaendeleza uhusiano wao ili wazidi kufahamiana na baada ya miezi mitatu kupita Janeth alirudi tena na vipimo vikafanyika na wote wakawa salama. Taratibu za kupeleka posa Kigali zikabarikiwa.
===

Mzee mzima nikapata hekaheka ya ku-‘host’ kitu kilichoitwa ‘pre wedding ceremony ‘ ambapo Bosio na Janeth wote walikuwa ni ma bibi harusi watarajiwa, tuliwaalika wajomba wa Bosio na Baba zake wakubwa na wadogo, pia familia ya Janeth kutoka Kigali ilihudhuria na ndugu na marafiki wa familia za Dikolu na Papa Blaze walihudhuria na kufanya msisimko wa aina yake jijini sherehe iliyofanyika katika moja ya kumbi maarufu jijini Dar.

Baaya ya wiki chache kupita mimi na Hamida tukashiriki ndoa jijini Kigali, Bosio pia alikuja yeye pamoja na mtarajiwa wake na wiki mbili zilizofuata tukashuhudia sherehe matata jijini Kinshasa kwenye ndoa ya Bosio na Papaa Blaze ambapo pia Janeth na mumewe Dikolu walihudhuria.
===

Janeth na Bosio wote muda huu wana watoto wachanga chini ya mwaka mmoja. Urafiki wa Tanzania, Rwanda na Congo DR ‘ukaimarika’ kwa kuunganisha familia hizo, Bosio alihamishia makazi yake ya kudumu Mbezi Dar es Salaam kwa mumewe, watoto wakewakubwa waliendelea kubaki Kishasa kwa kuwa bado wapo wanasoma lakini huja wakati wa likizo kumsalimia mama yao, Janeth na Dikolu walinunua uwanja maeneo ya Kimara Dar es Salaam na ujenzi unaendelea, biashara ya duka kule Kigali amewachia wadogo zake na yeye amefungua 'boutique’ nyingine kubwa hapa Dar es Salaam na ameanza kuagiza mizigo ya dukani kwake na kwa wadogo zake moja kwa moja kutokea Uturudi na Thailand.

Furaha imetujaa moyoni kwa kufanikisha furaha za mabinti hawa wa Kigali na Congo DR. Hekaheka zitaongezeka nyumbani kwangu maana wajukuu wanazidi kuongezeka na ikifika msimu wa kushambulia mapera hekaheka za mchezo wa maliwato zitamkuta Hamida akiwasaidia wajukuu zake.
===




MWISHO.



Nimelazimika kuifupisha kwa sababu ya mabadiliko ya ghafla ya ratiba zangu.
 

Attachments

  • guav1.jpg
    guav1.jpg
    17.3 KB · Views: 49
  • WEDDRDC1.jpg
    WEDDRDC1.jpg
    677 KB · Views: 53
  • WEDDRWA1.jpeg
    WEDDRWA1.jpeg
    120.4 KB · Views: 51
  • JWC1.jpg
    JWC1.jpg
    35.1 KB · Views: 58
  • DK1.jpg
    DK1.jpg
    343.8 KB · Views: 54
  • BC3.jpeg
    BC3.jpeg
    10 KB · Views: 48
  • BC2.jpeg
    BC2.jpeg
    8.9 KB · Views: 45
  • guav2.jpg
    guav2.jpg
    31.5 KB · Views: 46
Hakika nikistaafu nami nashika njia ya [emoji1206] mpaka DRC [emoji1787]
Mkuu, usisubiri hadi ustaafu.

Kama hujaoa bado tembelea sasa. Lakini angalizo usiwe na papara maana kule ni kama restaurant, unaweza kuagiza chakula lakini kila ukigeuza shingo kuagalia walivyo agiza wenzako utaona ndio vizuri.

Hivyo chukua muda kusoma 'menu'.
 
Back
Top Bottom